Ulikuwa unafanya nini ukiwa na miaka 16?

Ulikuwa unafanya nini ukiwa na miaka 16?

Katika umri huu nilikuwa naupiga mpira haswaaa na unanitiii......kipaji changu kilimezwa na mfumo wetu wa elimu dah.....
 
Kuna mtu kaniambia et ww ulikuwa kiongoz wa UMISETA
Hahaha.

Na mnavyokuwaga na madharau sasa viongozi wa UKWATA wa kike.

Hata usemeshwe..utongozwe utamwangalia mtu kwa dharau huku ukisonya kwa vifungu vya Biblia. Utafikiri mpo Mbinguni.
 
umri huo tulikuwa tunasoma uyo dogo hata ukimuuliza maana ya democracy hawezi kuitaja
 
Nilikua nakimbizana na Kenyaman mixer Master Maebe bila kumsahau Afande Steve pale makongo secondary. Kula sana rojo na juis ya miwa.
 
Huyu dogo, Ansu Fati,ana umri wa miaka 16. Tayari anachezea Barcelona na amefunga goli na kuwa mchezaji mdogo kupita wote kuwahi kufunga goli pale Barca.

Sasa usiniulize nilikuwa nafanya nini nikiwa na miaka 16. Ninachokumbuka nilikuwa bingwa wa kuangua zambarau. [emoji28][emoji28][emoji2365] View attachment 1195167
Nilikuwa form one Shinyanga mjini shule niliyosoma inabaki kuwa siri.
 
Kidato cha pili, ila neno characteristics likinishinda kutamka.
 
Back
Top Bottom