Ulikuwa unafanya nini ukiwa na miaka 16?

Ulikuwa unafanya nini ukiwa na miaka 16?

16 yrs old, ndo mwanzo wa kuingia kwenye makundi ya wacheza martial arts mtaani, yaani muda wote wahuni nipo nao ni mchezo wa kupiga poomse/styles tofauti za kung fu bila kusahau shotokan karate aisee ila imenijenga sana mpka leo sijutii kuwa na wale wahuni.
 
16 yrs old, ndo mwanzo wa kuingia kwenye makundi ya wacheza martial arts mtaani, yaani muda wote wahuni nipo nao ni mchezo wa kupiga poomse/styles tofauti za kung fu bila kusahau shotokan karate aisee ila imenijenga sana mpka leo sijutii kuwa na wale wahuni.
Hayo mambo nlianza nkiwa na miaka kumi
 
A) Nilikuwa Kidato cha tatu Napamba na Mwalimu ***** wa Kiswahili huku Fundisha yake ya Mjengo Wa Tungo & Uhakiki Wa Fasihi Andish nikiwa Simpati,Nimechezea Viboko vya hapa na pale kwa kukimbia majaribio yakee oooohh Shiit.


B) Kipindi hichi ndicho niliianza kuonja Viroba (Zed) Nilikuwa na Mabrother Wahuni Wahuni Walikuwa wakinywa wakati mwingine Wakinishawishi lakini mimi nilikataa katakata,
Siku moja isiyo na jina nikafikiria nini tamu ya kilevi,Nikaanza taratibu ya kujaribu nikiwa Peke yangu nikiwa nijificha.

Weekend Moja nikanunua 500tsh kiroba nikajirupua,Mwanzo Machungu nilikunywa robo nikabwaga yaliyobaki lakini kile kidogo kikanipa stimu confidence,lahaula nikawa mpya kabisa ukichanganya na balehe(Ujana) nikasema hapa yule mtoto mwarabu wa Isevya hachomoki nitamwaga full mashairi yaliyo jaa kisado...Aaawapi

Nikawa nakunywa kila weekend maganda ya viroba natupa chini ya uvungu yakawa kibao siku mabroo wanafunua down wanakuta miganda kibao,Wanauliza vipi kulikoni Nami niwakajibu labda niwaulize nyinyi (Moyoni Tayari Bwege kakamatwa Mfano Wafala aliyefumwa akipata Uroda Demu kiganja).


C) Nilikuwa na Simu Ya Nokia Simu yangu yapili(Mwanafunzi Kidato cha tatu) Sasa kulikuwa na binti alikuwa ananinikubali (Ujana) lakini anashindwa kunitell live,akanambia Niazame simu yako kisha wakati wakunirudishia akaandika kwa simu "I LOvE YOU ALISINA" basi kijana nikafanye kweli kama yale yafanyavyo na baba & mama basi ikawa raha ndani ya Utamu Uwiiiiiiiiiiii kiiitikio chakeee binti yule.


"Ama Kweli Bongo Motoni"
 
16 yrs ilikuwa 1997,Tulikuwa tunakatazwa kucheza Mpira tuliambiwa kuwa tutavunjika.
Tuliambiwa tusome Mpira hauna maana .
Tulisoma mfecane war, Zanzibar revolution, why Egypt is Nile and nile is Egypt discuss 20 marks.
 
Nilikua kidato Cha 3 Jangwani.. nawaza kutoroka shule nikasagule mitumba karume
 
Dah.....ndiyo nilijaribu molotov yangu ya kwanza ambayo ilileta tafrani kitaani [emoji2960]
 
Nilikuwa std 4 na monita na nilikuwa mdogo kuliko wote darasani
Miaka 16 std 4, bila shaka ulisoma enzi za utawala awamu ya kwanza au ya pili. Halafu eti we ndo mdogo class hahaaaaaaa
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Nilikuwa bingwa wa kutega ndege kipindi hicho. Dah enzi hizo mtabe wa kutumia ulimbo wa miti ya kisamvu mpira natumia kumbikumbi kama chambo.
 
Umri huo hapo Popatlal Sec School ilikuwa ni kukimbizana na Mr Ghalibu na Mr Mussa waalimu walikuwa wanapenda sifa hao, hasa ikiwa zamu yao.
 
Nakumbuka nilikuwa nimemeza classification topic yote, ulikuwa ukiuliza nomenclature ya kiumbe yeyote nakujibu
 
Back
Top Bottom