Ulikuwa na ndoto gani ulipokuwa mtoto na ziliishia wapi?

Deadbody

JF-Expert Member
May 30, 2015
4,276
6,585
1573576261911.png
 
Kiutoto utoto unatamani almost kila unachoona watu wa karibu wanafanya

Kuwa DJ mana nili/napenda sana mziki na clubbing
Kutumikia kanisa,vile nikienda kanisani naona mchungaji pale mbele natamaniiiii
Kuwa muigizaji
Kuwa engineer ,nikafight weeeeeee nikamilishe ndoto yangu until Olevel mambo yalivyoenda tofauti na matarajio

Kwa sasa niko mbali sana na ndoto zangu,haipo hata moja niliyokamilisha hapo
 
Wengine maisha yetu kama kunguru tunaishi tu ndoto zilishakufaga kitambo muhimu kuishi tu na kutengeneza generation itayokuwa bora na kuhakikisha wakafanikiwa zaidi katika kutimiza ndoto zao.
 
Mimi nilipokuwa mtoto sikuwa na ndoto yoyote kubwa, kwa kuwa mimi ni mwanamke nilikuwa nafikiria ipo siku nitakuwa na mume na watoto. Nilipofika sekondari nilitamani sana kada ya sheria na nikaazimia kusoma sheria, sikusomea hiyo ila mpaka kesho nawatamani wanasheria ....yaani hakuna watu naonaga maisha wameyapatia kama wanasheria
 
Back
Top Bottom