Pyepyepye
JF-Expert Member
- Jan 6, 2017
- 1,940
- 3,857
Miaka kadhaa iliyopita, mjomba wangu niliyekuwa nikiishi kwake, aliniahidi kulipa gharama zote za chuo, nilikuwa nashughulikia michakato ya kutafuta uwezesho wa kuendelea na masomo, lakini baada ya kauli ile nikaacha kila kitu na kumsubiri yeye.
Pesa aliyoitegemea ilikuwa ya mkopo, siku ya siku mkopo ukaingia, akaniita akanieleza na kuniambia nimsindikize benki akachukue pesa, tuliongozana hadi benki akachukua pesa, tukarudi home
Siku tatu baadae, niliona mjomba anaboresha sebule kwa kununua samani (ikumbukwe kipindi hicho nilikuwa naishi kwake) na vitu vingine vingi, jioni ya siku ile mjomba aliniita na kuniambia "Natamani sana kukusaidia, lakini siwezi kuharibu mahusiano yangu na mke wangu kwa ajili yako, Mama Japhe ameshauri hizi pesa tununue vitu na kama ulivyoona tumeshanunua, wewe fanya utaratibu mwingine"
Ulishawahi katishwa tamaa na yule uliyemtegemea kabisa?
Hebu tupe uzoefu wako katika hili.