Ulianzaje kukaa gheto?

😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂
 
Aisee hatari,soon baada ya kumaliza chuo way back 2014 nikarudi home nikajaribu mishe za maskani ikawa chenga na maneno mengi ya maudhi,nikauza pc nikazama Dar kuna mwana akanipokea

baada ya mwezi wa kutafuta ramani mshikaji kaniunganisha kazi alipokuwa anafanyia salary 270,000 per month nikapiga kaz by septemba 2015 kibarua kikaota nyasi kampuni ilifilisika mfukoni nina 1,200,000 jamaa akasema saiz kila mtu aangalie namna ya kujisaidia

Nikapiga akili mambo magumu had pesa ikakata hiyo ni may mwaka uliofuata,nikarudisha mpira kwa kipa tena kwa nauli ya kusaidiwa na mdau tuliyefahamiana tuu.Maskani michosho mingi kuna siku nikagoma kufanya ishu fulani fulani wakanitimua nikapanda gari hadi swax,alikuwepo mwana fulani home nilitoka na 60,000 baada ya kulipa nauli nikabakiwa na 40,000 hapo hakuna anayejua nikikokwenda.
Nikamkuta mwana akanipokea nikamwambia nimekuja kusaka life kazi yoyote ntafanya.jamaa akasema utakula ila pia kulala tafuta geto,ndo ikawa mara ya kwanza nimeanza kupanga hiyo ni june 2016 hapo godoro ni mabox mimi na ndoo moja tu ndo kiti hicho.

Asubuhi nawahi kwenda kwenye vibarua jioni nakula kwa mshikaji nachagua nikipata.Baridi yote iliniishia maana nilikuwa na shuka tu na sakafu ya baridi,mwezi wa kumi baada ya kudunduliza nikanunua godoro na vyombo vichache vya kuanzia maisha.Ilifika kipindi hali ikawa ngumu sana sometime hakuna kazi unashindia miwa na bumunda tuu huku unawaza kodi na bili za maji na umeme,kodi ilikuwa 12,000 umeme 1000 na maji 2000 jumla 15,000 lakini inasumbua.

Piga sana kazi za zege na saidia fundi kutwa 5000 ila ndo hivyo lazima maisha yaende

By Novemba 2016 Mungu saidia kuna mwana akanifanyia connection ya kazi za ukandarasi ambazo ndio fani yangu from there hadi leo hii ndio nilipata nafuu ya maisha japo ni kazi za muda zinaishia zinakuja tena so wanaofanya kazi kwa wakandarasi wanaelewa.

Pamoja na kwamba sijatoboa niko kwenye nafuu maana nina familia na nina boma siku yoyote ntahamia kwangu

Ila kitu sitosahau nilipata tabu sana na ishu iliyonisikitisha nilipata demu nikamketa geto baada ya kuona jinsi lilivyochoka hakutaka kukaa na kuanzia hapo akaniblock.Wakati fulani pia nikiwa kwenye ukidampa kuna demu alinielewa but wenzie walimponda eti ntampa pesa gani wakati nashindia ukidampa nae akasepa nikaacha kabisa kutokea mademu
 
mi Niko mbioni...kukaaa ghetooo kikubwa uzima
 
Hahah dah hawa viumbe hawataki Shida..pole sana mkuu na hongera sana kwa struggle..kutoka hom inatakiwa uwe mbish kwel ,ila ndio njia ya kujitegemea
 
Hahah dah hawa viumbe hawataki Shida..pole sana mkuu na hongera sana kwa struggle..kutoka hom inatakiwa uwe mbish kwel ,ila ndio njia ya kujitegemea
Unfortunately walisahau kwamba siku huwa zinatofautiana jana sio leo,hadi leo hii kwa upande wao mambo sio mazuri na wameshazalishwa ndo wamechoka hadi huruma
 
WANAGETTO NISAIDIENI NIPATE CHUMBA MAENEO HAYA MAANA MADALALI WANATUKAMUA SANA
-Anayejua chumba maeneo ya Mabibo hostel,sinza,changanyikeni,survey,makongo juu,ubungo external,mwenge na riverside....
Budget yangu ni cha 40k au 50k kwa mwezi...
Tusaidiana na wanaotafuta vyumba maeneo hayo pia...

Nipm nipigie au nitext kwa namba 0759432654
 
Siku ya kwanza kuhamia kwangu, nakumbuka nililala chini kwenye tiles, nilikuwa nimeshafanya usafi nikasogea kula bata maeneo ya sinza mpaka saa 8 usiku, nikiwa nnarudi home kwa wazee nikajisemea ngoja nikakague tena kwangu, hapo hamna kitu nikafika nikaangusha sitting room, kuanzia hiyo siku sikuwahi kulala tena home

Kesho yake asubuhi nikazama game nikanunua sofa bed kwa 395,000/= nakumbuka nilikuwa nnalitamani sana afu likawa kwenye ofa nikajilipua, sahani, frying pan, sufuria na glass, nikarudi huome nikang’oa TV yangu, music system + king’amuzi na ki fridge kidogo nilikuwa nnatumia chuo nikabeba na kimeza cha kishkaji cha kuwekea Tv nikamuaga mzee mimi ninasepa nahamia sinza, akasema poa nikapita mwenge nikachukua jiko la gas + mtungi

Hii siku ya pili nikaanza na asset zangu zilikuwa ni sofa bed, kimeza cha kuzushi cha tv, tv, music, jiko la gas, mtungi na vyombo vya jikoni...

Kwa miezi miwili mfululizo nilikuwa nnalala sitting room
 
Hongera sana mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…