Mafian cartel
JF-Expert Member
- Nov 19, 2021
- 4,280
- 7,963
Umepambana sana keep pushingKipindi Niko chuo siku za weekend nachomoka mara home kwa mzee, mara kwa bi.mkubwa, mara Kwa washkaji… sasa nikienda weekends kwa wana nakuwa inspired kinoma! Mpaka sometimes likizo Naweza kutumia hadi week mbili kwa washkaji staki tena kwenda maskani, baada ya wanangu kumaliza mmoja akaenda Ulaya mmoja akapata kitengo Mkoa fulani kwa sababu kwao walikuwa na watu upande wa ujombani. Kipindi wana wana-separate mimi Niko home kwa Bi.mkubwa life ikaanza kuwa michosho hamna michongo wala nini na kama unavojua nyumbani dharau na kejeli+ nyodo Hasa kutoka kwa madogo huwa haziishi. Sasa pale home bi.mkubwa alikuwa kaolewa tu inamana sio kwetu kwa “100%” mzee mzima nikawa Uncomfortable siku moja nilivurugwa vibaya mno mapema alfajiri nikasepa kuelekea Magomeni kwa jamaa zangu wengine ambapo ni nyumbani kwao na mwanangu mwingine wa Karibu sana ambaye yuko Mamtoni kitambo tangu tuko O-level ila bahati nzuri ukaribu na urafiki wetu wa kushibana ulikaribisha undugu mpaka nikaweza kukaa kwao bila pingamizi. Kama zali baada ya kukaa pale siku kadhaa rizk ikawa inapatikana na mfukoni sikaukiwi ingawa ugenini ni ugenini tu Sio wote walipenda uwepo wangu pale. Msimamizi wa ile nyumba ambaye alkuwa ni shangazi yake na mwanangu alinipenda sana na kuniamini kutokana na nidhamu na uaminifu kiasi kwamba mpaka kunishirikisha maswala kadhaa ya familia… kimbembe kikaja kuna shangazi yake mwingine wa huyo mwanangu ambaye nilienda kuishi kwao kutokana na ups and down za familia alikuwa anaishi mtoni na yeye sasa akaja bongo kula goodtime na kufatilia michongo yao mingine huku bongo ya ujenzi na biashara zao akanikuta naishi pale na kabla alipata taarifa. Dahh! Yule shangazi hakupenda kabisa uwepo wangu pale na akaagiza niondoke. Kwa sababu mwenye pesa ana kauli yule shangazi wa kwanza msimamizi wa mjengo hakuwa na namna akaniita na kuniweka wazi. Nikiwa kwenye tathmini nikapokea simu kutoka majuu hakuwa mwingine bali ni Mama mzazi wa rafiki yangu na akanitaka nibaki hapo kwa sababu mwana tayari nilimchana kila linaloendelea maishani kwangu kipindi hicho. Siku zilizidi kusogea ingawa maisha yalikuwa mazuri ya amani pale na utulivu lakini maneno ya chini chini yalikuwepo. Shangazi msimamizi wa nyumba anazidi kuwa pressurized kutoka kwa Dada’ake kwamba kijana aondoke hapo sasa ukawa mvutano kati ya mawifi dhidi yangu. Nikaona isiwe kesi nikiwa katika maandalizi ya kusepa mwanangu akanivutia waya akaniambia siku si nyingi nakuja bongo usiondoke kwanza. Mwana akaja na life ikawa inaendelea Kumbe mwanangu alikuja na Neema. Alijua wazi mwanae sina kitu na Niko kwenye situation ngumu ingawa rizq ya pesa za vocha na kubadili mashati inapatikana. Akanipatiaga kitita kirefu cha pesa nakumbuka ilkuwa baada ya mwezi mtukufu na baada ya sikukuu ya eid mnamo mwaka fulani. Nikafanye mafekechee ya kutafuta chimbo maeneo fulani maeneo ya Mikocheni “A” uswahilini ambapo Nlkuwa na mwanangu mwingine anaishi kule lakini alikuwa anafanya kazi dukani. Ikabidi aniunganishe na wana wengine ambao ni ndugu zake tukawa tunakaa ghetto moja. Nikarudi Magomeni na kuaga baada ya kuweka mambo sawa na nikaanza maisha rasmi kama mpangaji. Life ikasonga na siku zikasogea wale wana niliokuwa naishi nao wakapata kazi sehemu tofauti hivyo wakalazimika kuhama… mmoja akaenda Visiwani mmoja hapahapa Dar maeneo ya kawe karibia na Mbezi kamanda nikabaki peke yangu tena ingawa sikupapenda maeneo yale kutokana na mazingira machafu na palikuwa uswahilini nikasubiri kodi iishe… baada ya muda nikapata mchongo ukaniongezea pesa kidogo ikabidi nihame sasa nikahamia Mikocheni “B” ambapo ghetto hata unaweza kumleta demu akagoma kuondoka [emoji1][emoji39][emoji1786] na baada ya wiki chache nikapata kibarua ofisi fulani maeneo ya Mbezi beach. Safari ya maisha ikaanzia hapo ingawa si haba Hohehahe anasongesha siku
Mnooooh yaan. [emoji39][emoji39][emoji39][emoji39]Mia2 dah
Mkuu mambo huwa yanagoma, yanayumba, kuna kufilisika, kuuumwa, kuhujumiwa ndg yangu unaamua kurudi nyuma na kujipanga upya.Hivi Kuna mtu ana 38yrs anaishi geto?? Aiseee! Umri huo kijana anatakwa awe na familia kwa maana mke na watoto. Sasa utaishije geto mzee mzima?
Hongera sana.View attachment 2229827View attachment 2229830maisha bado sjayapatia, bado kidoooooogo
Ahsante mkuu! Nimeona nikazie kwenye Uzi wako maana nimekumbuka mbali sana,umenikumbusha kitu muhimu kwenye historia ya maisha yangu maana hata mimi niliwahi kuishi na watu baki na ndio walionisaidia.Umekazia sana mkuu! [emoji1477][emoji1488]
Nashkuru Mungu niliyajua haya mapema na niliishi ndani ya misingi hiyo… siku zikasogea na Mungu akanionesha njia
Ni nukta muhimu sana za kukazia kwa vijana walio kwenye hatua za kutafuta katika maisha binafsi.
We noma mzee [emoji122][emoji122]Hata ningekua bakhess utumbo siachiiiiii[emoji1316]
Hata ningekua bakhess utumbo siachiiiiii[emoji1316]
Hivi Kuna mtu ana 38yrs anaishi geto?? Aiseee! Umri huo kijana anatakwa awe na familia kwa maana mke na watoto. Sasa utaishije geto mzee mzima?
Mkuu mambo huwa yanagoma, yanayumba, kuna kufilisika, kuuumwa, kuhujumiwa ndg yangu unaamua kurudi nyuma na kujipanga upya.
Maisha ni kitabu kina kurasa nyingi na kila ukurasa una habari zake.
Ahsante mkuu! Nimeona nikazie kwenye Uzi wako maana nimekumbuka mbali sana,umenikumbusha kitu muhimu kwenye historia ya maisha yangu maana hata mimi niliwahi kuishi na watu baki na ndio walionisaidia.
Halafu wanawake na mashemeji niliowakuta kila nilipokuwa nikienda nilikuwa nikiishi nao vizuri sana kwa heshima na adabu.
Tamaa niliziweka pembeni pamoja na mitego yao, hakuna kitu kibaya kama kuingilia mapenzi ya watu. Yaani umekaribishwa kwa watu unaanza kutamani vidada ulivyovikuta na wake au wapenzi wa kaka zako. Hii siyo poa unajitengenezea mazingira magumu.
Mkuu mimi baada ya kufanikiwa kiasi fulani niliwapelekea zawadi japo kidogo lakini kuonyesha moyo wa shukrani. Japo wengine sijui hata wako wapi ,ila niliobahatika kuwaona niliwashukuru kwa wema wao.
Yaani hata kama unaishi nao nyumba za kupanga unawapa heshima zao,wakikuomba msaada wa kazi ambazo unaziweza fanya ilimradi hazikuondolei utu wako na heshima yako.
Mimi ninaamini kama kijana ukiweza kuishi na watu baki vizuri huku ukivumilia madhaifu yao mpaka unafanikiwa na kuamua kuanzisha mji wako huwezi kushindwa kwenye maisha wala kuishi na mke wako.
Maana walimwengu ni shule tosha wadogo zangu, wengi hapa ni wadogo zangu maana nimekuwa ghetto kitambo sana.
Ahsante!!
hiyo radio gani? niuzie pc mojaView attachment 2229827View attachment 2229830maisha bado sjayapatia, bado kidoooooogo
Karibu sana mkuu. Mwanzilishi wa huu uzi tumpe big up maana unasaidia vijana wengi kupata upenyo wa kuanza maisha.Busara kubwa sana! Nazidi kupata shule kutoka kwako kiongozi…, nazidi kujifunza [emoji1488]
Radio ni Seapiano
Mungu abariki harakati zako mkuu!Ghetto ninaloishi lina mkeka,ndoo ya maji na mifuko yangu ya nguo..napambana nafanya biashara ya kutembeza bidhaa za urembo.wiki hii mambo ni mazuri jumatatu mauzo yalikuwa 37,000 leo 26,000 napambana kutafuta hela pia nasali sana ili mwaka 2023 nije kuwa na ghetto zuri lenye vitu vizuri ndani..
Matumizi yangu hayafiki 5000 kwa siku na mara nyingi ni chini ya 4000 hela ya kula naitoa kwenye biashara hii hii ambayo niliianza jumatano iliyopita hadi jumapili nilipumzika niweza kusave 63,000 hadi leo na nimeshatoa hela ya kwenda kuongeza vitu kesho kariakoo..
Lengo langu niongeze biashara ya pembeni ili inigharamie bill zangu za kila siku.Lengo langu la mwaka ujao niwe na ghetto zuri lenye vitu vizuri ndani vilevile ninunue bodaboda hata ya mtumba iniingizie pesa na vilevile niwekeze kwenye kilimo kama sitafanikiwa katika yote hayo matatu basi at least hayo malengo mawili yatimie.
Uzi huu umenigusa sana hadi nmeamua kuishi mwenyewe kwangu kiukweli sijawahi kuandika post ndefu kuliko hii hapa JF ila kwa hisani ya uzi huu nimeshare jambo langu smartphone yenyewe ninayotumia ni majanga panapo majaaliwa nitaleta mrejesho wa maendeleo ya biashara na picha ghetto langu kwa sasa..
Roger that!
Ahsante mkuu. Unajua nini, kuishi kwingi unajifunza mengi, kuishi na wengi ni kuona mengi.Maisha yanatufundisha mambo mengi sana. Ishi vizuri na watu upate vitu.Kiongozi una busara na uelewa mpana sana! Mungu akuzidishie
Umenifurahisha uliposema unasali sana. Ibada ni nzuri inakuondolea msongo wa mawazo na kutokujihusisha kwenye vikundi viovu.Ghetto ninaloishi lina mkeka,ndoo ya maji na mifuko yangu ya nguo..napambana nafanya biashara ya kutembeza bidhaa za urembo.wiki hii mambo ni mazuri jumatatu mauzo yalikuwa 37,000 leo 26,000 napambana kutafuta hela pia nasali sana ili mwaka 2023 nije kuwa na ghetto zuri lenye vitu vizuri ndani..
Matumizi yangu hayafiki 5000 kwa siku na mara nyingi ni chini ya 4000 hela ya kula naitoa kwenye biashara hii hii ambayo niliianza jumatano iliyopita hadi jumapili nilipumzika niweza kusave 63,000 hadi leo na nimeshatoa hela ya kwenda kuongeza vitu kesho kariakoo..
Lengo langu niongeze biashara ya pembeni ili inigharamie bill zangu za kila siku.Lengo langu la mwaka ujao niwe na ghetto zuri lenye vitu vizuri ndani vilevile ninunue bodaboda hata ya mtumba iniingizie pesa na vilevile niwekeze kwenye kilimo kama sitafanikiwa katika yote hayo matatu basi at least hayo malengo mawili yatimie.
Uzi huu umenigusa sana hadi nmeamua kuishi mwenyewe kwangu kiukweli sijawahi kuandika post ndefu kuliko hii hapa JF ila kwa hisani ya uzi huu nimeshare jambo langu smartphone yenyewe ninayotumia ni majanga panapo majaaliwa nitaleta mrejesho wa maendeleo ya biashara na picha ghetto langu kwa sasa..
Roger that!
Uwanja wa Amani?Niko mitaa ya villa park hapa kwa mbele kidogo kabla hujafika uwanjani
Safi sana,usikate tamaa, keep hustling.Nlipost hiii mwaka 2020 na badae December mwaka huo huo nikawa nasepa maskan kwenda kuanza maisha kitaaa bila kuwa na mishe yoyote. Kiukweli nilipiga kazi yoyote iliokuja mbele yangu na hiii ikansaidia kukutana na washikaj mbalimbali ambao ikasaidia kupeana michongo. Hadi Sasa npo get naona hatua zinaenda ila kwa mwendo wa Kobe.