Nyumbani Baba ni Yanga, Mama ni Simba.
Siku ambazo Yanga ilikuwa ikishinda, nyumba nzima tunaletewa zawadi, kuanzia watoto mpaka Mama. Kama ulikuwa na kosa unaasamehewa na siku hiyo hulazimishwi kulala mchana. Nyumbani tulikuwa na kuku alipewa jina la Sekilojo Chambua, ilo jina alipewa tangia akiwa kifaranga mpaka akawa Jogoo.
Kiufupi Yanga kushinda, tafsiri inayonijia ni Kwa namna gani familia yetu ilikuwa na furaha back in the days. Now days kila mmoja yuko anapopajua yeye, maisha ya utafutaji yametutawanya. Nyumbani kabaki Baba na Mama kama walivyoanza.