Ulianzaje kuipenda timu unayoishabikia?

Ulianzaje kuipenda timu unayoishabikia?

Drogba mnyama, jamaa alifanya niipende Chelsea.
 
ARSENAL
FA community 2003 Arsenal vs man utd bado nikiwa dogo janja sana nilikua na mabraza 2 moja shabiki wa arsenal mwingine man utd , siku ya game kama kawaida tulikua tunaangalia maigizo yale kwa aunt yangu mara paap wakaja ma uncles na mabraza wakatuambia “ muda wa ball huu badilisheni channel” daah madogo janja tukanuna ikabidi tuangalie mpira ivyo ivyo kuna bro wangu moja huyo nilikua napenda kwenda nae against sana sasa yeye alikuwa man utd damu damu ikabidi mwamba niwe arsenal.

Nakumbuka free kick ya henry ilipigwa mbali sana arsenal akasawazisha goli ikawa 1-1 wakaenda penalties arsenal akapigwa, man utd wakabeba ngao.
Nakumbuka wakati tunaenda shule nikawa namlaumu braza wa arsenal ameshabikia timu mbovu akawa ananiambia bahati mbaya tu dogo[emoji23] , huyu mwingine ananipa maneno nihamie man utd kutokana na kutokuwa na tv home enzi izo msimu wa golden trophy ukanipita.

2004 mzee akachukua tv game ya kwanza kabisa kuiona kipindi icho ikawa game ya Arsenal vs man utd nakumbuka tukafa tena goli 2 -0 ( van nistroy na wayne rooney walitupia goli, van alishangilia vibaya mno mpaka nikawa nawauliza mabro mbona anashangilia ivyo ndo wakanipa mkasa mzima).

Toka hapo nikawa Arsenal fan wa kudumu kabisa hakuna game ilikua inanipita hata tu ya Blackburn vs wigan nilikua naangalia , ubishi wa mpira ukawa mwingi hasa pale kitaa watoto tunaopenda mpira na mabraza walikua wengi kuna wengine sisi tupo primary lakini tunabishana na mabraza wa secondary kabisa[emoji23].

Tulikua tunafuga mbwa basi jioni tunaenda kuwafuatia chakula basi njiani ni ubishani wa mpira tupu mara tuhesabu watu wanaopita wamevaa jezi za arsenal na man utd wapi ni wengi au hata kuwasimamisha madogo na vijana kuwauliza wao ni timu gani? Arsenal ikaniingia kichwani haswa pamoja na kula vichapo vingine lakini mapenzi yakawa yanaongezeka ulikuwa huniambii chochote kuhusu henry na ashley cole.
UEFA tukatolewa na bayern walitupiga 3-1 nikawa nalalamika tunafungwa mpaka na hiki kitimu [emoji23][emoji23] wakaniambia dogo hii timu hatarii sana acha kabisa, second leg tukashinda 1-0 nauliza vipi mbona tumetoka na tumeshinda nikapewa elimu ya goli la ugenini hapo[emoji23]

Nakumbuka pia kuna game arsenal vs man utd iliisha kwa 4-2 ilichezwa saa 4 usiku daah ile game ilikuwa [emoji91] tukala chuma 4 CR7 ni wa moto na mikasi yake ile, kesho yake mtaani madogo wakahama timu wakaenda liverpool na chelsea na baadhi ya mabro kabisa wakahamia man utd ila mwamba nikakomaa na arsenal.
Those days nilikua nafuatilia mpira asee mpaka machozi arsenal tukifungwa mpaka bi mkubwa alikua anashangaa nalia kisa timu [emoji23][emoji23], maana ilikua fujo mtaani timu yako ikifungwa yaani njia nzima ulikua unaiona chungu wakati wa jioni kuwafuatia mbwa chakula ni unapigwa majungu tu.

2023 baada ya kukosa ubingwa wa epl nikaona hii miaka 20 ya Arsenal inanitosha (2 decades ) hizi timu sio kabila nikaona nianze moja na wanangu wa Newcastle.

Rasmi mimi ni Newcastle fan nianze nao moja kabisa kama ku hunt makombe tuwe wote[emoji38] kuliko kubaki Arsenal, mpaka rafiki angu moja akawa ananiambia yaani arsenal inaanza kuwa tamu mpaka hela ya usajili inatoa then wewe ndo unaondoka mwanangu wewe kweli umezoea shida [emoji23][emoji23].
 
Swali zuri sana.

Nilianza kuishabikia Yanga ningali mdogo sana mwaka 1969 wakati Simba bado inaitwa Sunderland. Wakati huo timu kubwa Dar zilikuwa ni Yanga, Sunderland, na Cosmopolitan (hii sijui iliishia wapi). Siku hiyo Yanga ilikuwa inacheza robo fainali ya kombe la Ubingwa wa Afrika dhidi ya Asante Kotoko ya Ghana, wakatoka droo ya 1-1 ikabidi zipigwe penalti ambapo yanga ilikosa penalti mbili huku Asante Kotoko ikikosa penalty moja tu na hivyo wao kuibuke kidedea. Golikipa wa Yanga wakati huo aliyekuwa akiitwa Elias Michael alikuwa golikipa aliyeonyesha uwezo wa juu sana- alikuwa kivutio changu cha kwanza kwani hata mimi huko mtaani nilikuwa golikipa wa mtaa. Halafu wachezaji wakina Kitwana Manara, Maulid dilunga, Salehe Zimbwe, Leonard Chitete, Omar Kapera na wengineo walinifurahisha sana nikawa mwana Yanga kuanzia pale.

Mchezo wa Simba Vs Yanga pale Nyamagana pia nilikwenda kuuona kwa treni pamoja na kaka yetu aliyetulipia gharama zote za usafiri na makazi. Gibson Sembuli, na Sunday Manara walituvutia sana, ila kivutio kikubwa alikuwa ni Leodgar Tenga kwani tuliambiwa alikuwa anasoma Engineering hapo Chuo Kikuu cha Dar. Kwa vile utotoni nilikuwa nnaota sana Uhandisi, basi Tenga akaongeza kunivutia sana Yanga.

Kuna wakati nilipoteza stimu miaka ya sabini tulipofungwa 5-0 na simba baada ya timu kuwa imevunjika katika makundi mawili ya Pan-African (Raizon) na Yanga-Afrikan (kandambili).

Hata hivyo sijaacha kuipenda Yanga hata inapokuwa matatizoni
 
1994 world cup marekani nilianza kuishabikia Brazil Roberto Baggio ali paisha penati Kwenye final
1994 World Cup Nigeria kina Rashid Yekini anafunga goli anaenda kushangilia ktk nyavu
1996 Olympic games Atlanta niliishabikia Nigeria enzi za Kina Sunday Oliseh JJ okocha Nwanko Kanu George Finidi nk
1996-97 Manchester United baada ya kuvutiwa na Paul Ince Eric Cantona nk ila kuwa shabiki mkubwa wa United ni 1999 ali pochukua UEFA champion league mbele ya Buyern Munich mjini Barcelona uwanja wa Nou camp. Goal mbili za Ted sheringham na Ole gunner mmasai.
1991 Simba alimfunga yanga kwa penati 6-5 afrika mashariki now Kagame cup ngoma ilipigwa Aman zanzibar. David mwakalebela akakosa penati.
 
Swali zuri sana.

Nilianza kuishabikia Yanga mwaka 1969 wakati Simba bado inaitwa Sunderland. Wakati huo timu kubwa Dar zilikuwa ni Yanga, Sunderland, na Cosmopolitan (hii sijui iliishia wapi). Siku hiyo Yanga ilikuwa inacheza robo fainali ya kombe la Ubingwa wa Afrika dhidi ya Asante Kotoko ya Ghana, wakatoka droo ya 1-1 ikabidi zipigwe penalti ambapo yanga ilikosa penalti mbili huku Asante Kotoko ikikosa penalty moja tuy na hivyo wao kuibuke kidedea. Golikipa wa Yanga wakati huo aliyekuwa akiitwa Elias Michael alikuwa golikipa aliyeonyesha uwezo wa juu sana- alikuwa kivutio changu cha kwanza kwani hata mimi huko mtaani nilikuwa golikipa wa mtaa. Halafu wachezaji wakina Kitwana Manara, Maulid dilunga, Salehe Zimbwe, Leonard Chitete, Omar Kapera na wengineo walinifurahisha sana nikawa mwana Yanga kuanzia pale.

Mchezo wa Simba Vs Yanga pale Nyamagana pia nilikwenda kuuona kwa treni pamoja na kaka yangu. Gibsona Sembuli, na Sunday Manara walituvutia sana, ila kivutio kikubwa alikuwa ni Leodgar Tengan kwani tuliamabiwa alikuwa ansoma Engineering hapo Chuo Kikuu cha Dar. Kwa vile utotoni nnilikuwa nnaota sana Uhandisi, basi Tenga akaongeza kunivutia sana Yanga.

Kuna wakati nilipoteza stimu miaka ya sabini tulipofungwa 5-0 na simba baada ya timu kuwa imevunjika katika makundi mawili ya Pan-African (Raizon) na Yanga-Afrikan (kandambili).

Hata hivyo sijaacha kuipenda Yanga hata inapokuwa matatizoni
Aisee.!
 
Swali zuri sana.

Nilianza kuishabikia Yanga mwaka 1969 wakati Simba bado inaitwa Sunderland. Wakati huo timu kubwa Dar zilikuwa ni Yanga, Sunderland, na Cosmopolitan (hii sijui iliishia wapi). Siku hiyo Yanga ilikuwa inacheza robo fainali ya kombe la Ubingwa wa Afrika dhidi ya Asante Kotoko ya Ghana, wakatoka droo ya 1-1 ikabidi zipigwe penalti ambapo yanga ilikosa penalti mbili huku Asante Kotoko ikikosa penalty moja tu na hivyo wao kuibuke kidedea. Golikipa wa Yanga wakati huo aliyekuwa akiitwa Elias Michael alikuwa golikipa aliyeonyesha uwezo wa juu sana- alikuwa kivutio changu cha kwanza kwani hata mimi huko mtaani nilikuwa golikipa wa mtaa. Halafu wachezaji wakina Kitwana Manara, Maulid dilunga, Salehe Zimbwe, Leonard Chitete, Omar Kapera na wengineo walinifurahisha sana nikawa mwana Yanga kuanzia pale.

Mchezo wa Simba Vs Yanga pale Nyamagana pia nilikwenda kuuona kwa treni pamoja na kaka yangu. Gibson Sembuli, na Sunday Manara walituvutia sana, ila kivutio kikubwa alikuwa ni Leodgar Tenga kwani tuliambiwa alikuwa anasoma Engineering hapo Chuo Kikuu cha Dar. Kwa vile utotoni nilikuwa nnaota sana Uhandisi, basi Tenga akaongeza kunivutia sana Yanga.

Kuna wakati nilipoteza stimu miaka ya sabini tulipofungwa 5-0 na simba baada ya timu kuwa imevunjika katika makundi mawili ya Pan-African (Raizon) na Yanga-Afrikan (kandambili).

Hata hivyo sijaacha kuipenda Yanga hata inapokuwa matatizoni
Heshima yako Mkuu,1969 Baba yangu ndiyo ana ajiliwa kwa mara ya kwanza akiwa kijana kabisa baada ya kumaliza masomo.Hapo bado hata hajafikiria kuwa na familia.Narudia tena Heshima yako Mkuu
 
Heshima yako Mkuu,1969 Baba yangu ndiyo ana ajiliwa kwa mara ya kwanza akiwa kijana kabisa baada ya kumaliza masomo.Hapo bado hata hajafikiria kuwa na familia.Narudia tena Heshima yako Mkuu
Asante; heshima yangu iko pale pale
 
Simba, sababu ya kwanza kufuata mkondo wa familia pili upande ule mwengine siipendi ile rangi, ya chanzo cha matatizo
 
Simba Sc niliipenda tangu nikiwa mimba. Sasa imagine mimba inafanya maamuzi bora kuliko wewe Uto?
 
West Ham vs Liverpool 2016.

Goal la Gerrard, captain fantastic...dakika za jioooooooni....
 
Fc bandari ya tanga
Baba yangu mkubwa alikuwa ni muajiriwa wa jwtz baada ya utumishi wake akapewa kazi hapa bandarini na walikuwa na timu yao aliwai kunipa jezi ya Fc bandari nikawa shabiki wake since hapo

GUNGU RANGERS ya kigoma
Hii timu ilikuwa na makao makuu yake sehemu ambayo mm nilikuwa nimepanga chumba so nikawa shabiki wake pia

WIZARD FC ya Kigoma
Hii timu nilikuwa shabiki baada ya Mimi kuhamia mtaa ambao hii timu ilikuwepo na siku ambayo nahamia wachezaji wa hii timu ndio walinisaidia kushusha vitu na kuvipanga geto
After nakumbuka niliwapa mchango wa jezi na mipira miwili

WAZEE FC ya ujiji hii baba mkwe wangu ni kipa hapo na ndio mchezaji mdogo timu nzima Ana miaka 56

MANCHESTER UNITED hii nilishabikia kwenye hiyo fainali dhidi ya Bayen Munich (Niliwaonea huruma Manchester)

YANGA
Hii timu nilifundishwa kushabikia na aliyekuwa meneja wa tanesco kigoma marehemu Nyaringa hawa yanga niliwapendea Rangi ya jezi na hiyo mechi walikuwa wanacheza na timu ya kiarabu siikumbuki lkn matokeo yalikuwa ni 0:0

MASHUJAA FC
Hii timu naishabikia sababu ya urafiki wangu na baadhi ya wakuu wa vikosi hapa kigoma Kama kanal Nyingo na Meja Kassimu walinipa free pass ya mechi zote za mashujaa zitakazochezewa lake tanganyika stadium
 
Inaonekana unapenda sana nyumbani mkuu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom