Ulevi wa pombe ni hatari kwa afya yako

Ulevi wa pombe ni hatari kwa afya yako

Nadhani mleta mada ungekuja na hoja nzito na ya msingi kushawishi viwanda vya pombe vyote vifungwe, hio ingekuwa solution, haya mengine uliyoandika ni kelele za bahari haziwezi kuzuia safari ya mashua.
Kodi apate wapi? Wakati TBL ndiyo mlipa kodi mkuu
 
Natumaini nikimaliza mwezi wa tatu bila kilaji ndio nimeacha hivyo, kuna mdau humu alitoa ushauri mzuri sana juu ya pombe, me bado naiongele na nakaa na walevi sema sigusi kabisa nakula maji tu lengo baada ya muda nione kitu cha kawaida na hakina maana kabisa. Pombe ni mbaya sana nilikosea watu heshima na kuwa mtu wa hovyo sana. Uzi mzuri sana huu.
Ulikuwa huli vizuri mkuu kabla ya pombe?
 
Hili bwege na halinacha zake hapa,hivi huo mshahara unaolipwa unatoka kwa baba yako?? Tbl ni mlioa kodi mkubwa hapa ila mnawapiga vita kila uchwao,muwaache kila mtu na starehe zake mbona wewe zinzi hatusemi au wewe huogopo ukimwi?? Mxuuu!! Shwain
[emoji1] [emoji1] [emoji1]
 
Kwa hili jiandae kupingwa na wengi, japokuwa uliyoyaandika yana ukweli ndani yake.

Ila yote kwa yote pombe sio haswa pale inaponywewa bila kipimo.
Hata ikatokea akapingwa but still ukweli ni ule ule,hata mnywaji mwenyewe anajua kuwa pombe ni hatari.
 
Muhudumu ongeza glass, maisha ndio haya haya! kwani uliumbwa uishi milele?
Je hizo figo, maini na firigisi unaenda nazo kaburini?
kama vipi si utoe uwape wanaohitaji?
Mhudumu ongeza glass weka wine, whisky, brand, banana, gongo weka mezani!
Mmmmh!Anyway mi nahisi uwezi kuchanganyachanganya kiwango hicho unless you are kidding!
 
MKUU KAMA KUNA KITU MBADALA WA POMBE NAOMBA UWAAMBIE MAANA POMBE KUIACHA WANASEMA NI KAZI MNO
Mimi niliacha kunywa pombe baada ya kumkubali YESU KRISTO kiukweli kabisa, kabla ya hapo nilijaribu kuacha ulabu lkn kila mara nilishindwa.

Sasa niko free sijawahi irudia hiyo kitu huu ni mwaka wa sita sasa.
So that naona njia mbadala ni kuwa mlokole kiukweli.
 
Muhudumu ongeza glass, maisha ndio haya haya! kwani uliumbwa uishi milele?
Je hizo figo, maini na firigisi unaenda nazo kaburini?
kama vipi si utoe uwape wanaohitaji?
Mhudumu ongeza glass weka wine, whisky, brand, banana, gongo weka mezani!
Pole na Mungu akurehemu.
 
Hili tangazo lingefaa enzi za Jakaya ila enzi hizi tumeshaachishwa kilazima pombe
 
Hakuna kitu kisicho na madhara pale ukitumiapo pasipo kiasi, hivyo pombe ni sehemu ya vitu vingi sana vyenye madhara makubwa pale uvitumiapo pasipo mipaka.
Pombe kiasi ni sawa na Balimi ngapi kwa siku?
 
Ulevi wa pombe ni ugonjwa unaoathiri watu wengi duniani. Kwa ulimwengu mzima,mamilioni ya watu wameathirika kwa njia moja ama nyingine kutokana na tatizo hili la ulevi wa pombe.

Pombe hupendwa na watu wengi na kuwepo kwake kumeanza tokea enzi za wahenga. Masimulizi ya pombe hupatikana ktk vitabu mbalimnali na hata Biblia imezungumzia na kuonya kuhusu ulevi wa pombe.

KWA NINI WATU
WANAVUTIKA KUNYWA
POMBE?

Sababu kubwa hasa huwa ni kutoa burudani kwa mtumiaji awapo ktk starehe zake za kila mara.
Ni kweli pombe isiponywewa kwa wingi ni kiburudisho, inaliwaza na kumfanya mtu achangamke, wakati mwingine watu hujiamini baada ya kunywa pombe.

POMBE IKINYWEWA
HUFANYA NINI MWILINI?

Pombe ikinywewa huingia tumboni, na baada ya muda hufika kichwani kwa kupitia kwenye mishipa ya damu. Matokeo Yale mtu huanza kuwa na furaha na kujiamini kwa muda.
Jinsi pombe inavyozidi kuingia tumboni ndivyo inavyozidi kuingia kwenye damu. Damu ikiwa na pombe nyingi hudhoofisha sehemu ya ubongo ambapo humfanya mtu kushindwa kupambanua jema na baya hata kumfanya aweze kujisaidia hadharani, kumtemea mate mwenzake nk.

AINA ZA POMBE.

Pombe zimegawanyika ktk sehemu tatu

1. Pombe Kali kiasi _ kama
bia, mbege nk.

2. Pombe Kali sana _ kama
vile divai.

3. Pombe Kali zaidi _ kama
vile whisky, gongo na
konyagi.

MADHARA YA ULEVI.

_ Kuugua magonjwa kama
kisukari, ugonjwa wa moyo,
utapiamlo , ini, kudhoofu akili,
na mwili, kusababisha ajali nk

Ni vizuri kutokunywa pombe kama hujaanza.
Na kama wewe ni mnywaji mahili tafuta msaada mapema.

Nawasilisha.
Wanaccm wote pale dodoma walilewa chakari!
Asilimia zote 100 walipombeka ukumbini.
 
Basi viwanda vya kutengeneza kombe vingefungwa.....
Acha tunywe tu pombe maana hakuna jinsi ila tu unapokunywa Tumia kiasi

Ova
 
Hakuna kitu kisicho na madhara pale ukitumiapo pasipo kiasi, hivyo pombe ni sehemu ya vitu vingi sana vyenye madhara makubwa pale uvitumiapo pasipo mipaka.
Kwa usimamizi wa dakitari inaweza kuponya vidonda vya tumbo.

Shida ni pale unapotumia bila ushaurl wa daktari huku ukiwa so mgonjwa, ni hatari kwa afya!!
 
Back
Top Bottom