Ulevi ulivyoharibu harusi

Ulevi ulivyoharibu harusi

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
58,636
Reaction score
220,438
Hapabiri za leo wapendwa,

Hiki kisa nimekutana nacho kwenye gazeti ndiyo nimeamua kushare na nyinyi leo

Beatrice akiwa mtoto wa pekee kwa wazazi wake, wazazi wake walikuwa na maisha ya kati, yaani wote ni waajiriwa, Beatrice alimaliza darasa la 12, matokeo yake hayakuwa mazuri sana lakini alifanikiwa kupata kazi kwenye duka maarufu mjini kwao la kuuza vitabu.

Beatrice ni binti mwenye mvuto, akiwa kazini alikutana na Victor kijana alieajiriwa kwenye ofisi moja mjini hapo, Victor alihitaji kitabu ambacho hakikuwepo kwenye store ile, lakini Beatrice alijitahidi kukitafuta kwenye store za karibu na kuweza kukipa, baada ya hapo kama shukrani Victor aliomba ampeleke lunch.

Kufupisha habari, urafiki uliendelea kuwa uchumba. Victor anatoka katika familia tajiri sana, kwahiyo aliposema anataka kuoa, wazazi wa Beatrice walifikiria jinsi watakavyofanya harusi ya binti, hawana utaratibu wa kuchangisha michango lakini waliweka fedha bank tangia Beatrice anazaliwa ili zije zimsaidie akienda chuo kikuu, bahati mbaya au nzuri hakwenda lakini wazazi waliziweka ili aje anunulie kiwanja watakapoona yuko tayari.

Basi wazazi waliamua kutoa pesa ile ili kugharamia harusi, maandalizi yalifanyika, wazazi wa Victor waliishi mbali wote waliwalsili pamoja na ma uancle, aunties, babu, bibi madada na marafiki. Wengi walikaa hotelini kwakuwa nyumba ya Victor ilijaa sana ndugu na marafiki.

Usiku mmoja kabla ya harusi wafanyakazi katika bookshop anayofanya Beatrice waliamua kumwaga mwenzao, walitaarisha hen night party, basi Beatrice alikwenda, kwa furaha walicheza kunywa na kula. Beatrice alilewa sana, aliamua atoke nje, alitapika sana akiwa peke yake, baada ya pale nguvu zilimwishia, aliangalia akaona kibao cha hoteli, basi alichotaka kwa muda ule ilikuwa kitanda cha kupumzika tu. Kwenye pochi iliyokuwa begani kwake alikuwa na credit card, aliitumia kuchukua chumba hotelini, alipopewa funguo aliingia ndani na kulala.

Wale wa kwenye hen night walijua ameamua kwenda nyumbani kwakuwa amechoka na wangemsihi akae Zaidi, kule nyumbani hawajui kinachoendelea, baba na mama wanaomba Mungu hawajui mtoto alipo, wamekwenda kanisani, padre baada ya muda aliwaambia watoke wapishe harusi nyingine muda wao umekwisha.

Hall la harusi limepambwa catering service wanashusha chakula, bibi harusi hajulikani alipo, amekuja kuamka saa 12 jioni, anatoka nje anafikiri ni asubuhi, anaambiwa ni jioni, kufika nyumbani baba na mama hawataki hata kumuona, Victor amebadilika sura, aibu aliyoingia bamoja na ndugu waliosafiri kutoka mbali. Uchumba ulikufa.

Hiki ndiyo kisa cha pombe kilichomtokea Beatrice.
 
Pombe ililaaniwa.
[emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125]
 
Pombe noma..Tena wadada wakinywa pombe zinakimbilia chini.
 
hakuwa hata na rafiki jamani? huu uongo huu
Alitoka nje mara moja hakuaga mtu ndani, watu wote walikuwa wanamtafuta hata marafiki wa karibu, sasa kama na simu betri ilikuwa low ndiyo nitolee tena.
 
Pombe ililaaniwa.
[emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125]
Imelaaniwa tangu lini?? Hebu kuwa na heshima Kwa chanzo kikubwa cha mapato Kwa nchi..
 
Hapabiri za leo wapendwa,

Hiki kisa nimekutana nacho kwenye gazeti ndiyo nimeamua kushare na nyinyi leo

Beatrice akiwa mtoto wa pekee kwa wazazi wake, wazazi wake walikuwa na maisha ya kati, yaani wote ni waajiriwa, Beatrice alimaliza darasa la 12, matokeo yake hayakuwa mazuri sana lakini alifanikiwa kupata kazi kwenye duka maarufu mjini kwao la kuuza vitabu.

Beatrice ni binti mwenye mvuto, akiwa kazini alikutana na Victor kijana alieajiriwa kwenye ofisi moja mjini hapo, Victor alihitaji kitabu ambacho hakikuwepo kwenye store ile, lakini Beatrice alijitahidi kukitafuta kwenye store za karibu na kuweza kukipa, baada ya hapo kama shukrani Victor aliomba ampeleke lunch.

Kufupisha habari, urafiki uliendelea kuwa uchumba. Victor anatoka katika familia tajiri sana, kwahiyo aliposema anataka kuoa, wazazi wa Beatrice walifikiria jinsi watakavyofanya harusi ya binti, hawana utaratibu wa kuchangisha michango lakini waliweka fedha bank tangia Beatrice anazaliwa ili zije zimsaidie akienda chuo kikuu, bahati mbaya au nzuri hakwenda lakini wazazi waliziweka ili aje anunulie kiwanja watakapoona yuko tayari.

Basi wazazi waliamua kutoa pesa ile ili kugharamia harusi, maandalizi yalifanyika, wazazi wa Victor waliishi mbali wote waliwalsili pamoja na ma uancle, aunties, babu, bibi madada na marafiki. Wengi walikaa hotelini kwakuwa nyumba ya Victor ilijaa sana ndugu na marafiki.

Usiku mmoja kabla ya harusi wafanyakazi katika bookshop anayofanya Beatrice waliamua kumwaga mwenzao, walitaarisha hen night party, basi Beatrice alikwenda, kwa furaha walicheza kunywa na kula. Beatrice alilewa sana, aliamua atoke nje, alitapika sana akiwa peke yake, baada ya pale nguvu zilimwishia, aliangalia akaona kibao cha hoteli, basi alichotaka kwa muda ule ilikuwa kitanda cha kupumzika tu. Kwenye pochi iliyokuwa begani kwake alikuwa na credit card, aliitumia kuchukua chumba hotelini, alipopewa funguo aliingia ndani na kulala.

Wale wa kwenye hen night walijua ameamua kwenda nyumbani kwakuwa amechoka na wangemsihi akae Zaidi, kule nyumbani hawajui kinachoendelea, baba na mama wanaomba Mungu hawajui mtoto alipo, wamekwenda kanisani, padre baada ya muda aliwaambia watoke wapishe harusi nyingine muda wao umekwisha.

Hall la harusi limepambwa catering service wanashusha chakula, bibi harusi hajulikani alipo, amekuja kuamka saa 12 jioni, anatoka nje anafikiri ni asubuhi, anaambiwa ni jioni, kufika nyumbani baba na mama hawataki hata kumuona, Victor amebadilika sura, aibu aliyoingia bamoja na ndugu waliosafiri kutoka mbali. Uchumba ulikufa.

Hiki ndiyo kisa cha pombe kilichomtokea Beatrice.
itakuwa alikuwa anajifunza
 
Amshukuru Mungu huyo mwanaume hakuwa wake.
 
Ninawafikiria wazazi wake baada ya kutumia akiba yote kwanye harusi ya binti yao.
 
Nikukumbuka siku nimekunywa bapa mbili za konyagi. Nilizingua Sana mbele ya baba mdogo na mama mzazi.. Pombe mbaya
 
kwa kawaida kila hotel inakuwa na muda wa check out.
sa ilikuwaje mpaka room attendants washindwe kugundua uwepo wake?
au alifanya booking ya room kwa zaidi ya siku moja? kama ni ndio inamaana hiyo hotel huwa hawafanyi usafi wa room zao?
Hii ni stori tu ya kujenga chuki dhidi ya pombe.
Hapa hata mimi nilishidwa kuelewa au alilipia siku mbili sifahamu, lakini ni true story aliitoa Beatrice na kuwaasa vijana wenzake wawe na control ya pombe wasiruhusu pombe iwecontrol.
 
Uongo wa kitoto, kwenye hiyo party ikiwa yeye ndiyo mhusika ni lazima alikuwa na patron, Kwa ajili ya dharula,

Pili Kwa Aina ya ulevi uliouzungumzia ni Kwa mtu ambaye anakunywa pombe Kwa Mara ya kwanza, Je inawezekana mtu ujifunze pombe siku yake ya kuagwa!!!??? Story haina uhalisia ushafel,
 
Bite na yeye unaendaje kwenye ulev siku moja kabla ya harus tena bila mtu wa karbu kukuangalia
Mchumia janga hula na nduguze
 
Back
Top Bottom