Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,720
- 215,778
Hapabiri za leo wapendwa,
Hiki kisa nimekutana nacho kwenye gazeti ndiyo nimeamua kushare na nyinyi leo
Beatrice akiwa mtoto wa pekee kwa wazazi wake, wazazi wake walikuwa na maisha ya kati, yaani wote ni waajiriwa, Beatrice alimaliza darasa la 12, matokeo yake hayakuwa mazuri sana lakini alifanikiwa kupata kazi kwenye duka maarufu mjini kwao la kuuza vitabu.
Beatrice ni binti mwenye mvuto, akiwa kazini alikutana na Victor kijana alieajiriwa kwenye ofisi moja mjini hapo, Victor alihitaji kitabu ambacho hakikuwepo kwenye store ile, lakini Beatrice alijitahidi kukitafuta kwenye store za karibu na kuweza kukipa, baada ya hapo kama shukrani Victor aliomba ampeleke lunch.
Kufupisha habari, urafiki uliendelea kuwa uchumba. Victor anatoka katika familia tajiri sana, kwahiyo aliposema anataka kuoa, wazazi wa Beatrice walifikiria jinsi watakavyofanya harusi ya binti, hawana utaratibu wa kuchangisha michango lakini waliweka fedha bank tangia Beatrice anazaliwa ili zije zimsaidie akienda chuo kikuu, bahati mbaya au nzuri hakwenda lakini wazazi waliziweka ili aje anunulie kiwanja watakapoona yuko tayari.
Basi wazazi waliamua kutoa pesa ile ili kugharamia harusi, maandalizi yalifanyika, wazazi wa Victor waliishi mbali wote waliwalsili pamoja na ma uancle, aunties, babu, bibi madada na marafiki. Wengi walikaa hotelini kwakuwa nyumba ya Victor ilijaa sana ndugu na marafiki.
Usiku mmoja kabla ya harusi wafanyakazi katika bookshop anayofanya Beatrice waliamua kumwaga mwenzao, walitaarisha hen night party, basi Beatrice alikwenda, kwa furaha walicheza kunywa na kula. Beatrice alilewa sana, aliamua atoke nje, alitapika sana akiwa peke yake, baada ya pale nguvu zilimwishia, aliangalia akaona kibao cha hoteli, basi alichotaka kwa muda ule ilikuwa kitanda cha kupumzika tu. Kwenye pochi iliyokuwa begani kwake alikuwa na credit card, aliitumia kuchukua chumba hotelini, alipopewa funguo aliingia ndani na kulala.
Wale wa kwenye hen night walijua ameamua kwenda nyumbani kwakuwa amechoka na wangemsihi akae Zaidi, kule nyumbani hawajui kinachoendelea, baba na mama wanaomba Mungu hawajui mtoto alipo, wamekwenda kanisani, padre baada ya muda aliwaambia watoke wapishe harusi nyingine muda wao umekwisha.
Hall la harusi limepambwa catering service wanashusha chakula, bibi harusi hajulikani alipo, amekuja kuamka saa 12 jioni, anatoka nje anafikiri ni asubuhi, anaambiwa ni jioni, kufika nyumbani baba na mama hawataki hata kumuona, Victor amebadilika sura, aibu aliyoingia bamoja na ndugu waliosafiri kutoka mbali. Uchumba ulikufa.
Hiki ndiyo kisa cha pombe kilichomtokea Beatrice.