Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 4,783
- 14,975
Ulega ametoa maelekezo hayo jijini Dodoma, Juni 01, 2025 akiwa ameongozana na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Stergomena Tax na kukagua barabara hiyo ambayo utekelezaji wake umekuwa wa kusuasua kwa sababu ya upungufu wa wafanyakazi na mitambo ya ujenzi.
Waziri Ulega amemuagiza Mkandarasi CHICO kuhakikisha anaboresha mpango kazi wake ili aweze kukamilisha kazi zilizobakia zikiwemo ujenzi wa makalvati pamoja na madaraja katika barabara hiyo.
Aidha, Waziri Ulega amebainisha kuwa Serikali hivi sasa ipo katika hatua za mwisho za manunuzi za kumpata Mkandarasi wa kujenga barabara ya njia nne na sita kuanzia Chamwino Ikulu hadi katikati ya jiji la Dodoma.
Naye, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Alhaj. Jabir Shekimweri amewashukuru Mawaziri hao kwa kufika na kukagua hatua za barabara hiyo kwani lengo la barabara hiyo ni kuleta muunganiko na ukaribu kati ya Wilaya za Dodoma Mjini na Chamwino hivyo utachochea maendeleo katika maeneo husika.
Akitoa taarifa ya mradi huo, Mkurugenzi wa miradi kutoka TANROADS, Mhandisi Japherson Nnko amewahakikishia Mawaziri hao kuusimamia kwa karibu utekelezaji wa ujenzi wa barabara hiyo ili ikamilike kwa muda uliopangwa ambapo hadi sasa umefikia asilimia 51.