Ule utapeli wa kijuha umeanza tena...

Nishawahi kupata sms kama hiyo miezi kadhaa nyuma ikabidi nimuhoji vizuri nijue ni Nani maana ni kweli Kuna jamaa yangu ana kituo cha kitamaduni ila namba si zake.
Nilipoona kimya na mi nikapotezea kiaina ila si kujua kabisa kama ni Yale ya Tuma hela kwa namba hii hadi juzi dogo alipo tumia sms hiyo hiyo Ndio nikastuka
 
Hapana. Namba wanayotumia ni ya kawaida, huo mfano ulionipa ni namba ya huduma ambayo huwa inapigwa kutoka kwenye system na hata ikikupigia hutaongea na mtu live ila utasikiliza tu maelezo na kufanya kile unachoelekezwa, lakini namba ambayo wahudumu wanatumia kuwapigia wateja ni ya kawaida, kwa mfano Vodacom wanatumia +255754100100
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hujasomeka
 
Pengine! Na si unajua haya mambo huwa yanakuja kutokana na experience mtu aliyokumbana nayo. Asante kwa kuniongezea maarifa.
 
We umenielewa,kuna jamaa huko anatafuta dictionary.
 
Mie dogo alisafiri kwenda Dodoma akaibiwa simu.Waliomuibia Simu wakaanza kuitumia simu yake kusambaza meseji kama hizo.Nikajifanya nimeingia king,nikasema nauliza maswali ya kuconfirm wewe Nani akataja jina la Dogo,upo wapi akataja Dodoma.We unatokea Kijiji Gani,na last born kwenu anaitwa Nani,na maswali kama hayo jamaaa akapotea
 
Wajinga Sana,ila kuna watu wanawakamata.
 
Mazungumzo ya Tapeli Na Mwalimu aliyetaka kuhama kituo Cha kazi.

Tapeli:Hallo,wewe ni Mwalimu Fulani bin Fulani Na unataka kuhama

Mwalimu:Ndiyo nina uhitaji sana wa kuhama huku niliko.

Tapeli:Mimi nipo Tamisemi kuna mtu hapa nipo naye Ana uwezo wa kukusaidia tatizo lako ndani ya muda mfupi

Mwalimu:Nitashukuru sana kama nitafanikiwa.

Tapeli:Ila huyu mheshimiwa anahitaji ya maji kidogo ili aweze kufanya zoezi lako la kukuhamisha.

Mwalimu:Anataka kiasi Gani Na lini?

Tapeli:Anataka kiasi Fulani (Ziatajwa laki kadhaa) Fanya haraka Sasa hivi maana nafasi ni chache Na wahitaji ni wengi.

Mwalimu:Kwa Sasa hivi kupata hela ni ngumu maana hela ipo benki Na muda huu hakuna magari Na kwa bodaboda nauli haitoshi.

Tapeli:Mchukue bodaboda uende naye mjini utamlipa ukifika benki.Ufanye hima Mwalimu

Mwalimu: Oooh umenipa wazo zuri nachukua bodaboda nitamlipa nikifika mjini.(Mwalimu anampanga bodaboda kuwa aseme hawezi mpeleke town Bila kuweka advance ya shilingi elfu kumi,nyingine atamalizia akifika town)

Tapeli:Fanya haraka ukichelewa ofisi zitafungwa Na utakuwa umekosa nafasi

Mwalimu:Nimeongea Na bodaboda amekataa kunipeleka Bila kuweka advance hela ya mafuta labda uongee naye wewe umshawishi anipeleke.

Tapeli anaongea Na bodaboda,bodaboda anagoma kumpeleka mwalimu,Bodaboda anamshauri Tapeli amkopeshe mwalimu hela halafu ye ndo atalipwa Na Mwalimu.Tapeli anaingia kingi anatuma elfu kumi kwa bodaboda.Bodaboda Na Mwalimu wanatoa fasta ile elfu kumi halafu Mwalimu anapiga simu kwa Tapeli.

Mwalimu:Ndugu yangu umeniokoa,nimeshaanza safari ya mjini.

Masaa kadhaa yanapita.

Tapeli:Vipi mmeshafika mbona kimya.

Mwalimu:Mkuu sio kila siku unatapeli tu watu nawe siku moja Moja ukitapeliwa siyo vibaya.

TapeliπŸ™Anatukana matusi yote Na anagundua kuwa naye kaliwa)
 
Huu ni utapeli wa msimu si zamani .Biashara ya utalii imeshika huu msimu
 
Zamani sana.nilisha wai kupigiwa cm na watu wa dizaini hiyo..but mwisho wa picha nikawataperi wao.baada ya kujua nimewaingiza king walinituka sana hahaha.
 
Wakikupigia simu kuwa mpole wachore tu πŸ˜πŸ˜πŸ˜πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ€£πŸ€£πŸ€£πŸƒβ€β™‚πŸƒβ€β™‚πŸƒβ€β™‚πŸš¬πŸš¬πŸš¬
 

Attachments

Hivi makampuni ya simu hayatambui hizi mamba kweli?!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…