Ule ukabila vipi?

Ule ukabila vipi?

Nyani Ngabu

Platinum Member
Joined
May 15, 2006
Posts
97,077
Reaction score
136,504
Maajabu haya!

Mtu ambaye walitaka kutuaminisha kuwa hakuwa anastahili kuwa mkuu wa majeshi...

Mtu ambaye tuliambiwa kapewa hiyo nafasi kwa sababu ya kabila lake la Kisukuma...

Mtu ambaye tuliambiwa kapewa hiyo nafasi na Msukuma mwenzake kwa sababu za kimkakati ili kulinda maslahi ya Wasukuma...

Ndo huyu huyu tunayeambiwa sasa hivi na walewale waliotuambia kwamba Usukuma wake ndo umemfikisha hapo alipo kuwa ndo alisimama kidete kumkingia kifua Rais Mama Samia Hassan, ambaye si tu ni mwanamke, bali ni Muislamu wa kutoka Zanzibar dhidi ya kundi liitwalo ‘Sukuma gang’ lililotaka kuihujumu katiba na kumchezea rafu Mama Samia?

Yaani huyu Msukuma Venance Mabeyo ndo aliwachenjia Wasukuma wenzake waliotaka kupora madaraka?

Yaani huyu Msukuma Venance Mabeyo, ambaye ni mshamba tu kama mimi na Wasukuma wenzangu wote, na ambaye pia ni kilaza tu kama mimi na Wasukuma wenzangu wote, ndo huyu leo anasifiwa kwa kusisitiza katiba ifuatwe na kwa kuahidi kuwa jeshi litakuwa tiifu kwa Rais wetu mpya?

Kweli kabisa huyu ndo yule Mabeyo aliteuliwa na hayati Rais Magufuli kuwa ndo mkuu wa majeshi au huyu Mabeyo wa sasa ni wa kuchonga?

Ni Msukuma kweli huyu Mabeyo? Kabisa kabisa?

Msukuma wa wapi huyu Mabeyo anayewachenjia Wasukuma wenzake namna hii?

Eti leo anapongezwa!!!! Na ni Msukuma eti!!!

Truth is stranger than fiction.
 
Back
Top Bottom