Ulaya pamenishinda narudi bongo

Status
Not open for further replies.
Mtoa mada ana umama sana ... Yaani mimi nifike euro halafu ni rudi tz nimerogwa au ...!!!! Nitafia huko huko hata kama pawe na shida kiasi gani
Ushasema unakinyaa utawezana??
 
Kinachomsumbua jamaa na kumfanya atamani kurudi bongo baada ya kufika huko na kukaa kipindi hiki kifupi ni kitu wanaita"home sickness". Ulaya hasa Scandinavia mfumo wao wa maisha ni tofauti sana ukilinganisha na tz. Huko kila mtu yupo busy na mishe zake hakuna muda wa kukaa vijiweni kupiga soga na kubishana nani zaidi kati ya Simba au Yanga ambayo tunaita "socialization". Ulaya hakuna 'socialization" kiasi kikubwa kama nchi zetu za kiafrica.

Kingine ni utofauti wa kitamaduni kwa ujumla wanaita "cultural shock" ikiwa ni pamoja na chakula. Kipindi cha miezi mi 3 hadi mwaka ni kipindi cha "transition" na "realization". Yaani ni kipindi unajifunza namna na style nyingine ya maisha ambayo ni tofauti sana na tz. Pia ni kipindi unaanza kuiona ulaya halisi sio Ile ya kusadikika kama tuisomavyo mitandaoni au tuionayo kwenye tv. Hivi ndio vitu mtoa mada anakabiliana navyo. Mtoa mada anahitaji uvumilivu wa hali ya juu kipindi hiki na kutokata tamaa kwani kuna Mambo mengi atayaona tofauti na ambavyo amesikia au akiyatarajia kuhusu ulaya. Akitoboa kipindi hiki cha transition atakuja kutuambia habari nyingine tofauti kabisa.

Nakubaliana na mchangiaji mmoja kwamba ajichanganye na wa Congo, warundi ama west Africans, hawa wenzetu wapo sharp na risk takers hivyo watamsaidia kumpa ujanja na vichochoro vya kupita japokuwa awe nao makini pia wanaweza muingiza pia chaka. Wa-tz ulaya hawana msaada sana, kuna sababu yake ambayo kuna siku nitashusha Uzi wa hii issue.

Cha mwisho, namshauri kama tayari anayo sehemu ya kulala na uhakika wa msosi hapo Sweden basi ajichukulie mwenye bahati kubwa sana na kama ni marathon basi yeye tayari yupo Mita 100 mbele ya wenzake. Mm baada ya miezi 3 nili ishiwa hela zote nilizotoka nazo tz huku nikiwa sijapata kazi bado. Ila nashukuru after kupambana sana nikapata kazi na hapo slowly nikaanza kubadili maisha yangu. Nashauri mtoa mada atulize ball mambo yatajiseti time after time. Ila kama imejishkiza tu kwa washkaji atafute mchongo ahamie Norway, Denmark au Germany. Huko kuna utofauti kidogo na namna nyingi za kuishi.

Ni hayo machache nikijaribu ku share uzoefu wangu wa miaka takribani mi5 niliyoishi scandavia na ulaya Kwa ujumla..way back 2007-2011.

Nilienda ulaya nikiwa kijana mdogo sana "fresh graduate from UDSM" and I was very ambitious. Hii ilikua ni katika kutimiza ndoto yangu tangu nikiwa secondary ya kufika na kusoma Europe.Nashukuru nilibeba box za kutosha nikajisomesha Masters na kurudi tz kujenga nchi. Sikuwahi kujuta kwenda na sikuwahi kujuta kurudi, naweza kusema "this was one of my best decision and life experience".
Ni hayo tu wananzengo...
 
Best comment
 

Habari ndio hiyo.........
 
Watu tupo kongo mwaka wa pili tunalenga madaraj hatukati tamaa itakua umesahau shida za bongo pambana mwanang kutoboa sio simpo
 
kaza
 
Lima hata mchicha mkuu au jaribu kwenda kwenye ranchi za wanyama wa kufugwa ukajitolee kuchunga wanyama bila kulipwa baadae tajiri akiona unafaa atakufikiria
 
...jaribu kujiuza..wakufir.e...maana huko mashoga wako free....hii Kazi hutafti huko...
 
Njoo inbox tuongee namna ya kupiga kazi
Haya ndo mambo yakiduanzi sipendagi nkufate inbox kufanya nin?? Msaada wowote ule we utoe hapa ili kma kuna mwingine anashida Kama yangu apate faida
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…