Ulafi na uroho wa vyakula ni tabia ya asili?

Ulafi na uroho wa vyakula ni tabia ya asili?

Mimi ni mfuatiliaji wa karibu sana wa tabia za wanyama. Wanyama wote wana ulafi wa chakula. Watapigana, wataumana mpaka kuuana kwa sababu ya chakula.

Tofauti yetu na wanyama ni dhamiri na utashi wa kujizuia, lakini kiukweli ndani mwetu tuna ulafi wa chakula. Ni vile tuna pretend tu.

Mara nyingi hata undugu unavunjika kwa sababu ya vyakula.

Ukiishi kwa ndugu wiki moja lazima mtagombana tu, na sababu kuu ni chakula japokuwa huwa tunasingizia vijisababu vingine, lakini kimsingi chakula ndicho hasa sababu kuu ya watu kugombana na undugu kufa.

Niliwahi fika msibani, nikamkuta mwanamke mmoja niliyemuheshimu sana anagombania vyakula. Kwa kweli nilimshusha hadhi sana.

Mara zote sio kwa sababu tuna njaa sana au tuna shida sana na chakula, ni vile tu tuna uroho na ulafi wa asili wa vyakula.

Hata kama una magunia ya mchele ndani, lakini bado unaweza kumnyima house girl sahani ya wali.
Na njia rahisi ya kuijua tabia ya mtu ni jinsi anavyopakua Chakula kilichopo kwa ajili yake na wengine.
 
Misibani kuna watu wanaficha maandazi na nyama kwenye mikoba[emoji3]
Mtu anachukua sahani zaidi ya moja huku akijua wenzie hawajapata.
Anachukua sahani ya kwanza halafu ile ya pili anachanganya na ile ya kwanza halafu anachukua nyingine anachagua huko nyama anajiwekea chakula anaacha.
Huu uroho uliopitiliza japo kila mtu ana madhaifu yake japo tumetofautiana ila wengine wamezidi kipimo kwakweli.

Sent from my Infinix X657B using JamiiForums mobile app
 
Japokuwa binadam ni wabinafsi ila kuna wengine wamezidi aisee.
 
Back
Top Bottom