Samcezar
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 13,096
- 22,824
Mtu mroho ni mtu ambaye anatamani kula kila anachokiona na anaweza akagusa gusa tu asile akamaliza akaacha. Mlafi ni mtu ambaye anakomoa.
Anaweza kula hadi kuvimbiwa akashindwa kuendelea ila akataka akusanye kilichobakia akaweke aendelee kula baadae.
Mtu mlafi huwa anajifikira yeye kwanza na hataki wengine wapate yeye anapofika.
Ngoja nikupe mifano. Mtu mroho anaweza kwenda kwenye harusi na akataka kuonja kila mapishi anayo yaona hapo katika vyombo vya vyakula akatamani kila anachokiona akitie mdomoni ila mwisho wa siku akianza kushiba huwa anakinai anaacha.
Mtu mlafi atataka ajaziwe sahani na ikibidi abebe na kingine aende nacho nyumbani kiwekwe kando. Huku akila kile alichowekewa katika sahani na anaweza kuwa kashiba ila akataka kurudia kula tena ili kukomoa kwasababu kwake anaona leo ikipita sitapata tena hii nafasi ya kula vitu vizuri hivi.
Ulafi ni tabia chafu na mbaya zaidi ya uroho kwasababu katika ulafi hautataka mtu mwingine apate utataka wewe ndie uwe pekee wa kupata chote.
Nilikuwa na ndugu yangu m'moja aisee muda wa msosi chakula anachochota aibu nilikuwa naona mimi. Tabia ile hakuiacha na yupo nayo kwa muda mrefu sana.
Naiskia alipokuwa mtoto alikuwa wakiwekewa chakula yeye anaanza kulilia vya wenzake na kutaka vyote awekewe yeye pekee yake hadi aibu. Sasa nilipopata hii story nikajua huyu hiki kitu kipo katika damu. Halafu sasa kwenye kutafuta aisee jamaa ni mvivu balaa. Sio mtu wa kujitafutia.
Alikaa kwa shangazi yangu , ambaye alishazoea kupika chakula mfano wali atatumia kilo na nusu na atakula yeye, binti yake , house girl, na bwana mdogo mtoto wa kaka yake na hicho chakula kikabakia hadi asubuhi wakaanzia siku. Ila jamaa alipokuja kujiegesha hapo alikuwa anapiga ile nusu na robo ya sufuria na kisiwatoshe wengine. Na hapo kajibana sana.
Mimi nikasema huu sasa sio ustaarabu. Nikatoka nae siku moja nikampa makavu kiume. Nikamwambia unajua ulafi huwa unauhusiano wa moja kwa moja na ubinafsi na uvivu. Sababu unahofu ya kutopata tena kesho kwasababu hautafuti wewe basi unaamua kukomesha ili kesho hata kisipokuwepo wewe uwe bado umeshiba au una akiba ndani.
Ila kama unatafuta unakuwa na uhakika kuwa kipo na hata kikikosekana utakwenda nunua kwa pesa yako au utaweza pata sapoti ya kupata pesa ya kununua kwa wanaokuzunguka.
Nikamwambia halafu wanaume huwa hatuli hivi kama dubu as if ukila chakula kingi unatibu njaa isijirudie tena. Nikamwambia hebu jitahidi kuwa na akiba ya pesa uwe hata unanunua vitu unapenda kula upunguze tabia ya kula chakula kingi kwa kukomoa basi kama vipi kafanye kazi kwenye mgahawa ili usiwaze sana msosi [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23].
Ila nikaona jamaa bado zile tabia hajaacha na lecture yote ile nilimpa ambayo nilimuelekeza namna za kupunguza ulafi. Ila yeye anaona kama unaongea vitu gani mimi siwezi acha kula kiasi nataka kwasababu watu wananisema vibaya.
Nikasema wacha nimuache. Hapa nawaandikia hivi bado jamaa hajaacha hii tabia. Na huwa anavunga tu akiwa mazingira fulani ila mfano aende kwa bi mkubwa especially siku za sikukuu chombo atakachoweka chakula wakati anakula huwa kama sio bakuli kubwa basi ni zile sinia za kulia biriani hizi sahani huwa hapendi.
Mimi huwa nakerekwa na ile tabia aiseeeee daaaaah.