Ulafi na uroho wa vyakula ni tabia ya asili?

Ulafi na uroho wa vyakula ni tabia ya asili?

GODZILLA

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2014
Posts
5,914
Reaction score
10,585
Mimi ni mfuatiliaji wa karibu sana wa tabia za wanyama. Wanyama wote wana ulafi wa chakula. Watapigana, wataumana mpaka kuuana kwa sababu ya chakula.

Tofauti yetu na wanyama ni dhamiri na utashi wa kujizuia, lakini kiukweli ndani mwetu tuna ulafi wa chakula. Ni vile tuna pretend tu.

Mara nyingi hata undugu unavunjika kwa sababu ya vyakula.

Ukiishi kwa ndugu wiki moja lazima mtagombana tu, na sababu kuu ni chakula japokuwa huwa tunasingizia vijisababu vingine, lakini kimsingi chakula ndicho hasa sababu kuu ya watu kugombana na undugu kufa.

Niliwahi fika msibani, nikamkuta mwanamke mmoja niliyemuheshimu sana anagombania vyakula. Kwa kweli nilimshusha hadhi sana.

Mara zote sio kwa sababu tuna njaa sana au tuna shida sana na chakula, ni vile tu tuna uroho na ulafi wa asili wa vyakula.

Hata kama una magunia ya mchele ndani, lakini bado unaweza kumnyima house girl sahani ya wali.
 
Hizo ni stage tu za maisha tunapitia.
Kuna wakati mawazo yako yatakuwa ni chakula tu hata utawanyima watu wengine.
Kuna kipindi utaacha kuwaza chakula utawaza pesa tu. Yaani utampa chakula ila pesa haupo tayari kumpatia.
Na kuna stage utafika utaanza kuwaza muda.Hiyo pesa utaitoa tu mradi muda usipotee.
 
Asa mkuu GODZILLA kama unajua uroho na ulafi wa vyakula ni asili ya binadamu kama ulivyoandika hapo,kwanini umshushe huyo mwanamke wa msibani?
Sikutarajia asee!

Vile alivyokuwa amesimama kidete huku kafunga kibwebwe.....Dooohh!

Nilificha uso kwa aibu!
 
Back
Top Bottom