Ukweli wa ziara ya Warioba wilaya ya Bunda

Ukweli wa ziara ya Warioba wilaya ya Bunda

Mkuu nadhani unamuongelea huyu mzee amepoteza mwelekeo hana jipya kaisha tena ndiyo anazidi kujimaliza.

Anajimalizaje wakati alishalitumikia taifa miaka na miaka na sasa amestaafu anakula pensheni yake bila shida? Unafikiri warioba ana ambitions nyingine zozote zaidi ya kutaka kutuachia watoto wake uridhi uliotukuka? Warioba ametengeneza historia ambayo haitasahaulika miongoni mwa watanzania kwa miaka mingi ijayo! Maccm bwana hata hamna akili!
 
Shida sio serikali tatu tu shida ni tunu za taifa, madaraka ya rais, muda wa ubunge na kuwawajibisha wabunge! Wanawake, ardhi, wafugaji na wakulima hawajahakikishiwa haki zao kwenye katiba ya CCM!

Ndio mkuu watu wengi wanadhani kutambuliwa tu na katiba tayari wameshapata haki zao, haki zilitakiwa kuandikwa kwenye katiba na c kusubiri kuja kutungiwa sheria ilo ni changa la macho ni muda tu utajieleza
 
Wasira akimuogopa Waryoba mimi najinyonga, tuulize sisi watu wa Bunda, tunajua Mzee wetu anatmiwa na watu wa kaskazini kwa manufaa yao siyo ya Watanzania.

Sema wewe, siyo eti sisi watu wa bunda.
 
Anajimalizaje wakati alishalitumikia taifa miaka na miaka na sasa amestaafu anakula pensheni yake bila shida? Unafikiri warioba ana ambitions nyingine zozote zaidi ya kutaka kutuachia watoto wake uridhi uliotukuka? Warioba ametengeneza historia ambayo haitasahaulika miongoni mwa watanzania kwa miaka mingi ijayo! Maccm bwana hata hamna akili!
Nnape keshawamaliza akili kwa mshahara wa buku 7. Hawajitambui akili zao zinawaza kukunwa tigo tu
 
Mzee warioba jina lake litabaki milee kwenye miyoyo ya watanzania na dunia
 
Danganya watoto wa sekondari siyo watu wazima kama siye pengine bavicha wenzako.

Kwani kuna kosa gani Warioba kufanya kongamano? Mbona JK anazunguka akifanya kampeni ya Katiba iliyopitishwa kimagumashi?
 
Kuna MwanaCCM hapa JF anajiita WA TANGA. mtu huyu kaandika rundo la propaganda dhidi ya Ziara ya Jaji Warioba.

Ieleweke Jaji Warioba wala CHADEMA au Ukawa hawajaanda Makongamano ya Warioba Bunda au Butiama.

Kilichotokea ni Baada ya Warioba kufika kijijini kwao Nyamswa kusalimia kama ada za kiafrika. Na Taarifa za uwepo Wa Warioba Bunda zilivyojiri Mjini. Basi Mara moja waumini Wa serikali tatu wakatengeneza kamati ya kumshawishi Warioba afanye Mhadhara juu ya kinachoitwa Katiba Pendekezwa.

Kamati hiyo ya waumini Wa serikali Tatu Bunda ilifika Nyumbani kwa Warioba jumatatu tarehe 13/10/2014. Na Warioba akaikubalia kamati waandae kongamano naye atatoa Mada hiyo.

Kongamano likaandaliwa na kamati na kufanyika Leo ukumbi Wa Heriet Mjini Bunda. Na Sasa linaendelea hadi SAA kumi na mbili jioni.

Gharama za Kongamano hili ni michango ya waumini Wa rasmu ya Warioba. Hasa wakazi Wa Bunda Mjini.

Fedha hizi hazikupatikana kutoka ukawa Bali michango ya watu Wa Bunda.

Maelezo haya ni kutoka kwa mratibu Wa kamati Hui Mjini Bunda.

Bw Daniel Ayot Charles

Hivyo Wassira kama hautaki jinyonge

Kifupi Warioba haitakii mema nchi hii na anadanganywa na UKAWA awe mgombea urais kwa chadema.
 
Last edited by a moderator:
toeni namba ya mpesa tuchangie hilo kongamano na harakati zake zingine huyu mtu mwema warioba..Go warioba....ikibidi niite na mm nikusaidie sehem zote za vijijini huko mkoani kwetu mara na kwingneko
 
toeni namba ya mpesa tuchangie hilo kongamano na harakati zake zingine huyu mtu mwema warioba..Go warioba....ikibidi niite na mm nikusaidie sehem zote za vijijini huko mkoani kwetu mara na kwingneko

Ntakutumia contact za bw Daniel Ayot. Mratibu Wa ziara hizi Bunda.
 
Kwani UKAWA si watanzania?Wanaohoji wanafiki tu.Hata kama UKAWA wakichangia ni halali pia.
 
Mimi nadhani kuna watu eidha Kwa makusudi au kwakutojua maudhui ya mada hii wanazungumza vitu Vya ovyo ovyo' suala" kwani kuzungumzia mtu kutumia kinywaji au chakula fulani ni aina ya udhalilishaji kwanza mtu kama Warioba wanaemdhihaki ni mtu wa viwango ambaye hakuna wa kimfananisha kwa watawala waliopo chama tawala kwa ulinganifu wa itaifa, uzalendo kwa TAIFA na watu wake, uadilifu, upeo wa kupambanua mambo na hata malengo kwa taifa na mengine mengi" na isitoshe watanzania wa leo si wale waliozoeleka kudanganywa na kulazimishwa mambo" wanauaona yanayoendelea' wanachukizwa nayo" ila wananyamaza kwakuwa eidha watanyanyaswa katika biashara zao' masomo yao au ktk shughuli zao za kila siku, ila hukumu ya haya yote ni siku moja. Endeleeni kujidanganya na muaminiyo.

Mwenye macho hata siku moja haongozwi na kipofu.

Viva mzee Warioba, viva watanzania.
 
Back
Top Bottom