Ukweli wa mambo kuhusu mama aliyeamua kuishi uchi juu ya paa la nyumba huko mbezi beach

If Lions could speak....

Hii story imekaa upande mmoja tu wa kumshtumu huyo mama na kuonesha TIB na Msama wako sahihi.

Ningependa kusikia pia upande wa wenye nyumba unasemaje
hata alipokaa juu ya paa na vyombo vya habari kuandika pia ilikua ya upended mmoja. Huyu mkopaji ni msanii huto kaa upate habari kutukana kwake. Tulichangia habari hii wengine ikapigwa ban toka mwanzo ilionyesha ni usanii mtupu
 
Dawa ya deni KULIPA,HATA UKIANIKA PAPUCHI HUJALIPA,,,NA AT THE SAME TIME MAMA MWENYEWE ANAJIDHALILISHA

Naam, kweli kabisa. Kukopa asali kulipa shubiri.

Mimi nadhani huyo mama anatafuta huruma ya umma tu maana umma haunaga muda wa kuchunguza, kuchanganua, na kupembua pumba na mchele.

Mimi nilitegemea kama kweli ana madai halali basi angeenda kushinda mahakamani na kudai haki yake huko kuliko kupanda kwenye paa na khanga yake moko na kujitia majnun.

Sasa yadaiwa kumbe hata si mke halali na mke halali tayari keshaenda mahakamani. Haya mambo bana...wakati mwingine kuujua ukweli huwaga ni ngumu sana.
 
Akili za kukolezea na moto. Urafiki wa kukopeana milioni 270? Bongo?

Hata mi nimeshangaa sana mtu kuweka nyumba yake collateral kwa mkopo wa mtu mwingine.

Nimpongeze tu mbeijing mwenzangu kwa kuwa so dramatic kutetea small hausi.

Anahitaji tuzo ya Oscar kwa kuwa melodramatic maana stunt aliyo-pull si ndogo na kama huruma toka kwa umma kaipata.

Sasa subiri na yeye aje kudai kuwa yeye ndo mke halali. Hapatatosha.
 
hiyo habari haina mashiko manake hata mimi nimeisoma ktk gazeti la DIRA, pia hata asubuhi blouse fm waliipa promo kwenye uchambuzi wao wa magazeti... naona kama kujitetea vile, ukweli utadhiri tu na haki itatendeka.. kwa nini washikilie bango kuwa huyo mama si ndoa halali ya mwenye nyumba? hata kama ni nyumba ndogo lakini haki anayo na ndo mana anaishi humo.
 
hiyo habari haina mashiko manake hata mimi nimeisoma ktk gazeti la DIRA, pia hata asubuhi blouse fm waliipa promo kwenye uchambuzi wao wa magazeti... naona kama kujitetea vile, ukweli utadhiri tu na haki itatendeka.. kwa nini washikilie bango kuwa huyo mama si ndoa halali ya mwenye nyumba? hata kama ni nyumba ndogo lakini haki anayo na ndo mana anaishi humo.

Ana haki gani sasa? Kama ana haki kwa nini asiende kushinda mahakamani?

Wao kama walikopa na walipe tu deni la watu, basi.
 
Akili za kukolezea na moto. Urafiki wa kukopeana milioni 270? Bongo?

Nimpongeze tu mbeijing mwenzangu kwa kuwa so dramatic kutetea small hausi. Alikuwa ananikera tu kwa kutovaa nguo. Kitu cha kujifunza kwa mke halali, hizi mambo za kusubiria miujiza ya ndoa sio zenyewe. Si mpeane talaka tu mgawane mali, kamamuujiza ukitokea mkarudiana si mtafunga ndoa upya? Ulaya wanafanya kila siku!


Acha kabisa rafiki, mzee wetu alishafanya huu 'ujinga', na tukapoteza nyumba tunajiona.....
 
Dawa ya deni
KULIPA,HATA UKIANIKA PAPUCHI HUJALIPA,,,NA AT THE SAME TIME MAMA
MWENYEWE ANAJIDHALILISHA

Kweli mkuu,dawa ya deni ndio hivyo! Na pia matumizi ya kuonyesha maeneo tulikotokea mbele ya jamii sii dawa bali ni kutafuta sympathy ya wananchi kijinga!
 
Back
Top Bottom