Ukweli wa mambo kuhusu mama aliyeamua kuishi uchi juu ya paa la nyumba huko mbezi beach


MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Messages
40,027
Likes
5,487
Points
280
MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined Feb 3, 2009
40,027 5,487 280
[h=3][/h]


WIKI iliyopita kuliibuka sakata zito lililochukua nafasi kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii, lililomuhusisha mama mmoja aliyejulikana kwa jina la Hezelina Mrema mkazi wa Mbezi Beach, eneo la Tangi Bovu jijini Dar es Salaam, kuamua kuishi juu ya paa la iliyodaiwa kuwa ni nyumba yake.Hatua hiyo ilisababisha baadhi ya wanaharakati kujitokeza na kuahidi kumsaidia mama huyo, aliyedai kuwa anataka kutolewa kwa nguvu ndani ya nyumba yake halali, ambayo ameijenga na mumewe Samwel Opulukwa.

UKWELI WA MAMBOUkweli juu ya suala hilo ni kwamba Hezelina hahusiki kwa namna yeyote na nyumba hiyo, ambayo ni ghorofa moja, kwani imebainika kuwa si mke halali wa Opulukwa na badala yake wana mahusiano ya kimapenzi.Imebainika kuwa mke halali wa Opurukwa alisha achana nae na mke wake huyo tayari alishaweka pingamizi Mahakamani la kutaka hati ya nyumba hiyo isibadilishwe mmiliki.Mbali ya Hazelina kutokuwa mke halali wa Opulukwa pia imebainika kwamba mwanaume huyo aliitumia nyumba hiyo kuweka dhamana ya mkopo kwenye benki ya TIB.Imebainika kuwa hatua ya Opulukwa kuweka nyumba yake dhamana ilikuja baada ya rafiki yake ambaye ni mmiliki wa kampuni ya Asasu Express Ltd kuhitaji fedha za kuendeshea bishara yake, lakini alikumbana na kikwazo cha kutakiwa kuwa na nyumba jijini Dar es Salaam, ambapo kwa kuwa hakuwa nayo aliona amtumie rafiki yake huyo kufanikisha mkopo wake kwa makubaliano kuwa ataulipa bila tatizo.


Hata hivyo mmiliki huyo wa kampuni ya Asasu alishindwa kulipa mkopo huo wa mamilioni ya fedha, ambapo benki husika ilianza harakati za kutaifisha mali zake ili kufidia deni hilo, hata hivyo hazikutosha na ndipo walipoamua kuiuza nyumba hiyo ya Mbezi Beach iliyopo kiwanja namba 235 Block D.
Imeelezwa kuwa benki ya TIB ilimpa Opulukwa taarifa zote za deni husika pamoja na kumpa Notisi ya kumtaka alipe deni husika ambalo ni 274,854, 256. 84 kutokana na rafiki yake kushindwa kulipa deni husika pamoja na mali zake kutaifishwa.


Ili kufuata taratibu za kisheria za kutaifisha nyumba ya Opulukwa, benki hiyo ilitoa tangazo la kutoa tenda ya kuuza nyumba hiyo, ambalo lilitolewa kwenye gazeti la serikali Januari 10,2011.


Hata hivyo Opulukwa hakutoa ushirikiano wowote, hali iliyosababisha benki ya TIB kuipiga mnada nyumba hiyo na kufanikiwa kupata mteja, ambaye aliinunua kihalali ikiwa ni pamoja na kubadilisha hati miliki ya nyumba hiyo.Jambo la kushangaza Opulukwa aliendelea kuishi ndani ya nyumba hiyo, TIB ilifanya harakati za kumtoa kwa kuyatumia makampuni kadhaa ya udalali ambayo yalishindwa kufanikisha kazi hiyo na ndipo Machi mwaka huu, jukumu hilo la kumtoa Opulukwa lilipelekwa kwa kampuni ya udalali ya Msama Auction Mart.


Baada ya Kampuni ya Msama Auction Mart kufanya taratibu zake za kikazi na kuridhishwa na uwepo wa deni husika, Juni 8, mwaka huu ilifika eneo la tukio na kuanza kumtoa Opulukwa.


Hata hivyo zoezi hilo lilikuwa gumu kutokana na baadhi ya maofisa wa Polisi wa Wilaya ya Kinondoni kuingilia kati, ambapo waliitisha kikao cha pamoja kati ya maofisa wa kampuni ya Msama Auction Mart na Opulukwa, ambapo maamuzi yalikuwa ni kusimamisha zoezi hilo hadi pale mkopaji huyo atakapopata baraka za Mahakama juu ya uhalali wa kuendelea kuishi kwenye nyumba hiyo.Baada ya maamuzi hayo ya jeshi la polisi, Opulukwa alifungua kesi ya madai ya kuvunjiwa nyumba yake na kuibiwa vifaa vyenye thamani ya shiringi 195 milioni, jambo ambalo halikuwa na ukweli wowote.


Juni 11, mwaka huu mara baada ya Opulukwa kukosa vielelezo vilivyompa uhalali wa kuendelea kuishi ndani ya nyumba hiyo kama alivyoagizwa na Mkuu wa Polisi wilaya Kinondoni, kampuni ya Msama Auction Mart iliendelea na zoezi la kumuondoa.


Wakati maofisa wa kampuni ya Msama Auction Mart wakiwa na uhakika wa kukamilisha zoezi lao pamoja na kuondoka eneo hilo,ghafla walipigiwa simu na walinzi walioachwa kwenye eneo hilo kuwa kuna mtu yupo ndani ya nyumba, ambaye inaelezwa aliruka ukuta ili kufanikisha lengo lake.Hatua hiyo ya Hazelina iliwashangaza maofisa wa Msama Auction Mart, ambao walichukua jukumu la kupiga simu polisi ili kuhakikisha mama huyo anaondolewa kwa njia ya amani na utulivu.Wakati huo tayari Hazelina alikuwa ameshapanda juu ya paa la nyumba hiyo, huku akitishia kujirusha ili kuutoa uhai wake endapo angetolewa kwa nguvu.


Aidha alikwenda mbali zaidi kwa kuvua nguo ili kuonesha utupu wake, lengo lake likiwa ni kutowapa nafasi walinzi wa kiume kutomsogelea.


Hatua ya mama huyu kuonesha utupu wake na kuendelea kukaa juu ya paa la nyumba hiyo ilizua maswali na kuwafanya baadhi ya waandishi wa Habari kufika eneo hilo ili kujua ukweli wa mambo.

Kutokana na kauli za uongo za mama huyo, alifanikisha kuwaaminisha waandishi wa habari kuwa kuna hila zinafanyika ili kupora nyumba yake, ambayo alidai kuwa ni halali yao.Hata hivyo maamuzi ya mama huyo kuendelea kukaa juu ya paa la nyumba hiyo, yalidumu kwa muda wa siku mbili, ambapo Juni 13, mchana kwa hiyari yake aliamua kushuka baada ya kumuona jamaa yake akiwa ameshikilia karatasi zilizodaiwa kuwa zimetoka Mahakama ya Kinondoni.Uchunguzi wa wetu umebaini kuwa Opulukwa hakumueleza ukweli mama huyo, ambapo ukweli halisi wa zoezi zima la kuhamishwa kwenye nyumba hiyo analijua.


Aidha imebainika kuwa mwanamama huyo si mke wa Opulukwa, kwani mke wake halali anajulikana kwa jina la Rachel Paulo Ng’wahi, amabaye ndiye aliyefungua kesi ya kupinga hatua ya mume wake kutumia nyumba yao kumuwekea dhamana ya mkopo rafiki yake ambaye ni mmiliki wa kampuni ya Asasu.Ukweli ni kwamba benki ya TIB na kampuni ya Msama Auction Mart, walikuwa sahihi kumuondoa Opulukwa kwenye nyumba hiyo, hakuna sheria yeyote waliyoivunja na hawakuwa na nia ovu ya kutaka kumpora mama huyo na Opulukwa aliyedai kuwa ni mumewe nyumba kama alivyodai kwenye vyombo vya habari.


chanzo. UKWELI WA MAMBO KUHUSU MAMA ALIYEAMUA KUISHI UCHI JUU YA PAA LA NYUMBA HUKO MBEZI BEACH - MPEKUZI HURU
 
Mkoroshokigoli

Mkoroshokigoli

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2012
Messages
14,621
Likes
2,691
Points
280
Mkoroshokigoli

Mkoroshokigoli

JF-Expert Member
Joined Dec 20, 2012
14,621 2,691 280
Hiyo nyumba,itasumbua hat miaka mia,ndo zilivyo kes hizo
 
Puppy

Puppy

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2011
Messages
2,415
Likes
817
Points
280
Puppy

Puppy

JF-Expert Member
Joined Oct 6, 2011
2,415 817 280
If Lions could speak....

Hii story imekaa upande mmoja tu wa kumshtumu huyo mama na kuonesha TIB na Msama wako sahihi.

Ningependa kusikia pia upande wa wenye nyumba unasemaje
 
mwekundu

mwekundu

JF-Expert Member
Joined
Mar 4, 2013
Messages
21,031
Likes
10,394
Points
280
mwekundu

mwekundu

JF-Expert Member
Joined Mar 4, 2013
21,031 10,394 280
If Lions could speak....

Hii story imekaa upande mmoja tu wa kumshtumu huyo mama na kuonesha TIB na Msama wako sahihi.

Ningependa kusikia pia upande wa wenye nyumba unasemaje
Ni kweli kabisa ,kiuhalali tumesikiliza upande mmoja tu!!


Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Mkoroshokigoli

Mkoroshokigoli

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2012
Messages
14,621
Likes
2,691
Points
280
Mkoroshokigoli

Mkoroshokigoli

JF-Expert Member
Joined Dec 20, 2012
14,621 2,691 280
Dawa ya deni KULIPA,HATA UKIANIKA PAPUCHI HUJALIPA,,,NA AT THE SAME TIME MAMA MWENYEWE ANAJIDHALILISHA
 
jamii01

jamii01

JF-Expert Member
Joined
Oct 1, 2010
Messages
1,872
Likes
456
Points
180
jamii01

jamii01

JF-Expert Member
Joined Oct 1, 2010
1,872 456 180
Muwe makini,mnapokopa kwenye haya mabenk hayana ubinadamu hata kidogo,bora mkimbilie kwenye saccoss hata kama mikopo yenyewe ni kidogo.
 
King'asti

King'asti

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2009
Messages
27,677
Likes
2,791
Points
280
King'asti

King'asti

JF-Expert Member
Joined Nov 26, 2009
27,677 2,791 280
Akili za kukolezea na moto. Urafiki wa kukopeana milioni 270? Bongo?

Nimpongeze tu mbeijing mwenzangu kwa kuwa so dramatic kutetea small hausi. Alikuwa ananikera tu kwa kutovaa nguo. Kitu cha kujifunza kwa mke halali, hizi mambo za kusubiria miujiza ya ndoa sio zenyewe. Si mpeane talaka tu mgawane mali, kamamuujiza ukitokea mkarudiana si mtafunga ndoa upya? Ulaya wanafanya kila siku!
 
R

rweiki

Member
Joined
Feb 23, 2010
Messages
40
Likes
0
Points
0
R

rweiki

Member
Joined Feb 23, 2010
40 0 0
Opulukwa labda amuombe mdogo wake fedha mbunge wa chadema Meatu amsaidie kufa kufaana naye si aliwabeba sana tu!

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Dancani

Dancani

JF-Expert Member
Joined
Apr 4, 2012
Messages
798
Likes
23
Points
35
Dancani

Dancani

JF-Expert Member
Joined Apr 4, 2012
798 23 35
morphine

morphine

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2012
Messages
3,089
Likes
358
Points
180
morphine

morphine

JF-Expert Member
Joined Jan 26, 2012
3,089 358 180
Ewaaa kumbe huu ndio ukweli wenyewe na sio ule wa ile post ingine? Au TIB bank wamekuja humu kundini kujisafisha wajameniiiii.....
 
Mkoroshokigoli

Mkoroshokigoli

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2012
Messages
14,621
Likes
2,691
Points
280
Mkoroshokigoli

Mkoroshokigoli

JF-Expert Member
Joined Dec 20, 2012
14,621 2,691 280
Opulukwa labda amuombe mdogo wake fedha mbunge wa chadema Meatu amsaidie kufa kufaana naye si aliwabeba sana tu!

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums

rweiki sidhan maana they are very selfish,,,,
unless amwambie mjomba wao mzee NIMROD MKONO,
 
Last edited by a moderator:
Dancani

Dancani

JF-Expert Member
Joined
Apr 4, 2012
Messages
798
Likes
23
Points
35
Dancani

Dancani

JF-Expert Member
Joined Apr 4, 2012
798 23 35
Akili za kukolezea na moto. Urafiki wa kukopeana milioni 270? Bongo?

Nimpongeze tu mbeijing mwenzangu kwa kuwa so dramatic kutetea small hausi. Alikuwa ananikera tu kwa kutovaa nguo. Kitu cha kujifunza kwa mke halali, hizi mambo za kusubiria miujiza ya ndoa sio zenyewe. Si mpeane talaka tu mgawane mali, kamamuujiza ukitokea mkarudiana si mtafunga ndoa upya? Ulaya wanafanya kila siku!
Sio hizo tu alizomdhamini kukopa, hizo milion 270 ni zilizobaki kukamilisha deni, ila kiasi halisi walichokopa hakitajwi maana habari za awali zinasema zimeshauzwa nyumba mbili na mali kadhaaa za yule rafiki yake ila bado linabaki deni hilo.
 
King Kong III

King Kong III

JF-Expert Member
Joined
Oct 15, 2010
Messages
32,810
Likes
15,253
Points
280
King Kong III

King Kong III

JF-Expert Member
Joined Oct 15, 2010
32,810 15,253 280
Source Dira =Msama Auction Mart
 
M

Mshirazy

JF-Expert Member
Joined
Mar 21, 2013
Messages
421
Likes
4
Points
0
M

Mshirazy

JF-Expert Member
Joined Mar 21, 2013
421 4 0
Huyo jamaa ni waajabu sn!yaan anakubali kuweka rehani nyumba yake ili kumridhisha rafiki!ona sasa yanayomkuta!
 
Nyanidume

Nyanidume

JF-Expert Member
Joined
Oct 24, 2012
Messages
2,336
Likes
547
Points
280
Nyanidume

Nyanidume

JF-Expert Member
Joined Oct 24, 2012
2,336 547 280
Huyo jamaa ni waajabu sn!yaan anakubali kuweka rehani nyumba yake ili kumridhisha rafiki!ona sasa yanayomkuta!
Huujui urafiki wao ni wa namna gani, otherwise asingefanya hivyo.
 

Forum statistics

Threads 1,273,084
Members 490,268
Posts 30,470,668