Potea wa potea
Senior Member
- Oct 9, 2013
- 117
- 28
Mimi nilishsjitoa huko muda mrefu
Cdm kwani bado ipo?
![]()
Malalamiko mengi yamezuka hususani ugawaji wa viti maalumu ya ubunge na udiwani ndani ya chama kikuu cha upinzani nchini. Mitandoni maoni na malalamiko yamesheheni kiasi kwamba mtu unaweza kuanza kufikiria 'Chadema mbioni kufa'? Watu wanatoa hoja mbalimbali na zingine ni za msingi kabisa, ni vema sababu hizi zikachukuliwa kwa uzito wa hali ya juu, badala ya kuzipuuza na hivyo kuhatarisha uhai wa chama hiki kinachoonekana ni tumaini la Watanzania kwa mabadiliko ya nchi hii.
Siku moja asubuhi nilipigiwa simu kutoka Dar es Salaam na mwanachama mmoja aliyelalamikia suala la upendeleo wa kikanda katika ugawaji vyeo na viti maalumu vya ubunge na udiwani. Ukipita katika kona nyingi za nchi yetu hutakosa kusikia watu wakilijadili suala hili la upendeleo ndani ya Chadema hasa katika kipindi cha kuanza kipindi kipya cha uongozi katika nchi yetu.
Mimi najiuliza je, malalamiko hayo ni ya kweli au ya kutungwa. Ni muda mrefu sasa watu wengi wamekituhumu Chadema kuwa kina mbegu ya upendeleo kwa wanachama wake. Ni vema viongozi wakuu wa chama hicho na washauri wao wakalichukulia jambo hili kwa uzito mkuu.
Kinachoonekana ni kwamba kuna baadhi ya wanachama katika maeneo mbalimbali ya nchi wametumia muda wao, akili na hata mtaji wa pesa zao kukijenga chama, lakini linapokuja suala la uteuzi wa vyeo na viti maalumu wanajikuta wanaachwa. Je, suala hilo lipoje ndani ya chama hicho kikuuu cha upinzani nchini.
Watu wanahoji inakuwaje, mtu anakuwa kiongozi ndani ya chama na anajitahidi kufanya yale yanayompasa kufanya kwa bidii na akachukua fomu ya kugombea kiti maalumu, lakini fomu yake ikapotea ofisini? Hujuma kama hii inaweza kuelezwaje na watendaji wakuu? Kama ni kweli mambo hayo yapo hata ndani ya Chadema wakati tulizoea kuyasikia yakitendeka zaidi ndaniya chama kikongwe CCM, kumbe sasa huo ugonjwa unaonekana kusambaa hata ndani ya Chadema.
Inakuwaje, watu wanahoji viongozi karibu wote makao makuu, viti maalumu ni kutoka Kaskazini, hili linatoa taswira gani ya chama kinachojinasibu ni chama mbadala wa chama tawala (CCM). Ukweli ni kwamba kama Chadema inataka kueleweka kama ndiyo chama mbadala cha CCM katika nchi hii lazima kijaribu kuepuka mitego yote ya chama tawala, kama upendeleo wa kikabila, udini, ukanda , na u-familia, urafiki na upambe. Watanzania tulilelewa na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere kwa kutaka sote tuwe sawa, tuheshimiane, tujaliane, tusaidiane na tusibaguane katika jambo lolote lile. Na dini zetu zisiwe ndiyo chanzo cha kuvuruga amani yetu kwani nchi hii haina dini ila kila mtu ana dini yake kitu ambacho ni imani yake binafsi isiyoingiliwa na itikadi yoyote na hata Serikali haiingilii.
Watanzania wanafikiri kwamba katika sehemu ambazo Chadema bado haijaeleweka ilikuwa ni muda mwafaka kuteua wanachama wa sehemu hizo ambao wametumia nguvu na muda wao kukijenga chama hicho kushika nafasi mbalimbali. Watanzania wanasema hii ingekuwa ni njia mojawapo ya kukijenga chama badala ya kukibomoa kwa kufanya upendeleo kama unavyoelezewa na kulalamikiwa na baadhi ya wanachama na wananchi kwa ujumla. Ni wazi kwamba Chadema bado ina kazi kubwa ya kujisambaza katika kila kona ya nchi hii yenye ukubwa mwingi na mahitaji tofauti ya wananchi wake.
Wananchi na baadhi ya wanachama wanalalamikia suala la kuachwa vijana ambao ndiyo moyo au nguzo ya chama cha Chadema katika teuzi za hivi karibuni. Inafahamika wazi kwamba taifa lolote bila kujali vijana basi linakuwa limekufa kabisa. Vijana ndiyo taifa na leo na kesho ambao lazima watazamwe kwa jicho la pekee katika jamii yoyote ile. Vijana wasiwe wanatumika tu kuwavusha wanasiasa (vigogo) wakati wa uchaguzi kama huo uliopita, halafu baada ya hapo wanawekwa kando na kusubiria tena miaka mitano ijayo watakapohitajika. Ni vema Chadema ikaanza kuamka kutokana na makosa yanayofanyika ili kiweze kujirekebisha kama vile waswahili wasemavyo ?kosa siyo kufanya, bali kulirudia kosa.?
Chadema acheni kujifanya viziwi wa kutosikia malalamiko na vilio wanavyotoa wananchi na baadhi ya wanachama wenu kwani ?lisemwalo lipo na kama halipo, linakuja.? Chadema acheni kujifanya vipofu wa kutokuona ukweli wa yale yanayofanyika ndani ya chama chenu, chukueni hataua sasa. Kwa upande wangu hali hii inatisha katika medani ya siasa zetu za demokrasia na utawala bora, na ndiyo maana naandika kwa kuthubutu kwamba ?Chadema mbioni kufa?? Najua makala haya hayatapendwa na baadhi yenu katika chama, lakini huwa nina amini kuwa ukweli utakuweka huru.Na wataalamu wanasema kwamba ?mtu anayekupenda ni yule anayekukosoa na kukuambia ukweli, badala ya yule mnafiki anayekuchekea na kukusifia mambo ya nje tu, au anayekupaka mafuta kwa mgongo wa chupa.?
Napenda kuwaasa Chadema kuchukulia kwa uzito wa pakee yale yanayosemwa katika kipindi hiki cha Uchaguzi Mkuu uliokwisha ili kuweza kujipanga vizuri zaidi. Ukweli ni kwamba pamoja na mikakati na mbinu lazima zipangwe, lakini Chadema lazima kisome alama za nyakati mapema zaidi. Kwa mfano sasa baada ya uchaguzi huu ambao unasemwa na baadhi ya wananchi umepora ushindi wa Ukawa lazima chama kijiulize ni kwa nini kilishindwa uchaguzi huo? Je, ni makosa gani chama kimefanya katika uchaguzi huo? Na sasa ni wazi kwamba wananchi wengi wanaona wazi kwamba bila kuwa na Katiba Mpya ambayo ina tume huru ya uchaguzi , CCM itaendelea kutawala milele. Hiyo ni changamoto kubwa kwa Ukawa na wapenda mabadiliko wote nchini, sasa kazi ni moja tu kudai Katiba Mpya yenye tume huru ya uchaguzi na kanuni safi za uchaguzi.
Mungu ibariki Tanzania na watu wake.
Chanzo; Makala Mwananchi
Chadema wanapumulia mashineCdm kwani bado ipo?
Chadema wanapumulia mashine
Teh Teh au kimachame...!Ungeandika kichaga labda ila kwakiswahili hapo umetwanga maji kwenye kinu
ni kweli kabisa MKUU aliyeasisi huu utabiri kwamba CHADEMA itakufa ni Steven Masatu Wassira ambaye yeye mwenyewe ameuawa kisiasa na CHADEMA hiyo hiyo tena kupitia Kamanda mwanamke. Lakini ukiangalia trend ya CHADEMA tangu kuanzishwa kwa vyama vingi utaona kwamba CHADEMA inazidi kuimarika kwenye kila uchaguzi na imezidi kuongeza viti vya vitongoji, vijiji,mitaa,madiwani, wabunge, kura za urais na idadi ya Halmashauri zinazoongozwa na CHADEMA. Ukiangalia kwenye kila uchaguzi CCM ndicho chama kinachoongoza kwa kupoteza kura nyingi na viti ilivyokuwa inavishikilia kuanzia ngazi ya vitongoji, vijiji, mitaa,kata,bunge,Halmashauri na kura za Rais. CCM pia imepoteza idadi kubwa ya viti maalumu na kiasi cha ruzuku ya vyama vya siasa iliyokuwa ikipata kutokana na kuporwa kura nyingi na CHADEMA hii hii ambayo propaganda zinasema itakufa! Ni matarajio yangu uchaguzi ujao wa 2020 CHADEMA itafanya vizuri zaidi ya mwaka huu kwa kuwa watanzania wengi wana imani nayo na ndiyo jicho lao kuhakikisha maslahi yao hayahujumiwi na CCM.CCM itaendelea kuporomoka hasa kwenye ngazi za vitongoji, vijiji, mitaa,kata na majimbo kwa sababu wagombea wa CCM hasa Wa vijijini na baadhi ya mikoa wanabebwa na wapiga kura wao kutokuwa na elimu ya urais ambao wanaamini propaganda wanazolishwa kwamba CHADEMA ni chama cha wachaga,cha wakristo,CHADEMA ikitawala kutatokea vita nk.Kadiri siku zinavyokwenda CHADEMA imekuwa ikipambana na propaganda hizo kwa nguvu kubwa kwa kwenda vijijini kwenye mikoa yote kukieneza chama na kufuta propaganda zote chafu kazi ambayo imezaa matunda na mafanikio kuonekana. Pamoja na kwamba CHADEMA haikupata majimbo mengine lakini utaona tofauti ya kura naona ya wagombea wa CCM na CHADEMA kwenye majimbo na kata CCM walizoshinda ni ndogo kulinganisha na chaguzi za nyuma ambopo ana CCM ilipota bila kupingwa ana tofauti ya kura ilikuwa kubwa sana.Ukiacha ushabiki wa wana ccm hapa jf na wale WA vijiweni pamoja na baadhi ya viongozi wasiojitambua kama Nape Nnauye na Steven Wassira,ukweli viongozi na wanachama wote makini wa CCM akiwemo Rais John Pombe Magufuli wanajua CHADEMA inaiimarika na ni hatari kwa utawala wao. Hii ndiyo sababu ya Magufuli kutupilia mbali ilani ya uchaguzi ya CCM na kutekeleza ile ya UKAWA. Mambo anayoyafanya Magufuli hivi sasa ndiyo yaliyokuwa yakisisitizwa na CHADEMA siku zote lakini wakawa wanapingwa na kubezwa na CCM. Tusubiri, pamoja na Magufuli kufanya vizuri katika uongozi wake hakutaisaidia sana CCM kwani watu waliambiwa chagua Magufuli wala si chagua CCM, sana sana atajiongezea kura zake za urais lakini wataendelea kupoteza viti na kura kwenye ngazi nyingine.Alitabiri Wasira kabla yake na sasa amekufa yeye kisiasa