Ukweli utakuweka huru: CHADEMA mbioni kufa?

Mphamvu

JF-Expert Member
Jan 28, 2011
10,702
3,288
Na Padre Baptiste Mapunda, Mwananchi

Malalamiko mengi yamezuka hususani ugawaji wa viti maalumu ya ubunge na udiwani ndani ya chama kikuu cha upinzani nchini. Mitandoni maoni na malalamiko yamesheheni kiasi kwamba mtu unaweza kuanza kufikiria "Chadema mbioni kufa" Watu wanatoa hoja mbalimbali na zingine ni za msingi kabisa, ni vema sababu hizi zikachukuliwa kwa uzito wa hali ya juu, badala ya kuzipuuza na hivyo kuhatarisha uhai wa chama hiki kinachoonekana ni tumaini la Watanzania kwa mabadiliko ya nchi hii.

Siku moja asubuhi nilipigiwa simu kutoka Dar es Salaam na mwanachama mmoja aliyelalamikia suala la upendeleo wa kikanda katika ugawaji vyeo na viti maalumu vya ubunge na udiwani. Ukipita katika kona nyingi za nchi yetu hutakosa kusikia watu wakilijadili suala hili la upendeleo ndani ya Chadema hasa katika kipindi cha kuanza kipindi kipya cha uongozi katika nchi yetu.

Mimi najiuliza je, malalamiko hayo ni ya kweli au ya kutungwa. Ni muda mrefu sasa watu wengi wamekituhumu Chadema kuwa kina mbegu ya upendeleo kwa wanachama wake. Ni vema viongozi wakuu wa chama hicho na washauri wao wakalichukulia jambo hili kwa uzito mkuu.

Kinachoonekana ni kwamba kuna baadhi ya wanachama katika maeneo mbalimbali ya nchi wametumia muda wao, akili na hata mtaji wa pesa zao kukijenga chama, lakini linapokuja suala la uteuzi wa vyeo na viti maalumu wanajikuta wanaachwa. Je, suala hilo lipoje ndani ya chama hicho kikuuu cha upinzani nchini.

Watu wanahoji inakuwaje, mtu anakuwa kiongozi ndani ya chama na anajitahidi kufanya yale yanayompasa kufanya kwa bidii na akachukua fomu ya kugombea kiti maalumu, lakini fomu yake ikapotea ofisini? Hujuma kama hii inaweza kuelezwaje na watendaji wakuu? Kama ni kweli mambo hayo yapo hata ndani ya Chadema wakati tulizoea kuyasikia yakitendeka zaidi ndaniya chama kikongwe CCM, kumbe sasa huo ugonjwa unaonekana kusambaa hata ndani ya Chadema.

Inakuwaje, watu wanahoji viongozi karibu wote makao makuu, viti maalumu ni kutoka Kaskazini, hili linatoa taswira gani ya chama kinachojinasibu ni chama mbadala wa chama tawala (CCM). Ukweli ni kwamba kama Chadema inataka kueleweka kama ndiyo chama mbadala cha CCM katika nchi hii lazima kijaribu kuepuka mitego yote ya chama tawala, kama upendeleo wa kikabila, udini, ukanda , na u-familia, urafiki na upambe. Watanzania tulilelewa na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere kwa kutaka sote tuwe sawa, tuheshimiane, tujaliane, tusaidiane na tusibaguane katika jambo lolote lile. Na dini zetu zisiwe ndiyo chanzo cha kuvuruga amani yetu kwani nchi hii haina dini ila kila mtu ana dini yake kitu ambacho ni imani yake binafsi isiyoingiliwa na itikadi yoyote na hata Serikali haiingilii.

Watanzania wanafikiri kwamba katika sehemu ambazo Chadema bado haijaeleweka ilikuwa ni muda mwafaka kuteua wanachama wa sehemu hizo ambao wametumia nguvu na muda wao kukijenga chama hicho kushika nafasi mbalimbali. Watanzania wanasema hii ingekuwa ni njia mojawapo ya kukijenga chama badala ya kukibomoa kwa kufanya upendeleo kama unavyoelezewa na kulalamikiwa na baadhi ya wanachama na wananchi kwa ujumla. Ni wazi kwamba Chadema bado ina kazi kubwa ya kujisambaza katika kila kona ya nchi hii yenye ukubwa mwingi na mahitaji tofauti ya wananchi wake.

Wananchi na baadhi ya wanachama wanalalamikia suala la kuachwa vijana ambao ndiyo moyo au nguzo ya chama cha Chadema katika teuzi za hivi karibuni. Inafahamika wazi kwamba taifa lolote bila kujali vijana basi linakuwa limekufa kabisa. Vijana ndiyo taifa na leo na kesho ambao lazima watazamwe kwa jicho la pekee katika jamii yoyote ile. Vijana wasiwe wanatumika tu kuwavusha wanasiasa (vigogo) wakati wa uchaguzi kama huo uliopita, halafu baada ya hapo wanawekwa kando na kusubiria tena miaka mitano ijayo watakapohitajika. Ni vema Chadema ikaanza kuamka kutokana na makosa yanayofanyika ili kiweze kujirekebisha kama vile waswahili wasemavyo ?kosa siyo kufanya, bali kulirudia kosa.?

Chadema acheni kujifanya viziwi wa kutosikia malalamiko na vilio wanavyotoa wananchi na baadhi ya wanachama wenu kwani "lisemwalo lipo na kama halipo, linakuja." Chadema acheni kujifanya vipofu wa kutokuona ukweli wa yale yanayofanyika ndani ya chama chenu, chukueni hataua sasa.

Kwa upande wangu hali hii inatisha katika medani ya siasa zetu za demokrasia na utawala bora, na ndiyo maana naandika kwa kuthubutu kwamba "Chadema mbioni kufa" Najua makala haya hayatapendwa na baadhi yenu katika chama, lakini huwa nina amini kuwa ukweli utakuweka huru.Na wataalamu wanasema kwamba ?mtu anayekupenda ni yule anayekukosoa na kukuambia ukweli, badala ya yule mnafiki anayekuchekea na kukusifia mambo ya nje tu, au anayekupaka mafuta kwa mgongo wa chupa.?

Napenda kuwaasa Chadema kuchukulia kwa uzito wa pakee yale yanayosemwa katika kipindi hiki cha Uchaguzi Mkuu uliokwisha ili kuweza kujipanga vizuri zaidi. Ukweli ni kwamba pamoja na mikakati na mbinu lazima zipangwe, lakini Chadema lazima kisome alama za nyakati mapema zaidi. Kwa mfano sasa baada ya uchaguzi huu ambao unasemwa na baadhi ya wananchi umepora ushindi wa Ukawa lazima chama kijiulize ni kwa nini kilishindwa uchaguzi huo? Je, ni makosa gani chama kimefanya katika uchaguzi huo?

Na sasa ni wazi kwamba wananchi wengi wanaona wazi kwamba bila kuwa na Katiba Mpya ambayo ina tume huru ya uchaguzi , CCM itaendelea kutawala milele. Hiyo ni changamoto kubwa kwa Ukawa na wapenda mabadiliko wote nchini, sasa kazi ni moja tu kudai Katiba Mpya yenye tume huru ya uchaguzi na kanuni safi za uchaguzi.

Chanzo: Mwananchi

 
CDM mali ya familia ya mtei wanahofia akiingia kiongozi kutoka kwingine familia itapoteza ukuu wake ..wao na ukanda ukabila na wao.
 
Ningefurahi sana, kupata mgawanyo wa hawa wabunge wa viti maalumu. CDM wamesemwa sana kuhusu ukanda na ukabila katika mgawanyo huu, je ni wabunge wangapi wanatokea kanda ya kaskazini? Kilimanjaro? Arusha?
Tunataka kujiridhisha kuwa huu ukanda unaosemwa ni kweli au ni platform ya kukichafua chama...
 
Hili cdm wanapaswa kulifanya kazi kwani lina ukakasi sana. Sijajua wana viti vingapi vya uhakika kwa upande wa viti maalum na mgawanyo ulikuwaje ili tuone upendeleo umekuwaje maana suala hili kwa kiwango fulani lina propaganda na ukweli kwa upande fulani. Ni vyema kuona viti ni vingapi, mgawanyo ulikuwaje na vigezo ilikuwa ni vipi. Si vibaya kujua vigezo viliwekwa kabla ama baada ya uchaguzi. Ila kiukweli suala hili linapigiwa kelele ni vyema kulifanyia kazi kama kuna nia ya dhati. Vinginevyo asiyesikia la mkuu ....
 
Nyumbu watajaa sasa hivi hivi hapa, ngoja nisepe zangu!, maana siku hivi wamekuwa wakali kama mbwa kichaa alojeruhiwa, Magu anavyowakimbiza ndo kabisa wanatafuta wa kufa naye!
 
mtaichafua sana CHADEMA wabunge mizee wapo ccm wale ving'ang'anizi toka miaka ya 80 wamo tu.
 
Padri Mapunda anavuna alichopanda.alitukana sana ccm na viongozi wake.

Kinachonishangaza kwa Mpunda kwanini alalamikie leo wakati malalamiko ya upendeleo wa kikabila, udini, ukanda , na u-familia, urafiki na upambe CHADEMA ni ya miaka mingi?
 
Ushauri wa kipumbavu huu! Hivi kuna yeyote anayelalamia hili kwa kufanya uchunguzi?

Inamaana kama mtu anaonekana ni mpiganaji wa kweli aachwe kwa ajili ya kuogopa vijineno vya propaganda za kijinga kisa ni mtu wa kaskazini?

Kama mtu alishinda kura za maoni aachwe tu kisa tu ana vinasaba vya kaskazini? Huu wote ni kipumbavu wa mtu asiyejua namna siasa inavyoendeshwa!

Tujiulize kati ya wabunge wote wa Chadema kupitia viti maalum ni wangapi watatokea kanda ya kaskazini? Chama hakiwezi kufa kwa sababu tu wachumia tumbo wachache hawakusikilizwa!

Majungu hayajengi zaidi ya kuchochea chuki za kijinga ndani ya jamii.
 
Ushauri wa kipumbavu huu! Hivi kuna yeyote anayelalamia hili kwa kufanya uchunguzi? Inamaana kama mtu anaonekana ni mpiganaji wa kweli aachwe kwa ajili ya kuogopa vijineno vya propaganda za kijinga kisa ni mtu wa kaskazini? Kama mtu alishinda kura za maoni aachwe tu kisa tu ana vinasaba vya kaskazini? Huu wote ni kipumbavu wa mtu asiyejua namna siasa inavyoendeshwa! Tujiulize kati ya wabunge wote wa Chadema kupitia viti maalum ni wangapi watatokea kanda ya kaskazini? Chama hakiwezi kufa kwa sababu tu wachumia tumbo wachache hawakusikilizwa! Majungu hayajengi zaidi ya kuchochea chuki za kijinga ndani ya jamii.

Anatropia ni mpiganaji wa kweli? Namuona alivoipigania CCM kwa kugombea jimbo ambalo walishakubaliana kuwa ni la Mtatiro.

Kwa niaba ya Padre Mapunda, pumbavu mwenyewe!
 
Anatropia ni mpiganaji wa kweli? Namuona alivoipigania CCM kwa kugombea jimbo ambalo walishakubaliana kuwa ni la Mtatiro.

Kwa niaba ya Padre Mapunda, pumbavu mwenyewe!

Siwezi kuingia katika ubishi na wewe ambaye ni Gamba sijajua unaitetea Chadema kwa maslahi ya nani! Uwezo wako mdogo wa kufikiri unaona ni sawa?Suala la Anatropia tuliambiwa kwamba liko ofisini linashughulikiwa unataka nini tena? Istoshe Anatropia pamoja na Mimi kutomkubali sana lakini slishawekeza vya kutosha na chama chake ndio maana Pale Chadema wana madiwani 8 kati ya 13 jimbo la segerea! Ujinga wake ni pale tume iliporudisha jina lake na yeye kukaa kimya kuendeleza ujuha wake.Narudia tena kukuita Mpumbavu kwa akili yako ilivyo.
 
iringa mjini cdm 14 ccm 4, mbunge msigwa , viti maalumu mgonokulima na lucy tendega eti hawa nao wachaga, au wameru
 
Siwezi kuingia katika ubishi na wewe ambaye ni Gamba sijajua unaitetea Chadema kwa maslahi ya nani! Uwezo wako mdogo wa kufikiri unaona ni sawa?Suala la Anatropia tuliambiwa kwamba liko ofisini linashughulikiwa unataka nini tena? Istoshe Anatropia pamoja na Mimi kutomkubali sana lakini slishawekeza vya kutosha na chama chake ndio maana Pale Chadema wana madiwani 8 kati ya 13 jimbo la segerea! Ujinga wake ni pale tume iliporudisha jina lake na yeye kukaa kimya kuendeleza ujuha wake.Narudia tena kukuita Mpumbavu kwa akili yako ilivyo.

Sijawahi kuwa gamba kihivyo, ila ni Shabiki wa Chama cha Mapinduzi, Chama Dume. Amewekeza kwenye chama chake, amepata ubunge wa Ukaskazini wakati Mtatiro hayupo Bungeni.

Sijashabikia Chadema, ila nataka ujue kuwa ni chama cha magumashi. Tusi lako nimelipokea kwa mikono miwili...
 
Ushauri wa kipumbavu huu! Hivi kuna yeyote anayelalamia hili kwa kufanya uchunguzi? Inamaana kama mtu anaonekana ni mpiganaji wa kweli aachwe kwa ajili ya kuogopa vijineno vya propaganda za kijinga kisa ni mtu wa kaskazini? Kama mtu alishinda kura za maoni aachwe tu kisa tu ana vinasaba vya kaskazini? Huu wote ni kipumbavu wa mtu asiyejua namna siasa inavyoendeshwa! Tujiulize kati ya wabunge wote wa Chadema kupitia viti maalum ni wangapi watatokea kanda ya kaskazini? Chama hakiwezi kufa kwa sababu tu wachumia tumbo wachache hawakusikilizwa! Majungu hayajengi zaidi ya kuchochea chuki za kijinga ndani ya jamii.

Kwa namna ya uandishi wako, haiwezekani ukawa umesoma alichokiandika mtoa mada, halafu ukamlaumu kwa kiasi hicho. Linalohitajika ni kufanya uchunguzi na kutoa majibu na vigezo vilivyotumika. Tujifunze kuvumilia maoni ya watu wengine. Najua unao uwezo mkubwa wa kujibu hoja tofauti na ulivyofanya.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom