Ukweli Unaoumiza kutoka kwa Rais wa Zanzibar kwenda kwa Watanganyika

Sasa watu wanalalamika kitu gani waswahili wanasema mkuki kwa nguruwe....... mbona sisi jumuia ya EA tumekataa wao kuja kununua ardhi kwetu japo wenzetu wameturusu lakini sisi kununua kwao, Na Zanzibar ana haki ya kufanya maamuzi kwa maslahi ya kisiwa chao maana wakiacha hivyo unaweza siku ukakuta Zanzibar imejaa wachaga huko ikaitwa small Moshi. Sababu zilezile tulizokataa kwa wenzetu EA sisi leo zinatukera. Kazi iendelee tu
 
Tanganyika haipo, ilishakufa...Haki ya Watanganyika huwezi ipata....

Kuna Nchi ya Zanzibar inayoishi na Haki zake...

Halafu kuna Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo nayo haiwezi kutetea Haki ya Watanganyika kwa kuwa Tanganyika HAIPO.

Tulambe Asali tu....
Aiseee.......nimesoma hii post. Nimesikitika. Kumbe wabara tupo tupo tu?
 
Sasa watu wanalalamika kitu gani waswahili wanasema mkuki kwa nguruwe....... mbona sisi jumuia ya EA tumekataa wao kuja kununua ardhi kwetu japo wenzetu wameturusu lakini sisi kununua kwao, Na Zanzibar ana haki ya kufanya maamuzi kwa maslahi ya kisiwa chao maana wakiacha hivyo unaweza siku ukakuta Zanzibar imejaa wachaga huko ikaitwa small Moshi. Sababu zilezile tulizokataa kwa wenzetu EA sisi leo zinatukera. Kazi iendelee tu
Nani amekuambia Kenya/Ugada/Rwanda/Burundi kuna ardhi ya iliyo wazi. Sisi tulikataa hili la ardhi kwa sababu TZ ni nchi pekee kwenye EAC yenye ardhi wazi/isiyomilikiwa. Lbada sasa hivi ambapo Juba na Congo (DRC) ambao kuna ardhi wazi. Lakini kufikiria kupata ardhi kwa sasa huko Congo na Juba zitakuwa hazikutoshi.
 
Wakuu Huu ni Ukweli Unaoumiza uliosemwa na Rais Wa Zanzibar Dr. Mwinyi Kuhusu Watanganyika Kumiliki Ardhi.

Kinachoonekana Ni Kwamba, Ardhi ya Wazazibar ni Kwa Ajili ya Wazanzibar Tu.

Ila Ardhi Iliyoko Tanganyika Kwa maana ya Tanzania Bara ni Ardhi ya Watu Wote Kwa maana ya Wazanzibar wakija Bara kuomba ardhi hawapewi masharti kama Wanayopewa Watanganyika wakitaka Kumiliki Ardhi Zanzibar.

Tuishi Kwa Kufikiri Sana.

View attachment 2202002
Hiyo ni kero ya muungano. Inafaa ijadiliwe na kupatikana jawabu sahihi. Taifa moja haliwezi kuwa na ubaguzi kati ya raia wake.

Ngoja nikuulize swali, maana sijui jibu lake. Je nikitaka kwenda kuoa Zanzibar nitaruhusiwa? Mimi ni mTanzania toka Bara.
 
Mtoa Tamko ni Mzanzibar anaemiliki ardhi bara. Watanganyika sijui nani katuloga

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Lakini inashangaza kidogo. Kwani mtu kama huyo anayetoa tamko hilo haoni lilivyo bovu? Ni aibu kabisa kwa kiongozi mkuu kusimamam jukwaani na kutamka jambo unaloona wazi kuwa linatoa ubaguzi kati ya jamii inayotakiwa kuwa moja, bila kubaguana.
 
Tanganyika ina ardhi kwani? Nchi ilikufa kitambo, tulieni, Tanzania ni mali yetu sote
 
Hiyo ni kero ya muungano. Inafaa ijadiliwe na kupatikana jawabu sahihi. Taifa moja haliwezi kuwa na ubaguzi kati ya raia wake.

Ngoja nikuulize swali, maana sijui jibu lake. Je nikitaka kwenda kuoa Zanzibar nitaruhusiwa? Mimi ni mTanzania toka Bara.
Umesikia SMZ inazuia mbara kuoa ama kuolewa na Mzanzibari?
 
Namna pekee ya kuweka heshima ya muungano ni kuwapa vitambulisho maalumu ya ukazi. Na ardhi wasimilikishwe bali wakodishwe. Na wahesabiwe kabisa.
Wakileta fyoko fyoko tunawavusha bahari waende kwenye hako kakifusi wanaita nchi.

Wazaliane na wingi wao kule hakuwezi watosha nakwambia lazima wataomba poo na kuona umuhimu wa muungano nguruwe hawa.

Maana wanatuchezea sharubu kwasababu hatuwanyooshei maelezo tunaenda nao kistaarabu sana.
 
Wakuu Huu ni Ukweli Unaoumiza uliosemwa na Rais Wa Zanzibar Dr. Mwinyi Kuhusu Watanganyika Kumiliki Ardhi.

Kinachoonekana Ni Kwamba, Ardhi ya Wazazibar ni Kwa Ajili ya Wazanzibar Tu.

Ila Ardhi Iliyoko Tanganyika Kwa maana ya Tanzania Bara ni Ardhi ya Watu Wote Kwa maana ya Wazanzibar wakija Bara kuomba ardhi hawapewi masharti kama Wanayopewa Watanganyika wakitaka Kumiliki Ardhi Zanzibar.

Tuishi Kwa Kufikiri Sana.

View attachment 2202002
Kufuta ujinga ni pamoja na kutafuta vyanzo/chanzo cha mambo YALIYOZOELEKA.....

Hivi tunayafahamu vyema maneno/maandishi ya baba wa taifa hayati El Comandante JKN?!!!

Ni yeye baba wa taifa....

Ni yeye.....

Yeye ndiye aliyesema kuwa serikali ya Zanzibar itabaki na kuifuta ya Tanganyika kwa KUOGOPEA KUKIMEZA KISIWA KILE....

Zanzibar ni ndogo......unaanzaje kuruhusu KUTOA VIBALI VYA KUMILIKI ARDHI kwetu sisi mamilioni wa huku bara ?!!!!

Hebu tuzionee AIBU nafsi zetu.....

#Siempre JMT🙏
#Siempre El Comandante JKN ,Hasta la Victoria JKN🙏
 
Wazanzibari wanapenda sana Muungano wa changu changu, chako changu.
Vijamaa ni vinyonyaji mpaka basi.

Ukivikuta vimetuna 🙇 kwenye bunge letu la Tanganyika kule Dodoma, unaweza ukadhani kuna jambo la msingi vinafanya!

Kumbe vinahemea tu kodi za Watanganyika.
Husuda zitakupa magonjwa wewe mzee 🤣🤣

Hivi lini wazanzibari waliulizwa kuhusu Muungano kabla ya 1964?!!!

Kwani wasingekuwa ndani ya huu Muungano wasingesimama kama taifa lililopata uhuru wake 1963?!!!

Tuache CHUKI kwa kuwaonea ndugu zetu hao....NDOA ilishapita na inakuaje watoto tunahoji uhalali wa ndoa ya wazee wetu ilihali WAMETUKUZA NA KUTUACHIA AMANI TELE ?!!!

Mawazo ya kibaguzi huwa siku zote hayana afya kwa UTULIVU mpana wa kijamii......

#Siempre JMT🙏
 
Namna pekee ya kuweka heshima ya muungano ni kuwapa vitambulisho maalumu ya ukazi. Na ardhi wasimilikishwe bali wakodishwe. Na wahesabiwe kabisa.
Wakileta fyoko fyoko tunawavusha bahari waende kwenye hako kakifusi wanaita nchi.

Wazaliane na wingi wao kule hakuwezi awatosha nakwambia lazima wataomba poo na kuona umuhimu wa muungano nguruwe hawa.

Maana wanatuchezea sharubu kwasababu hatuwanyooshei maelezo tunaenda nao kistaarabu sana.
Mkuu Samcezar kwa hekima zako wewe si wa kuwaita binadamu wenzako NGURUWE....

Chanzo cha haya ya kuhitalafiana ni baba wa taifa.....muasisi wa Muungano.....

Yeye ndiye aliyetuambia kuwa huu ni muungano wa kipekee kabisa na akaogopea Zanzibar KUMEZWA na Tanganyika......

Ni yeye aliyeogopea Zanzibar kupoteza historia ya uhuru wake wa 1963.......

Sasa iwe alikuwa sahihi ama laa ,la muhimu ni kuwa taifa moja limeshaundwa na tukianza kuyatafuta mapungufu kamwe HATUTOYAKOSA kwetu na kuasisiwa kwa mataifa yote ulimwenguni......

La kushika ni kuwa tuna AMANI(ibezwe vyovyote vile)......

Tukianza kuishambulia Zanzibar basi tutaanza kushambuliana hata sisi wabara kwani yako maeneo ambayo hayakutaka kupambania uhuru 💯 p kwa kuogopea kupoteza walichonacho......

Yapo maeneo yenye utajiri mkubwa ambao unatumika na maeneo mengine.m....

Yapo maeneo yaliyocheleweshewa maendeleo ilihali tu nchi iwe salama kipindi cha kupigania uhuru wa jirani zetu......

Je nao waamke na wasimame dhidi ya maslahi mapana ya taifa letu ?!!!!!

#Siempre JMT🙏
 
Je unataka na wazanzibari waseme kuwa mh.Dr Mwinyi ni mbara aliyeshinda urais wa Zanzibar ?!!!😳😳🤣🤣

Tumeshakuwa taifa moja...CHOKOCHOCHO ni husuda tu......

#Siempre JMT🙏
 
Back
Top Bottom