Ukweli: Tozo za Tanesco ni kodi ya mita, si kodi ya Majengo

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,657
218,145
Hii ndio taarifa inayofichwa na Mamlaka na ambayo inawachanganya wananchi, na wala ule uongo wa Viongozi kwamba Nyumba za Tope au za nyasi hazitatozwa hiyo kodi, sasa umedhihirika rasmi kwamba ulikuwa uongo baada ukweli kubaini kwamba kila nyumba inatozwa kodi ya jengo kupitia mita hizo bila kujali hali ya nyumba yenyewe.

Lengo la uzi huu si kulalamika, bali kuikumbusha Serikali ya Tanzania Umuhimu wa KUSEMA UKWELI KWA RAIA wake badala ya kutegemea ulaghai mara zote, Haiwezekani nyumba yenye mita 6 tena nyingine zimesajiliwa kwa majina tofauti na la Mwenye nyumba zote hizo zikakatwa tozo ya jengo hilo hilo, kimsingi kodi hii ni kodi ya Mita, SI KODI YA MAJENGO KAMA TULIVYODANGANYWA AWALI.

Malalamiko ya wananchi wa vijijini huko Wilayani Kyela ni Makubwa sana baada ya sasa kuanza kukatwa Tozo ya miezi minne , kwa madai kwamba hawakukatwa huko nyuma kutokana na makosa ya mtandao, HATIMAYE TANZANIA YAANZA KUWALIPISHA KODI YA MAJENGO WENYE NYUMBA ZA TOPE KWA VILE TU WALIKUBALI UMEME WA REA.

Nakulilia Tanzania
 
Wenyewe wangefanya tifauti nyumba za jinijini..manispaa...miji mikuu ya mikoa..labda wananchi wangelipi 3000 kwa mwez..harafu wilayani na centres kubwakubwa kama katoro..wangelipa2000 harfu vijini 300
 
wenyeww wangefanya tifauti..nyumba za jinijini..manispaa...miji mikuu ya mikoa..labda wananchi wangelipi 3000 kwa mwez..harafu wilayani na centres kubwakubwa kama katoro..wangelipa2000 harfu vijini 300
Waporaji hawawezi kufikiria hilo
 
Subiri mabawacha na mabavicha wenzio waje wakuzodoe kwamba wewe unampinga mama utakuwa sukuma gang
 
Mbaya zaidi haijulikani inakoenda hiyo tozo.

Mwenye taarifa juu ya ujenzi wa vituo vya afya katika tarafa tajwa naomba aweke mrejesho hapa kama kuna hata dalili za kusafisha eneo la ujenzi wa kituo cha afya huko toka tutangaziwe kuwa hela imepelekwa
 
Cha ajabu wanachukua tozo alafu huduma ya umeme ndo imekua ya hovyo kupita kiasi, kwa matendo yao ccm wana laana sio bure
 
Sita mbona chache sana tuu. Kuna sehemu frem za biashara zipo 16 na kila frem ina meter yake. So hapo zipo 16 na kila mmoja analipa kodi ya jengo.
Asante sana mkuu kwa ufafanuzi. Ile sentensi yake ni tata. Hilo neno mita alitakiwa alifafanue kuwa ni mita za luku.

Mimi nilidhani ni mita kipimo cha urefu.
 
Back
Top Bottom