Francis12
JF-Expert Member
- Sep 30, 2016
- 7,533
- 22,278
TANZANIA HAKUNA AMANI, KUNA UVUMILIVU.
Ni siku 18sasa, Afisa wa Usalama wa Taifa aliyemshikia Bastola aliyekuwa Waziri wa Habari, Sanaa na michezo Mhe. Nape M. Nnauye (Mb) akimzuia asiongee na vyombo vya habari, hajakamatwa wala kuchukuliwa hatua yoyote ile, pamoja na Waziri wa mambo ya ndani Mhe. Mwiguli Nchemba (Mb) kumuagiza IGP Mangu kumkamata na kumchukulia hatua Afisa huyo wa usalama.
Wakati matukio hayo yakiendelea kuiweka nchi kwenye taswira mbaya giza limeendelea kutanda, aliyekuwa mshauri wa mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA na mwanachama wa CHADEMA kamanda Ben-Rabiu Wa Saanane kutoweshwa kusikojulikana, kwasababu ya kuikosoa serikali na kuhoji uhalali wa shahada ya juu (PhD) ya Rais Magufuli. Kuhusu kupotea Kwa Ben Saanane, Bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania limeihoji serikali kupitia Mbunge wa Arusha Mjini Mhe. Godbless J. Lema (Mb) ambaye ni Waziri kivuli wa Mambo ya Ndani ya Nchi. Mhe. Lema amehoji, kwanini serikali itumie pesa nyingi kuwatafuta na kuwalinda wanyama kuliko kuwatafuta na kuwalinda wananchi? Alihoji pia, nchini Tanzania, wanyama wana thamani kubwa kuliko wananchi?? Alimtaka Waziri wa mambo ya ndani kuhakikisha Ben anapatikana, kinyume na hapo nchi itagawanyika vipande vipande.
Mbali na hayo, kumekuwa na taarifa za kuokotwa miili ya watu waliouawa na kutupwa pembezoni mwa mito na mabwawa, tena miili hiyo ikiwa imefungashwa kama vifurushi, na serikali haionekani kuchukua hatua, jambo ambalo linawaweka wananchi mashakani, na kupelekea kila mtanzania kuishi Kwa mashaka nchini, Kwa sababu ya serikali iliyopo madarakani.