Ukweli Tanzania hakuna amani, kuna uvumilivu

TANZANIA HAKUNA AMANI, KUNA UVUMILIVU.

Ni siku 18sasa, Afisa wa Usalama wa Taifa aliyemshikia Bastola aliyekuwa Waziri wa Habari, Sanaa na michezo Mhe. Nape M. Nnauye (Mb) akimzuia asiongee na vyombo vya habari, hajakamatwa wala kuchukuliwa hatua yoyote ile, pamoja na Waziri wa mambo ya ndani Mhe. Mwiguli Nchemba (Mb) kumuagiza IGP Mangu kumkamata na kumchukulia hatua Afisa huyo wa usalama.

Wakati matukio hayo yakiendelea kuiweka nchi kwenye taswira mbaya giza limeendelea kutanda, aliyekuwa mshauri wa mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA na mwanachama wa CHADEMA kamanda Ben-Rabiu Wa Saanane kutoweshwa kusikojulikana, kwasababu ya kuikosoa serikali na kuhoji uhalali wa shahada ya juu (PhD) ya Rais Magufuli. Kuhusu kupotea Kwa Ben Saanane, Bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania limeihoji serikali kupitia Mbunge wa Arusha Mjini Mhe. Godbless J. Lema (Mb) ambaye ni Waziri kivuli wa Mambo ya Ndani ya Nchi. Mhe. Lema amehoji, kwanini serikali itumie pesa nyingi kuwatafuta na kuwalinda wanyama kuliko kuwatafuta na kuwalinda wananchi? Alihoji pia, nchini Tanzania, wanyama wana thamani kubwa kuliko wananchi?? Alimtaka Waziri wa mambo ya ndani kuhakikisha Ben anapatikana, kinyume na hapo nchi itagawanyika vipande vipande.

Mbali na hayo, kumekuwa na taarifa za kuokotwa miili ya watu waliouawa na kutupwa pembezoni mwa mito na mabwawa, tena miili hiyo ikiwa imefungashwa kama vifurushi, na serikali haionekani kuchukua hatua, jambo ambalo linawaweka wananchi mashakani, na kupelekea kila mtanzania kuishi Kwa mashaka nchini, Kwa sababu ya serikali iliyopo madarakani.
Mkuu!
Wewe na yeyote ambae mnaamini nchi hii hakuna amani, nitawashauri, msiote amani ya kaburini, mkiwa hai duniani...amani inayozidi hii, iko kabutini kwa wafu!
...uzoefu wangu nikifanya kazi Beirut, na nikisafiri kikazi, kila wiki kwenda bandari ya Tripol(ya Lebanon, nt libya), miaka ya 1991/92 unanifanya niwashangae watanzania wenye mawazo ya aina yako...
...kuna amani...iko, tena bure! Usipigane, tii sheria!
 
bila shaka we ni mzee sasa, Mzee Tanzania kuna UTULIVU sio AMANI tokana na vigezo vya UNITED NATIONS (U.N) ukivyitumia vile huwezi sema kuna AMANI..Nitumie EMAIL yako nikutumie hivyo vigezo
 
Siku hizi bosi wako hakupi nafasi kuweka kipande cha habari kwenye magazeti na vipindi, na ndio maana unakuja kuandika humu!?

Bado unapenda kusoma wadau wa humu wakupe tips za kuandika huko!?

Muhimu acha kuchochea amacho hakipo nchini, wewe mwana upinzani.

Mtanyooka tu
Uchochezi ktk uzi huu ni upi? Inamaana haya aliyoandika si ya kweli? Labda kama ww si mmbongo! Yote haya yalilipotiwa mkuu!
 
Sasa bado mpo mnafanya nini katika nchi ambayo haina amani kwa nini msiende kuoba hifadhi katika nchi zenye amani kwani sheria za kimataifa zinaruhusu
Hapo chanzo ni utawala, utawala ungekua mzuri hata angepost Mara 20000 yasingetokea yaliyotokea.

Aman inaharibiwa na wakubwa, huku mitandaoni ni sehem pekee kwa wananchi wanyonge wasio na pakusemea ndipo wanaposemea

Kama walau mambo yapo vizur mtu huwezi pata sapport
Wewe binafsi bila ushabiki unaweza kuliambia jamvi utawala huu umekuathiri vipi? Maana wengi wanaolalamika ni watu waliokuwa wanatengeneza hela chafu.
TANZANIA HAKUNA AMANI, KUNA UVUMILIVU.

Ni siku 18sasa, Afisa wa Usalama wa Taifa aliyemshikia Bastola aliyekuwa Waziri wa Habari, Sanaa na michezo Mhe. Nape M. Nnauye (Mb) akimzuia asiongee na vyombo vya habari, hajakamatwa wala kuchukuliwa hatua yoyote ile, pamoja na Waziri wa mambo ya ndani Mhe. Mwiguli Nchemba (Mb) kumuagiza IGP Mangu kumkamata na kumchukulia hatua Afisa huyo wa usalama.

Wakati matukio hayo yakiendelea kuiweka nchi kwenye taswira mbaya giza limeendelea kutanda, aliyekuwa mshauri wa mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA na mwanachama wa CHADEMA kamanda Ben-Rabiu Wa Saanane kutoweshwa kusikojulikana, kwasababu ya kuikosoa serikali na kuhoji uhalali wa shahada ya juu (PhD) ya Rais Magufuli. Kuhusu kupotea Kwa Ben Saanane, Bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania limeihoji serikali kupitia Mbunge wa Arusha Mjini Mhe. Godbless J. Lema (Mb) ambaye ni Waziri kivuli wa Mambo ya Ndani ya Nchi. Mhe. Lema amehoji, kwanini serikali itumie pesa nyingi kuwatafuta na kuwalinda wanyama kuliko kuwatafuta na kuwalinda wananchi? Alihoji pia, nchini Tanzania, wanyama wana thamani kubwa kuliko wananchi?? Alimtaka Waziri wa mambo ya ndani kuhakikisha Ben anapatikana, kinyume na hapo nchi itagawanyika vipande vipande.

Mbali na hayo, kumekuwa na taarifa za kuokotwa miili ya watu waliouawa na kutupwa pembezoni mwa mito na mabwawa, tena miili hiyo ikiwa imefungashwa kama vifurushi, na serikali haionekani kuchukua hatua, jambo ambalo linawaweka wananchi mashakani, na kupelekea kila mtanzania kuishi Kwa mashaka nchini, Kwa sababu ya serikali iliyopo madarakani.

Kila siku mi ntazidi kuamini Tanzania hakuna amani Ila uoga na unafiki ndo vimetawala......Kwa mtiririko wa matukio haya ipo siku damu za waliopotezwa wote zitanena.

TANZANIA ni sawa na nyasi zilizokauka zinasubiri mtu azitie petrol na kuziwasha moto
Tuache unafk tz hakuna amani

Ova

Mazingira magumu Haya amani itoke wapi? MTU hana uhakika wa kurudu nyumbani salama,hana uhakika na kibarua hofu ya kutumbuliwa, matibabu bahati nasibu,afisa Tra au polisi akikukaribia presha juu, mikopo elimu ya juu majanga! Amani gani mnazungumzia; kutopigana kwa mitutu au?

Hii nchi ilipofikia watu watajilinda na hapo,hali itakua mabaya kuliko. ni km ccm mmoja alivyosema magufuli atajilinda na kuaminisha watu wa kanda ya ziwa kua anaonewa,nao wataamini na kumlinda ! Ss km magufuli atalindwa na watu wa kanda ya ziwa km bashite anavyomlinda,cc tuco na ulinzi, km wanawake wazee na watt,tumlilie Mungu wetu tu.manake polisi ndo hao wanavamia clauds na mkuu wa mkoa.bastola ndo hizo zinatembea njenje km kalamu,mwendesha pikipiki acpo c mama sheria ya policcm ni kumuua,ili aache mke na wanae,au wazazi wake wakihangaika na njaa,km yy ndo alikua mleta rizki,hiyo ccm haiwahusu.ukweli amani nchini imetoweka,na wala huo uvumilivu haupo kilichopo ni kukata tamaa na woga wa kutupwa ruvu tu,ndicho kilichopo nchini ss hivi.

HATUJIVUNII KUWA WATANZANIA TUNAVUMILIA KUWA WATANZANIA

kwa kweli sasa tuna-anza ishi kama SOMALIA, SUDAN, NIGERIA KUSINI (MAIDUGURI) n.k.. AMANI YETU IKO WAPI? USALAMA WETU UKO WAPI?. WATANZANIA TUNAISHI KWA UWOGA SASA

Uchochezi ktk uzi huu ni upi? Inamaana haya aliyoandika si ya kweli? Labda kama ww si mmbongo! Yote haya yalilipotiwa mkuu!
 
Sasa bado mpo mnafanya nini katika nchi ambayo haina amani kwa nini msiende kuoba hifadhi katika nchi zenye amani kwani sheria za kimataifa zinaruhusu
Wewe binafsi bila ushabiki unaweza kuliambia jamvi utawala huu umekuathiri vipi? Maana wengi wanaolalamika ni watu waliokuwa wanatengeneza hela chafu.
Kusolve tatizo siyo kulikimbia Bali kulikabili......Tuko hapa kupambana na mbegu chafu tena mbaya mliyoiotesha ili kizaz kijacho kiishi kwa amani kwani hata Mwl Nyerere angekimbia na kuwa mwoga kama wewe tusingekuwa hapa. Acha woga na unafiki bali andaa maisha mazuri ya kizazi chako kijacho.....*Our lives begin to end when we keep silence about things that matter*
 
Sasa bado mpo mnafanya nini katika nchi ambayo haina amani kwa nini msiende kuoba hifadhi katika nchi zenye amani kwani sheria za kimataifa zinaruhusu
Wewe binafsi bila ushabiki unaweza kuliambia jamvi utawala huu umekuathiri vipi? Maana wengi wanaolalamika ni watu waliokuwa wanatengeneza hela chafu.
Watu kama nyie,hali ikinukaa inabidi tuanze na watu kama nyie ....ikibidi majina kukesha getini au mlangoni kwako!

Ova
 
Tatizo letu wa TZ jambo baya likimtokea Mtanzania mwenzetu kama sio wa ule upande wetu, ndugu yetu wa karibu au ni taarifa tu ya magazetini, redioni au TVini basi its non of our business. Hayatuhusu.
 
Nchi ina amani japo watu kama wewe, mkijificha kwa ID feki, mnaandika mambo ya uchochezi (yasiyo na ushahidi bali hisia binafsi, zenye mlango wa kisiasa), kuichonganisha Serikali na Raia.

Mnyama anaweza kuwa na thamani kuliko binadamu pale binadamu anapokosa sifa za ubinadamu.

Wewe unaweza kuwa mmojawapo. Rejea mabandiko yako yote humu jamvini, ulioanzisha au kuchangia, yana sifa zote nilizozitaja, za kumfananisha binadamu na mnyama.
Tanzania haina aman ila ina wananchi wavumilivu na wanafiki na waoga tumia akili kutafakari sii nywele.
 
Wewe ni katika hao niliowagusia.

Ninaishi kwenye nchi ya amani na ndiyo maana wananchi tunaposoma maneno kama yako hayo, wengi tunayadharau na kuendelea na maisha yetu kama kawaida.

Viongozi wa kisiasa, upinzani, wanafanya kila jitihada kuichonganisha Serikali na wananchi, lakini siku kwa siku, wanaendelea na maisha yao.

Viongozi wa vyama vya upinzani na wafuasi wao wanafanya kila waliwezalo kuwadharirisha viongozi Serikalini, lakini maisha yanaendelea.

Wabunge wa upinzani wanajitahidi kuitukana Serikali na siyo kuikosoa, bado Bunge linaendelea na shughuli zake.

Kwa mifano hiyo, huenda kwako amani ikatafsiriwa kama hali ya uvumilivu, kwa kuwa moja ya misingi ya amani ni uvumilivu. Na mvumilivu kamwe hawezi kuwa na sifa ya woga au unafiki. Mvumilivu ni mtu mkweli, jasiri, hodari na anayejiamini kuliko.
 
Siku hizi bosi wako hakupi nafasi kuweka kipande cha habari kwenye magazeti na vipindi, na ndio maana unakuja kuandika humu!?

Bado unapenda kusoma wadau wa humu wakupe tips za kuandika huko!?

Muhimu acha kuchochea amacho hakipo nchini, wewe mwana upinzani.

Mtanyooka tu
Mkuu vp hela za lumumba ni tamuu eeh? Niazime japo tzs650000 nimalizie kulipa ada ya chuo maana boss wako hakunipa mkopo olas/heslb
 
Hii nchi ilipofikia watu watajilinda na hapo,hali itakua mabaya kuliko. ni km ccm mmoja alivyosema magufuli atajilinda na kuaminisha watu wa kanda ya ziwa kua anaonewa,nao wataamini na kumlinda ! Ss km magufuli atalindwa na watu wa kanda ya ziwa km bashite anavyomlinda,cc tuco na ulinzi, km wanawake wazee na watt,tumlilie Mungu wetu tu.manake polisi ndo hao wanavamia clauds na mkuu wa mkoa.bastola ndo hizo zinatembea njenje km kalamu,mwendesha pikipiki acpo c mama sheria ya policcm ni kumuua,ili aache mke na wanae,au wazazi wake wakihangaika na njaa,km yy ndo alikua mleta rizki,hiyo ccm haiwahusu.ukweli amani nchini imetoweka,na wala huo uvumilivu haupo kilichopo ni kukata tamaa na woga wa kutupwa ruvu tu,ndicho kilichopo nchini ss hivi.
Ipo siku hizi sumu moyoni zitakuja kutoka.
 
Wewe ni katika hao niliowagusia.

Ninaishi kwenye nchi ya amani na ndiyo maana wananchi tunaposoma maneno kama yako hayo, wengi tunayadharau na kuendelea na maisha yetu kama kawaida.

Viongozi wa kisiasa, upinzani, wanafanya kila jitihada kuichonganisha Serikali na wananchi, lakini siku kwa siku, wanaendelea na maisha yao.

Viongozi wa vyama vya upinzani na wafuasi wao wanafanya kila waliwezalo kuwadharirisha viongozi Serikalini, lakini maisha yanaendelea.

Wabunge wa upinzani wanajitahidi kuitukana Serikali na siyo kuikosoa, bado Bunge linaendelea na shughuli zake.

Kwa mifano hiyo, huenda kwako amani ikatafsiriwa kama hali ya uvumilivu, kwa kuwa moja ya misingi ya amani ni uvumilivu. Na mvumilivu kamwe hawezi kuwa na sifa ya woga au unafiki. Mvumilivu ni mtu mkweli, jasiri, hodari na anayejiamini kuliko.
Kwa akili ndogo hiyo uliyo nayo si rahisi kuweza kutofautisha aman na uvumilivu kwa mfano tu ndio maana hata wewe mke unaweza vumilia mateso ya mume wako sababu huna namna ya kumfanya au huna wa kukumsaidia au huna pa kusemea lakin ukimya wako na uvumilivu dhidi ya mateso hayo haimaanish una amani , hivi nyie watu manasoma shule za wapi nyie au ndio BRN maana mnaonekana vichwani mmejaza tope tupu , maana mna hoja ambazo hata mwanagu wa darasa la tatu hawezi kutoa. Unanipotezea mda wangu bure wapo watu wenye akili timamu na wenye hoja zenye mashiko nyie makapuku mnatupotezea wakati tu humu maana mnaushabiki wa kipumbavu na uongo uongo kuliko uhalisia , shit

Utafiti umeitaja tanzania kuwa nchi ya ngapi wananchi kuto kuwa na furaha!!?? au hupendi kufuatili taarifa zinao pingana na mawazo na fikra zako duni hizo? Hapo ndipo utaniambia hiyo ni amani au uvumilivu ndani ya mateso.
 
Siku hizi bosi wako hakupi nafasi kuweka kipande cha habari kwenye magazeti na vipindi, na ndio maana unakuja kuandika humu!?

Bado unapenda kusoma wadau wa humu wakupe tips za kuandika huko!?

Muhimu acha kuchochea amacho hakipo nchini, wewe mwana upinzani.

Mtanyooka tu
Wewe utakula kwa propaganda za kusema ukweli wa watawala
 
Wewe ni katika hao niliowagusia.

Ninaishi kwenye nchi ya amani na ndiyo maana wananchi tunaposoma maneno kama yako hayo, wengi tunayadharau na kuendelea na maisha yetu kama kawaida.

Viongozi wa kisiasa, upinzani, wanafanya kila jitihada kuichonganisha Serikali na wananchi, lakini siku kwa siku, wanaendelea na maisha yao.

Viongozi wa vyama vya upinzani na wafuasi wao wanafanya kila waliwezalo kuwadharirisha viongozi Serikalini, lakini maisha yanaendelea.

Wabunge wa upinzani wanajitahidi kuitukana Serikali na siyo kuikosoa, bado Bunge linaendelea na shughuli zake.

Kwa mifano hiyo, huenda kwako amani ikatafsiriwa kama hali ya uvumilivu, kwa kuwa moja ya misingi ya amani ni uvumilivu. Na mvumilivu kamwe hawezi kuwa na sifa ya woga au unafiki. Mvumilivu ni mtu mkweli, jasiri, hodari na anayejiamini kuliko.
Unavumilia huku unapata ulcers
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom