Kuna mambo mengi kuhusu Salum Msabaha.... Siku alipokwenda ITV ilikua kasheshe tupu.... nadhani alikwenda pia DTV, lakini hawakumuani kwamba ndiye Msabaha...... Kwa kifupi wa kuulizwa ni Ali Ameir Mohamed (Katibu wa Wabunge wa CCM wakati wa tukio alikua Waziri wa Mambo ya Ndani) na Abdalah Rashid aliyekua Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi.... Mengine zaidi baadaye.. lakini ni topic muhimu sana kuichambua.....
Ilianza kama utani,,, alipiga picha na Balozi wa Misri akiwa amevalia suti yake na akiwa amenyoa ndevu, ikatoka katika magazeti ya CCM ya UHURU,,, wakati huo ndio mkakati unaanza kuiva.
Akatangazwa kuandika barua ya kujizulu, lakini akawa haonekani, wakasema kafichwa, akaja akibukia katika magazeti ya Mtanzania wakati huo Salva RWeyemamu huyu wa Ikulu akiwa Mhariri Mtendaji na anaijua sana hiyo story.. Mtanzania likaandika kwamba Msabaha kaonekana Motel Agip chini ya ulinzi wa dola na CCM... kabla ya kutimua mbio na kukimbilia ubalozi wa Sweden ama Norway (Sikumbuki vyema), pale akaomba msaada, wale jamaa wakawaita CUF wakiwa katika gari maalumu wakamchukua na kumtembeza katika vyombo vya habari, katima TV alionekana mwoga zaidi wakati akitangaza kuhusu kutekwa wakati Alionekana kuwa kawaida kabisa wakati akitangaza kujiuzulu TVZ.... Inawezekana ubalozi walimuuza ama alikua tu mwoga baada ya kuwatoroka walinzi wa serikali pale Motel AGIP... kwa kweli hiyo ni kashfa kubwa kama ikiibuliwa tena baada ya kuwa mtu mwenyewe ni kiongozi na mtendaji wa juu wa CCM