CCM Zanzibar jipangeni, ni aibu kushinda katika namna mnayoshinda

AVRAM

JF-Expert Member
Feb 13, 2017
616
882
Sio kwa Zanzibar, kama ni makali ya Mheshimiwa Mwenyekiti wa CCM kuimarisha chama basi ni huko huko Tanganyika kwa Zanzibar CCM iko hoi si kwa mbinu zozote za kisiasa zitakazotumika ikaweza kushinda, mbinu pekee inayoweza kuipa ushindi CCM Zanzibar ni matumizi ya nguvu, na kutumikisha Askari wanaomilikiwa na Serikali ya SMZ kupitia Idara maalum za Serikali na wale wanaokuja kuokotwa matawini wanajulikana kama MAZOMBI, JANJAWEED na majina mengine mabaya mabaya).

Sio kweli kwamba Kitaifa Upinzani unaelekea kudhoofika, na si vyema wanachama na viongozi wa CCM kujiamini kuwa CCM inaimarika na kung'ara kama chama cha ukombozi kilicholeta uhuru katika nchi.

CCM inadhoofika kwa njia ileile iliyozidhoofisha vyama vya aina yake. Lazima CCM iende kwa kuwa muda umebadilika na kasi ya maendeleo kupitia CCM hairidhishi hivyo kila uchao vijana wanaozaliwa na kukuwa huja na hoja pamoja na maarifa mengine sio yale ya akina kingunge, Warioba na akina Salim Ahmed Salim pamoja na Salmin Amour, kwa wakati wao walifikiri ndivo, sahihi sana, lakin sio sasa hivi, CCM mubadilike msiwafananishe wananchi wa miaka ya 1960 na 1980 mkawachukulia sawa na wananchi wa TZ wa miaka hii ya 2000, badilisheni ajenda zenu hasa kule Zanzibar ambako kila muhula wa uchaguzi ukifika mnashindwa vibaya sana mnabakia kubirua namba na kughilibu wananchi kisa hawakupenda kuwachagua CCM, mapenzi ya Wazanzibari hayako kwenu msilazimishe kushinda. Mnatia aibu kuonekana kukosa mbinu mbadala ya kujihakikishia ushindi licha ya kuwa chama Dola.

Chama kikuu cha upizani Zanzibar CUF kinafanikiwa kuishawishi jamii ya wazanzibari walio wengi hususan wasionufaika na mifumo ya uongozi iliyopo sasa. Hii yote ni kwasababu chama hiki kinabeba ajenda ya asili ya wazanzibari katika kujitawala na kujiamulia mambo yao katika nyanja zote za maisha iwe kiuchumi, kijamii na kisiasa, ajenda ambayo huchagizwa na unyanyasaji wa kila namna unaofanywa na Serikali ya Tanganyika iliojificha katika koti la muungano.

Asilani abadani sio viongozi wa CCM ama wa SMZ wanaoweza kuwapigania Wazanzibari kupata haki yao ndani ya inayoitwa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano, si CCM katu, kila muhula wa Uchaguzi unapofika utashughudia namna CCM Tanganyika inavyokuja kuwapangia na kuwachagulia kiongozi mamluki ambae anaonekana hatakuwa na chagizo na mashaka katika kuimarisha mazila na mabaya yanayotendwa na Tanganyika dhidi ya Zanzibar, na bahati mbaya sana kutokana na muingiliano wa watu wanaojiona kiasili ni Watanganyika ambao mara zote ndio wanaopewa kipaombele katika kushika madaraka ndani ya chama na Serikali kwa kuonekana wao ndio walinda Mapinduzi na wale wenzao ambao huwaonekana kuwa na asili hiyo huwa hawapati ile imani na kuaminiwa sana hadi kufika kupata hadhi na daraja hizo, inakuwa rahisi kughilibiwa na kujikuta hawawezi kutetea hoja na matakwa yao wawapo Dodoma katika mkutano mkuu wa chama, hivyo chaguo na mapendekezo yao huwa hayazingatiwi sana na kujikuta wametwanga maji au kwa msemo wa kiswahili wamechinjiwa baharini, maana hata damu yao huwa haiyachi alama kutoa ishara kwa wengine kuwa wameonewa.

CCM Zanzibar badilikeni, si busara hata kidogo kwa miaka hii ya 2000s na kwa aina ya vijana waliopo sasa, kukusanya rika la vijana katika makundi tofauti mkaanza kuwapa ama kuwalisha propaganda zisizo macho wala miguu, ati bibi, mama na dada zenu walifagilishwa barabara/njia kwa maziwa ya vifua vyao, na kuendelea kuwajenga uzalendo kwa kuwataka walinde nchi kwa kuwa warabu watakuja kuinyakuwa na kurudisha utawala wa kisultani uliokuwapo kabla ya mapinduzi.

Si vyema kuendelea kutumia vitisho na propaganda za kiimla kulazimisha Wazanzibari kuichagua CCM, na si vizuri kubakia na mawazo yaleyale ya kuvunja na kuwatenga ama kuwanyanyapaa wengine, ama wale wote wanaonekana kukataa manyanyaso yanayofanywa na Tanganyika kuonekana ni wapizani na hawafawi kuwepo ndani ya CCM, jaribuni kuwa na utamaduni wa kuambiana ukweli na kustahamiliana na kusikilizana pale mmoja wenu anapothubutu kusema ukweli unaokukereni kwa nia ya kujenga chama au nchi na sio kumgeuka na kumuita mpizani na msaliti.

Kila uchaguzi unapokwisha na kugundua kuwa mlishinda kijanja janja, kilazima lazima na mlitia huruma kwa namna mnayoshinda, huwa mnaanza kuotezeana vidole na kuchaguana walio ndio na wengine huwa sio, huwa mnajaribu kuwataja wale wanaoonekana wamekisaliti chama badala ya kukaa na kujipanga vyema kwa ajili ya uchaguzi ujao, jambo ambalo mnatofautiana na wenzenu CUF, mara tuu baada ya Uchaguzi kuisha na kugundua kuwa wameshindwa kimazabe mazabe hurudi ndani na kukipanga chama katika swafu imara kabisa kuanzia ndani ya familia hadi katika ngazi ya taifa na kila mmoja hutekeleza jukumu lake hadi kufika watu wengine kama mm kushangaa hawa viongozi na vijana wa CUF wanavyojaribu kutekeleza miongozo na mikakati yao kama vile wanapigania imani ya dini zao, kiukweli vijana na wanachama wa CUF Zanzibar wametangamana sana sanaaaaa katika utekelezaji wa mikakati yao hadi kufika kuwashangaa, kama vile wanalipwa mishahara minono minono kumbe vile ni uzalendo na kuwa na imani na chama chao, siwasifu wao kwa kuwazoofisha Vijana na wanachama wa CCM ila natolea mfano huu ili CCM ijifunze namna ya kujenga hoja zenye umakini na uyakini pale wanapoamua kwenda mbele ya vijana wao kuwaelekeza mikakati ya chama chao badala ya kuwaambia pumba ambapo mara nyingi hutorokwa na wale vijana wenye uyakini na upambanuzi wa mambo ama mazingira wanayoishi nayo.

CCM Zanzibar njoni na sera na mikakati inayotekelezeka na sio kuimarisha majimbo na maskani za vijana kwa kuwapelekea TV na ving'amuzi, ati jezi na mipira kwa ajili ya kukuza vipaji vya soka, wawakilishi na wabunge kuweni waungwana kiasi, hivi kweli kwa akili zenu miradi mnayoianzisha kuimarisha kaya masikini mnazani italeta maendeleo katika nyumba ama hizo mnazoziita kaya masikini. Miradi ya uzoaji taka, upandaji miti, utunzaji bustani za mbogamboga na mengine kama hii, hivi kweli ingelikuwa inawahusisha wake, watoto na jamaa zenu mngeliwaruhusu kushiriki katika miradi hii kwa nia na tamaa kwamba inaweza kuwainua kiuchumi na hali zao kimaisha kwa ujumla, Waheshimiwa ifike wakati muone haya na kuwaonea huruma wananchi wenu.

Serikali imefanya ilichofanya mpaka imefika sasa kujishtukizia kuwa katika jamii kuna kaya masikini kama mnavyoziita, SMZ imeshindwa kujiuliza kisa na mkasa kama sio sababu ya uwepo wa hizi kaya masikini/fukara katika jamii, ukichunguza kwa umakini utagundua wengi ya wanaoishiriki katika miradi hii ni wale wanawake ambao hali zao kiuchumi katika familia zao zinasikitisha na hii ni kutokana na uchumi wa Zanzibar kukua katika nambari na sio katika hali za wananchi wenyewe.

Kila uchau SMZ inajisifu kuwa uchumi umekuwa lakin haitaki kuurudisha ukuaji huu katika maisha ya watu huku mitaani wanakoishi bali inaubakisha katika vitabu na midomoni mwa viongozi tuu, haitaki kuamini kuwa hali ya maisha ni ngumu mitaani na wananchi wanashindwa kujipatia mahitaji yao binafsi katika umuruwa wa kawaida hali ambayo inapelekea ukuaji wa kasi wa uwepo wa kaya fukara badala ya kusema masikini na ndio maana miradi ya kaya masikini imechukua wananchi wengi kuonesha hali si shwari huku mitaani, na hii yote ni baada ya matendo ya SMZ yenyewe. Sitaki kusema kuwa Serikali imesababisha umasikini huu na hatimae kuja kwa mlango wa nyuma kuwaonesha wananchi wake kuwa inawajali na kuwapenda sana kwa kuwaletea miradi hii. (umasikini huu ni zao la matendo ya serikali kwa wananchi wake).

Si busara kuwaaminisha wananchi kuwa hali mbaya walionayo itaondoka kupitia utekelezaji wa miradi hiyo, isipokuwa serikali inahitajika kujenga uchumi imara utakao tengeneza ustawi wa jamii mzuri kwa watu wa tabaka zote, na hii sio gumu kwa kuwa Zanzibar ni kisiwa cha biashara, kitu cha msingi cha kufanya ni kutekeleza kwa vitendo sera ya bandari huru, ambayo iliwahi kuinekana inaleta tija na manufaa kwa jamii kwa ujumla.

Serikali inapaswa kupunguza kodi kwa bidhaa ambazo zinaonekana kuhitajika kila siku mfano bidhaa za vyakula na nyenginevyo mfano wa hizo na badala yake kupandisha kodi kwa bidhaa za starehe na anasa (pombe, sigara, magari ya hadhi na nyenginezo kama hizo) kwa makusudi mazima ya kupunguza zigo la kodi na kufumka kwa bei za bidhaa ambao serikali yenyewe haiwezi kuudhibiti na wala Benki kuu ya Tanzania BOT hawashughulishwi nao sana.

Msife moyo wananchi, lakini sio kwa kasi hii, mengi yanafanyika pengine hatujui undani wake lakini tunayaona, maskuli ya sekondari kila wilaya binafsi nimeshughudia tunakwenda mdogo mdogo; ila kasi haifurahishi, barabara zinajengwa ila si kwa kasi hii wananchi tutaridhika, tunahamu na shauku kubwa kuona na kushughudia Zanzibar inatajwa ulimwenguni kwa sifa zake zilezile za zamani, sifa nzuri nzuri katika kila nyanja, si michezo, afya, elimu, uchumi na nyenginezo, tunasogea ila kidogo kidogo mmnnnnoooo, kujipa tamaa imo na kupongezana kunafaa.

CCM Zanzibar kuachia nchi hamtaki basi badilikeni, na sisi hayo maendeleo tunayoyaona Singapore, Taiwan, Mauritius na kwengineko tunayataka. Lakin katu hatuwezi kuyapata kwa misimamo na tabia za namna mlizonazo ndani ya chama.

Ahsanteni,

ILA NISEME KWELI INAUMAA KUONA TUPO TULIVYO.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa Zanzibar hawana chochote labda waokote wabara wawapeleke kule angalau wapate kura za kufutia machozi Bila ya hivyo watausikia ushindi WA halali.

Wazanzibar hawadanganyiki Kwa hela yako ukiwapa watakula na mwisho watakueka dole lá numa.

Wanayajua yote hayo. Si Zanzibar wala bara ccm inapoweza kushinda Kwa uchaguzi huru na haki.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tuambieni kwanza Sefu anaapishwa lini,mwaka wa nne huu unakatika,tumeshona sare zinapauka sasa
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom