Ukweli ni upi kuhusu sakata la Salum Msabaha?

Mtu wa Pwani

JF-Expert Member
Dec 26, 2006
4,191
674
Miaka mingi imepita lkn bado kuna tukio moja lilitokea kule Zanzibar miaka ya tisiini linaniacha nikiwaza na kutafuta jawabu bila ya kupata.

Mheshimiwa Salim Msabaha alikuwa mwakilishi wa jimbo la Mkunazini kwa tiketi ya CUF hakutimiza hata miaka miwili tukasikia kuwa mheshimiwa katekwa na CCM kwa ushirika wa serikali ya muungano na spika wa baraza la wawakilishi.

Na amelazimishwa ajiuzulu kama tulivyoonyeshwa kwenye tvz(alionyeshwa akijieleza kujiuzulu wadhifa wake).

Mheshimiwa huyo hatukumuona tena hadi tukamuona kwenye itv na viongozi waandamizi wa CUF wakati ule katibu mkuu ni Shaaban Khamis Mloo na wenziwe na Salim akaeleza kuwa alitekwa na kupelekwa bara kufichwa.

Baadae niliondoka Zanzibar na baada ya muda nnasikia huyu bwana yuko CCM.

Ukweli ni upi? Alitekwa kweli au nn kilimkuta?

Maana CUF baada ya kumpata walikuwa wakimwita shujaa, na ukipita Mkunazini utakuta kila sehemu kumechworwa kuwa Salim shujaa.

Ninaomba mwenye kujua ukweli nnaomba atuhabarishe ili tuweze kuweka sawa historia yetu
 
mtu wa pwani, huyu mtu naona kazama kizamo kibaya kwani hata hupati habari zozote ,niliwahi kusikia habari zisizo na ushahidi kwamba anadarisisha hapo tanzania bara(source; porojo za mitaani.com).labda kafuata mikoba ya omar awesu dadi. who knows?. ukweli na uhalisi wake bado ni giza.
 
hili suala mie linanighumisha sana

maana baaada ya kutokeza kwenye ITV alifanyiwa mkutano wa hadhara na kueleza kuwa kweli ametekwa na kudai CCM walimtesa sana mpaka kufikia kukubali kujiuzulu na kuwaingiza watu chungumzima walioshiriki ktk kumteka akiwemo mkuu wa mkoa wa mjini magharib wakati ule Mh Abdallah Rashid na Spika wa baraza la wakilishi na vyombo vya usalama wa taifa.

Uchaguzi mdogo ukafanyika kule jimboni kwake na Mh Juma Duni Akachaguliwa kuwa muwakilishi.

sasa nikaondoka na sikubahatika kuzifuatilia siasa za nyumbani kwa karibu ila kila leo nnasikia salim msabah na CCM, mara mkuu wa organization ya propaganda mara hivi mara vile.

ukwelio ni up na kwa nn CCM wam empa madaraka hayo makuu?

jee yale yote tuliosikia ilikuwa ni igizo tu ?
 
What is this all for, what are your intentions in asking this question.

Huyu ni mkuu wa kitengo kisichokuwa cha kikatiba ndani ya CCM yaani mkuu wa kitengo cha propaganda ........
 
Kuna mambo mengi kuhusu Salum Msabaha.... Siku alipokwenda ITV ilikua kasheshe tupu.... nadhani alikwenda pia DTV, lakini hawakumuani kwamba ndiye Msabaha...... Kwa kifupi wa kuulizwa ni Ali Ameir Mohamed (Katibu wa Wabunge wa CCM wakati wa tukio alikua Waziri wa Mambo ya Ndani) na Abdalah Rashid aliyekua Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi.... Mengine zaidi baadaye.. lakini ni topic muhimu sana kuichambua.....

Ilianza kama utani,,, alipiga picha na Balozi wa Misri akiwa amevalia suti yake na akiwa amenyoa ndevu, ikatoka katika magazeti ya CCM ya UHURU,,, wakati huo ndio mkakati unaanza kuiva.

Akatangazwa kuandika barua ya kujizulu, lakini akawa haonekani, wakasema kafichwa, akaja akibukia katika magazeti ya Mtanzania wakati huo Salva RWeyemamu huyu wa Ikulu akiwa Mhariri Mtendaji na anaijua sana hiyo story.. Mtanzania likaandika kwamba Msabaha kaonekana Motel Agip chini ya ulinzi wa dola na CCM... kabla ya kutimua mbio na kukimbilia ubalozi wa Sweden ama Norway (Sikumbuki vyema), pale akaomba msaada, wale jamaa wakawaita CUF wakiwa katika gari maalumu wakamchukua na kumtembeza katika vyombo vya habari, katima TV alionekana mwoga zaidi wakati akitangaza kuhusu kutekwa wakati Alionekana kuwa kawaida kabisa wakati akitangaza kujiuzulu TVZ.... Inawezekana ubalozi walimuuza ama alikua tu mwoga baada ya kuwatoroka walinzi wa serikali pale Motel AGIP... kwa kweli hiyo ni kashfa kubwa kama ikiibuliwa tena baada ya kuwa mtu mwenyewe ni kiongozi na mtendaji wa juu wa CCM
 
yeah wakati umefika kujua ukweli juu ya kilichotokea.

maaana kuna siri kuu hapa
 
Nafikiri hakuna haja ya kumzungumzia huyu Bwana Muda wake umekwisha..wamepita wengi na watakuja wengi tu baada yake..Bahati mbaya kabisa SIASA za Bongo zimejaa walevi...kama wewe si MLEVI watafanya HILA uwe MLEVI..utaonja mpaka utanogewa...
 
Sidhani kama ni sahihi kuacha kuzungumzia... Huyu bwana kesho utasikia anagombea Urais Zanzibar na kwa wanaomjua anasema yeye ana uwezo kuwa Rais wa Zanzibar
 
Ni kwa namna hii ndio historia inapofutwa kwa makusudi eti keshapitwa,jamii ijayo inayo haki ya kujifunza siasa zetu kwa kufahamu yapi yaliyotokea ,nani alihusika na hatima yake.

Tuko hai ,tulikuwepo hili likitokea lakini hatujui ukweli ni upi?!!!!!!!!!

Wenye facts tupeni ili tujue na kesho yuwarithishe jamii ijayo,mkichelea ndio yale malalamiko ya wapigania uhuru walio wengi kutopewa nafasi ya kihistoria isipokuwa Mwal.J.K na wateule wake.

Namkumbuka Kanyama Chiume kwa kitabu chake cha harakati za Uhuru wa Tanganyika,amesimulia mengi ya muhimu kwa urithi wa sisi ambao tumezaliwa miaka ya 70 mpaka sasa.Tuige mfano huo kwa kuandika na kutoa taarifa electronically kwa jamii.Muda unaruhusu
 
Waandishi wa habari wamuulize, aliahidi kutunga kitabu kuhusu kile kilichoitwa, "Sakata la Msabaha" huu ni wakati mwafaka wa kumtaka kuweka wazi kuhusu azma yake hiyo, au ndio amezibwa mdomo kwa kusogezwa karibu na "chungu"?
 
Haya hayajapita na kama wanaojua watueleze pia wat happened!
Lakini tujue tu ya kuwa wakati ule CCM kwenye BARAZA LA WAWAKILISHI ilikuwa haina two third, na mimi naamini ilikuwa inatafutwa hiyo two third kwenye sinema ile. .
Cuf walikuwa na majimbo 21 Pemba na 3 Unguja
Ccm walikuwa na majimbo 26 yote Unguja na pemba 0
Wajumbe 10 viti vya wanawake. CCM 6 na Cuf 4
Wajumbe 10 kuteuliwa na Rais
Wakuu wa Mikoa 5 wanaingia kwa nafasi zao
MWanasheria mkuu wa Serikali
Wajumbe wote walikuwa ni 76. CCM 48 na wa Cuf 28.
Idadi ya 48 CCM ilikuwa haitoshi na kama itakumbukwa hata Dk Salmin alitaka kubadili katiba ili aendelee ikashindikana. Alihitajiwa mjumbe mmoja au wawili ili kuweka two third ya Ccm.
Radio mbao: Mkuu wa Mkoa na Wilaya wake waliahidi jimbo kuchukuliwa na Ccm, matokeo Cuf kidedea ( Juma Duni). Wote Salmin akawapiga na chini.
Kwa sasa Salum Msabah ni mjumbe Nec CCM, nafasi 20 Zenji.
Mtu wa pwani umtafute Eddie Riyami plz akupe data.
Usanii mtupu!
 
Huyu jaamaa nimemuulizia sana, wakati naondoka TZ ndio alikuwa ametangaza kurudi CCM, na Mkapa alimkaribisha kabisa katika chama cha mapinduzi.

Alikuwa shujaa sana kule visiwani, lakini nadhani hakuwa fiancial stable and CCM use it as loop hole.Alipo rudi CCM alisema " Maalim mandevu yake tutayakata". Yeye na lamwai mkapa aliwaita vijana wakorofi na kusema sasa wamerudi kundini.

I always want to know what happened to him. alikuwa na Elimu ya dini deep sana. Ameweza kuonekana katika midahalo ya kidini couple of times.
 
huyu bwana sidhani kama alikuwa na tatizo la financial, familia yake iko vizuri ana jamaa zake arabuni walikuwa wakiwawasaida sana.

na ndugu zake Issa na Mbarouk nnategeme mambo yao mazuri na hawako tanzania.

ni kweli alikuwa mtu aliebobea sana ktk mambo ya dini na alijijengea jina sana kwa waumini wa zanzibar.

side

nnakumbuka hata edi riyami alizungumza kuhusu sakata la msabah kwenye tv lkn kwa vile mwenyewe alisema katekwa ikawa inaonekana kama vile edi ni CCM kwa hiyo ndio anaspin tu.

kwa hakika ukweli wa igizo lile unahitajika kuwekwa kweupeni.

nnategemea mna mafunzo mengi ya siasa zetu hizi tunazoenda nazo.

FM Marshal, Jasusi, Halisi, Mswahili, Kichuguu, Mkjj, Mkandara, Lunyungu na wengine wengi hebu tushirikiane kuupata ukweli wa sakata hili.

na kipindi hiki ndio neno SAKATA liliporindima zanzibar na nyimbo kutungwa sakata lako
 
Radio mbao: Mkuu wa Mkoa na Wilaya wake waliahidi jimbo kuchukuliwa na Ccm, matokeo Cuf kidedea ( Juma Duni). Wote Salmin akawapiga na chini.
Kwa sasa Salum Msabah ni mjumbe Nec CCM, nafasi 20 Zenji.
Mtu wa pwani umtafute Eddie Riyami plz akupe data.
Usanii mtupu!

Hapo umekuna kipele

K
 
ndugu zangu ndio hili tumeshindwa kupata data zake

mawlimu wangu kichuguu, mzee wa kijiijini, FM marshal na wengine hivi hili ndio limeshindwa kulitafuta data zake?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom