Kabla ya kuamua kuoa/kuolewa ni lazima uwe tayari kubadili mfumo wa kimahusiano kati yako na wazazi wako kihisia,kiuchumi n.k. Tambua wazi kwamba ukiamua kuoa/kuolewa wa kwanza kumshirikisha hisia zako,mawazo yako,fikra zako,mipango yako, anapaswa kuwa mkeo/mumeo vinginevyo ujue kuwa haujawa tayari kuoa/kuolewa hivyo JIPANGE!.Haiwezakani ukaamua kuoa/kuolewa wakati huo huo unataka uhusiano wako na wazazi wako ubaki kwa kiwango kile kile,HAIWEZEKANI!!! ndio maana, hata maandiko yamebainisha wazi "mtu atamwacha baba na mama yake,naye ataambatana na mkewe/mumewe!" hii ni kutokana na ukweli kwamba kuamua kuoa/kuolewa ni kuamua kuingia katika wajibu wa kina wenye mapana na marefu yake unaohitaji deep concetration hususani katika utunzaji na usimamizi wa ndoa/familia ili kuhakikisha inastawi vema!