Tukitaka Taifa letu liwe mahali salama, cha kwanza ni lazima liwe na uongozi mzuri. Na kazi ya kuhakikisha Taifa linakuwa na uongozi mzuri, ni la sisi wananchi.
Wananchi hatustahili kuwa chawa wa watu au vyama, bali tuwe chawa wa kudumu wa ukweli, ingawa ni sahihi pia, kile ninachokiona mimi kuwa ni kweli kinaweza kisiwe ukweli, lakini ukweli hubakia ni ule ule wakati wote.
Viongozi wetu wanapofanya vizuri ni vizuri kuwapa moyo ili wafanye vizuri zaidi. Wanapofanya vibaya, ni muhimu kuwakosoa ili wabadilike, au kama hawawezi kubadilika, mamlaka zilizowaweka kwenye nafasi za uongozi ziwaondoe.
Kuna watu wanafikiria kuwa wanastahili kuwa viongozi wakati wote, na wengine wanaona kutokuwa viongozi ni adhabu. Hao ni tatizo kubwa. Ndio hao walio tayari kufanya chochote ili kuupata uongozi. Hawa ni maadui wa Taifa. Huwa ndio ambao kila siku, usiku na mchana wanafikiria kuweka hata sheria mbaya, wapo tayari kutumia vyombo vya dola vibaya, wapo tayari kufanya hata hadaa, na wakati mwingine wapo tayari kuteka, kutesa, na hata kuua ilimradi wabakie madarakani.
Kwa kuangalia mahali ambapo nchi ilikuwa kabla ya utawala wa Rais Samia, hakika yaliyofanyika katika muda mfupi wa uongozi wake, yanastahili pongezi KUBWA SANA:
1) Watu wengi waliofungwa kwa uonevu, hasa kutoka vyama vya upinzani, sahizi wapo huru. Ni furaha ilioje kwa wanafamilia wa watu hawa. KAMA BADO WALIOPO GEREZANI, TUNAOMBA WOTE WAACHIWE HURU.
2) Miili ya watu kupatikana kwenye viroba, watu kutekwa, kuteswa, kushambuliwa kwa risasi kama alivyofanyiwa Lisu, hakusikiki tena. TUNAOMBA KUWE NA SHERIA INAYOZUIA KABISA VYOMBO VYA USALAMA KUTEKA WATU. MTU KAMA ANA KOSA AKAMATWE LAKINI ASITEKWE.
3) Watu kutengenezewa kesi za uhujumu uchumi, na kuporwa pesa zao kwenye akaunti za benki, kumekoma. ILI KUZUIA MAMBO HAYA KUTOKEA TENA, ZILE SHERIA ZILIZOWEZESHA HAYO KUTENDEKA, ZIFUTWE.
5) Police kugeuka kuwa idara ya mapato barabarani, kumetoweka au kupungua. ILI KUWEKA MAZINGIRA MAZURI YA MATUMIZI YA BARABARA, VIBAO VYA 50KM/HR NA MATUTA KILA SEHEMU, KUANGALIWE UPYA, MAPENDEKEZO YATALETWA KWENYE JUKWAA LETU ILI WADAU WACHANGIE MAWAZO MAANA NI KERO KUBWA.
6) Kauli za uwongo za viongozi wa Serikali zimepungua. Zile kauli za uwongo kama zile za kusema eti makinikia yana dhahabu 90%, eti tunadai kodi ya zaidi ya trilioni 400 kutoka kampuni ya madini, tunajenga miradi yetu yote kwa pesa ya ndani; na ili wananchi waendelee kudanganywa mpaka tukajitoa mwenye UWAZI WA SERIKALI. WAKATI RAIS ANAJITAHIDI KUWEKA WAZI TAARIFA ZA KWELI, BADO KUNA VIONGOZI WANAOPENDA UWONGO, VIONGOZI WA NAMNA HIYO WAONDOLEWE. Ni haki wananchi kuambiwa ukweli wakati wote, hata kama ni ukweli unaoumiza.
7) Kwenye demokrasia, mwanga mkubwa umeanza kuonekana. Taarifa ya kikosi kazi aliyokabidhiwa Rais, na mara moja Rais kutoa kauli ya kuanza kuifanyia kazi, ni hatua kubwa sana. MAPENDEKEZO YALE YAKIFANYIWA KAZI NA KUTEKELEZWA KIKAMILIFU, HAKIKA RAIS SAMIA ATAWEKA ALAMA KATIKA TAIFA HILI, ISIYOFUTIKA. CHADEMA, bila ya kuangalia mchakato ulivyoanza, unganishe nguvu na wadau wengine ili Taifa lililobora. Kufanya hivyo kuna faida kubwa zaidi kuliko kuendelea kuwa nje. RAIS AEBDELEE KULINDA HAKI ZA KIDEMOKRASIA KWA KUHAKIKISHA TUNAKUWA NA KATIBA NA SHERIA ZINAZOHIFADHI HAKI HIZO. TUNASUBURIA SIKU AMBAPO KILA MWANAJF ATAPENDA KUWEKA JINA LAKE HALISI WAZI BILA YA HOFU YA KUTEKWA AU KUITWA KWEBYE KAMATI YA MAADILI YA BUNGE KAMA ALIVYOFANYIWA NDUGU YETU MAYALA, KWA VILE TU AMETOA MAONI YAKE.
8) Rais amekuwa akiufuta uchumi wa nadharia, uchumi usio na mizizi, na kujenga sustainable economy. Rais ni dhahiri anatengeneza mifumo ya uchumi imara, uchumi unaojiendesha, siyo ule uchumi wa hadaa. Japo, kwa haraka, tunaweza tusione matokeo yake kwa sababu inahitaji muda. Mambo yale ya kusema, eti korosho zote zitanunuliwa na jeshi, au kuanzia leo hakuna kuuza mahindi nje, yanaharibu na kuua sustainable economy, kwa sababu unaua mifumo ya uzalishaji, usafirishaji, utunzaji na uuzaji; shughuli ambazo zote kwa pamoja huchangia na kuhuisha uchumi. TUNAOMBA SERIKALI ISIISHIE TU KWENYE MAELEKEZO NA MAAGIZO, BALI IENDE PIA KWENYE KUTENGENEZA MABADILIKO YA SHERIA ILI KULINDA MIFUMO YA UCHUMI.
Kwa namna nchi ilivyokuwa imeharibika, mabadiliko yanayofanyika sasa hivi, hayawezi kutoa matunda tarajiwa kwa muda mfupi, lakini nina hakika mbeleni kila mmoja ataona faida ya kuwa na mifumo mizuri ya uongozi.
KWA YALE AMBAYO RAIS SAMIA NA WASAIDIZI WAMETENDA VEMA, JAPO NI WAJIBU WAO, TUNAWAPONGEZA,NA KUWATIA MOYO WATENDE VIZURI ZAIDI. NA KILA WALIPO NA DHAMIRA NJEMA, MWENYEZI MUNGU AKASHUSHE BARAKA ZAKE. Lakini viongozi wanafiki, wazidi kuumbuliwa na kuanikwa. Tunataka viongozi walio wakweli kwa kauli na vitendo.
Kwa vyovyote vile, tupo kwenye mazingira mazuri zaidi sana sasa kuliko ilivyokuwa katika utawala uliotangulia.
Kule Simiyu kuna kijana kafungwa miaka 7 jela kwa kumsema vibaya Rais. Hatujui alisema nini, lakini kwa vyovyote vile, hata kama sheria zetu zinaruhusu adhabu kama hiyo, busara ingetumika. Adhabu hiyo ni kali sana. Kama kuwafunga wapinzani kwa kumkosoa Rais haikuwa jambo jema, basi haitakuwa sahihi pia kumfanyia jambo hilo hilo mwingine yeyote. Kwa vyovyote vile, hukumu kama ile haiwezi kumfurahisha hata Rais Samia ambaye anataka kuijenga nchi yenye demokrasia, uhuru wa maoni na haki.