Ukweli ni Kwamba Rais Samia ameleta mwanga

Ukweli ni Kwamba Rais Samia ameleta mwanga

Bams

JF-Expert Member
Joined
Oct 19, 2010
Posts
19,768
Reaction score
49,949
Tukitaka Taifa letu liwe mahali salama, cha kwanza ni lazima liwe na uongozi mzuri. Na kazi ya kuhakikisha Taifa linakuwa na uongozi mzuri, ni la sisi wananchi.

Wananchi hatustahili kuwa chawa wa watu au vyama, bali tuwe chawa wa kudumu wa ukweli, ingawa ni sahihi pia, kile ninachokiona mimi kuwa ni kweli kinaweza kisiwe ukweli, lakini ukweli hubakia ni ule ule wakati wote.

Viongozi wetu wanapofanya vizuri ni vizuri kuwapa moyo ili wafanye vizuri zaidi. Wanapofanya vibaya, ni muhimu kuwakosoa ili wabadilike, au kama hawawezi kubadilika, mamlaka zilizowaweka kwenye nafasi za uongozi ziwaondoe.

Kuna watu wanafikiria kuwa wanastahili kuwa viongozi wakati wote, na wengine wanaona kutokuwa viongozi ni adhabu. Hao ni tatizo kubwa. Ndio hao walio tayari kufanya chochote ili kuupata uongozi. Hawa ni maadui wa Taifa. Huwa ndio ambao kila siku, usiku na mchana wanafikiria kuweka hata sheria mbaya, wapo tayari kutumia vyombo vya dola vibaya, wapo tayari kufanya hata hadaa, na wakati mwingine wapo tayari kuteka, kutesa, na hata kuua ilimradi wabakie madarakani.

Kwa kuangalia mahali ambapo nchi ilikuwa kabla ya utawala wa Rais Samia, hakika yaliyofanyika katika muda mfupi wa uongozi wake, yanastahili pongezi KUBWA SANA:

1) Watu wengi waliofungwa kwa uonevu, hasa kutoka vyama vya upinzani, sahizi wapo huru. Ni furaha ilioje kwa wanafamilia wa watu hawa. KAMA BADO WALIOPO GEREZANI, TUNAOMBA WOTE WAACHIWE HURU.

2) Miili ya watu kupatikana kwenye viroba, watu kutekwa, kuteswa, kushambuliwa kwa risasi kama alivyofanyiwa Lisu, hakusikiki tena. TUNAOMBA KUWE NA SHERIA INAYOZUIA KABISA VYOMBO VYA USALAMA KUTEKA WATU. MTU KAMA ANA KOSA AKAMATWE LAKINI ASITEKWE.

3) Watu kutengenezewa kesi za uhujumu uchumi, na kuporwa pesa zao kwenye akaunti za benki, kumekoma. ILI KUZUIA MAMBO HAYA KUTOKEA TENA, ZILE SHERIA ZILIZOWEZESHA HAYO KUTENDEKA, ZIFUTWE.

5) Police kugeuka kuwa idara ya mapato barabarani, kumetoweka au kupungua. ILI KUWEKA MAZINGIRA MAZURI YA MATUMIZI YA BARABARA, VIBAO VYA 50KM/HR NA MATUTA KILA SEHEMU, KUANGALIWE UPYA, MAPENDEKEZO YATALETWA KWENYE JUKWAA LETU ILI WADAU WACHANGIE MAWAZO MAANA NI KERO KUBWA.

6) Kauli za uwongo za viongozi wa Serikali zimepungua. Zile kauli za uwongo kama zile za kusema eti makinikia yana dhahabu 90%, eti tunadai kodi ya zaidi ya trilioni 400 kutoka kampuni ya madini, tunajenga miradi yetu yote kwa pesa ya ndani; na ili wananchi waendelee kudanganywa mpaka tukajitoa mwenye UWAZI WA SERIKALI. WAKATI RAIS ANAJITAHIDI KUWEKA WAZI TAARIFA ZA KWELI, BADO KUNA VIONGOZI WANAOPENDA UWONGO, VIONGOZI WA NAMNA HIYO WAONDOLEWE. Ni haki wananchi kuambiwa ukweli wakati wote, hata kama ni ukweli unaoumiza.

7) Kwenye demokrasia, mwanga mkubwa umeanza kuonekana. Taarifa ya kikosi kazi aliyokabidhiwa Rais, na mara moja Rais kutoa kauli ya kuanza kuifanyia kazi, ni hatua kubwa sana. MAPENDEKEZO YALE YAKIFANYIWA KAZI NA KUTEKELEZWA KIKAMILIFU, HAKIKA RAIS SAMIA ATAWEKA ALAMA KATIKA TAIFA HILI, ISIYOFUTIKA. CHADEMA, bila ya kuangalia mchakato ulivyoanza, unganishe nguvu na wadau wengine ili Taifa lililobora. Kufanya hivyo kuna faida kubwa zaidi kuliko kuendelea kuwa nje. RAIS AEBDELEE KULINDA HAKI ZA KIDEMOKRASIA KWA KUHAKIKISHA TUNAKUWA NA KATIBA NA SHERIA ZINAZOHIFADHI HAKI HIZO. TUNASUBURIA SIKU AMBAPO KILA MWANAJF ATAPENDA KUWEKA JINA LAKE HALISI WAZI BILA YA HOFU YA KUTEKWA AU KUITWA KWEBYE KAMATI YA MAADILI YA BUNGE KAMA ALIVYOFANYIWA NDUGU YETU MAYALA, KWA VILE TU AMETOA MAONI YAKE.

8) Rais amekuwa akiufuta uchumi wa nadharia, uchumi usio na mizizi, na kujenga sustainable economy. Rais ni dhahiri anatengeneza mifumo ya uchumi imara, uchumi unaojiendesha, siyo ule uchumi wa hadaa. Japo, kwa haraka, tunaweza tusione matokeo yake kwa sababu inahitaji muda. Mambo yale ya kusema, eti korosho zote zitanunuliwa na jeshi, au kuanzia leo hakuna kuuza mahindi nje, yanaharibu na kuua sustainable economy, kwa sababu unaua mifumo ya uzalishaji, usafirishaji, utunzaji na uuzaji; shughuli ambazo zote kwa pamoja huchangia na kuhuisha uchumi. TUNAOMBA SERIKALI ISIISHIE TU KWENYE MAELEKEZO NA MAAGIZO, BALI IENDE PIA KWENYE KUTENGENEZA MABADILIKO YA SHERIA ILI KULINDA MIFUMO YA UCHUMI.

Kwa namna nchi ilivyokuwa imeharibika, mabadiliko yanayofanyika sasa hivi, hayawezi kutoa matunda tarajiwa kwa muda mfupi, lakini nina hakika mbeleni kila mmoja ataona faida ya kuwa na mifumo mizuri ya uongozi.

KWA YALE AMBAYO RAIS SAMIA NA WASAIDIZI WAMETENDA VEMA, JAPO NI WAJIBU WAO, TUNAWAPONGEZA,NA KUWATIA MOYO WATENDE VIZURI ZAIDI. NA KILA WALIPO NA DHAMIRA NJEMA, MWENYEZI MUNGU AKASHUSHE BARAKA ZAKE. Lakini viongozi wanafiki, wazidi kuumbuliwa na kuanikwa. Tunataka viongozi walio wakweli kwa kauli na vitendo.

Kwa vyovyote vile, tupo kwenye mazingira mazuri zaidi sana sasa kuliko ilivyokuwa katika utawala uliotangulia.

Kule Simiyu kuna kijana kafungwa miaka 7 jela kwa kumsema vibaya Rais. Hatujui alisema nini, lakini kwa vyovyote vile, hata kama sheria zetu zinaruhusu adhabu kama hiyo, busara ingetumika. Adhabu hiyo ni kali sana. Kama kuwafunga wapinzani kwa kumkosoa Rais haikuwa jambo jema, basi haitakuwa sahihi pia kumfanyia jambo hilo hilo mwingine yeyote. Kwa vyovyote vile, hukumu kama ile haiwezi kumfurahisha hata Rais Samia ambaye anataka kuijenga nchi yenye demokrasia, uhuru wa maoni na haki.
 
Ukiachana na demokrasia na haki za watu, Magufuli alikuwa rais wa hatari sana kwenye uchumi wa nchi
Kwa sababu alikuwa hatabiriki kwenye maamuzi maamuzi muhimu na alikuwa hasikilizi mtu

Imagine lile suala la korosho kipindi kile anaagiza jeshi kukusanya na kubangua hata kwa mabomu

Imagine kipindi kile maduka ya kubadilishia fedha yanavamiwa ghafla na wanajeshi na kupora fedha zote

Imagine ule utopolo unaoitwa vitambulisho vya machinga, visivyokuwa na jina wala picha
 
Haya Mambo yataoneonekana kama ni muhimu endapo Serikali itaamua inaweka usawa katika high cost of living
Mambo ya kusifu ni ujinga mkubwa Sana na fikra mfu
Serikali unabidi kuikosoa na sio kuisifia huu Upumbavu unawasumbua Sana watanzania
Serikali makini inafata katiba ya nchi
Na sheria
Sasa huyu sa100 anafata katiba yetu kwa usahihi?
Tuache Upumbavu wa kuwasifu watu wanaoishi kwa Kodi zetu wanyonge
 
Mwanga umeanza kuonekana kutoka kwenye giza la kutisha.

Kuwatia Moyo Viongozi wetu waendelee kufanya right things sio kuwapinga pinga tu for the sake of kupinga haiko hivyo, kuwakosoa iwapo tunaona kuna makosa sio kukosoa tu bila tija.

Naona tunaelekea kuzuri, tuenedelee na mijadala yenye kujenga hili Taifa letu sote.
 
Huyu ndiye hafai kabisa. Kama yule aliua mmoja mmoja basi huyu anaua na kudhulumu maelfu. Watu wanakufa kwa njaa na hali ngumu ya maisha huduma mbovu za afya miundombinu haiendelezwi.Maelfu ya wajane huko vijijini wanadhulumiwa kila siku kwa tozo za KIPUMBAVU, Anamtumia mwanaye mgonjwa fedha anakatwa tozo kama mfanyabiashara!

Kwa mambo yanayoendelea hapa nchini kwa sasa, Ni wazi kwamba wananchi hawana tena imani chini ya uongozi wa awamu hii ya sita. Kila unapoenda ni lawama na hali ya kutoridhika na utendaji wa serikali.

1: Uchumi wa Tanzania Umeporomoka. Laiti kama uongozi ungekuwa thabiti hakika uchumi ungekuwa wa kati daraja la juu tofauti na hali ilivyo sasa ambapo Tanzania imeporomoka kutoka nafasi yake ya 8 kati ya nchi 10 zenye uchumi bora Africa mpaka nje ya top 10 na kuzidiwa na vinchi kama Ghana na Angola

2: Laiti kama uongozi ungekuwa imara nidhamu na uwajibikaji kazini ungekuwepo. Leo hii tunashuhudia wananchi wakihoji kuhusu hali ya umeme nchini pasipokuwa na majibu au majibu yenye uwalakini. Lakini pamoja na hayo bado viongozi wamebaki wakiwa maofisini pasipo kuwajibika kwa namna yoyote.

3: Kwa miaka kadhaa Tanzania imekuwa ikiifanya juhudi kubwa kujikwamua kiuchumi kwa kuanzisha miradi mikubwa na ya kimkakati. Licha ya kwamba tangu awamu ya sita iingie madarakani hakuna mradi wowote wa kimkakati ulioanzishwa bali pia hata ile miradi iliyokuwa ikiendelea imekuwa ikisuasua

4: Serikali ingekuwa makini hakika Umeme usingekuwa wa mgao.Tangu Rais S.S.H aingie madarakani hali ya upatikanaji wa umeme nchini imekuwa mbaya sana. Hali hii imepelekea kurejea kwa mgao wa umeme ambao watanzania wengi walishausahau tangu miaka kadhaa iliyopita.Hali inayopelekea kuwatesa wananchi hususan wale wanaotegemea umeme kujipatia vipato katika shughuli zao za kila siku.

5; Hali ya upatikanaji wa maji imekuwa ya kusuasua. Kwa miezi kadhaa hususan katika jiji la Dar es salaam pamekuwa na mgao wa maji. Hali iliyopelekea kukosekana kwa maji kwa muda mrefu katika maeneo mengi.Hali ambayo hakuwahi kushuhudiwa hapo awali.

6: Tozo zisizokuwa na tija na zilizoua uchumi wa wengi.Serikali ya awamu ya sita imedhulumu na kunyang'anya kwa nguvu fedha za wananchi kwa kigezo cha tozo katika miamala ya simu. Mama mjane anapomtumia mgonjwa wake hospitali kwa ajili ya matibabu anakatwa fedha ambayo kimsingi haikuwa ya biashara. Kwa mujibu wa report kutoka Vodacom hivi karibuni miamala ya simu imepungua kwa asilimia zaidi ya 30!. Hili si jambo la kupuuza hata kidogo kwa uchumi wa nchi.Ni sawa na kutoa fedha mfuko wa kushoto na kuhamishia Kulia.

7: Kupanda kwa bei ya Mbolea.Mara tu baada ya awamu ya sita kuingia madarakani bei ya mbolea ilipanda karibu mara mbili ya bei ya awali.Hii ni imepelekea uchumi wa watanzania wengi ambao ni masikini na wanategemea kilimo kudhoofika.

8; Kupanda kwa bei ya mafuta ya kupikia
9; Kupanda kwa bei ya mafuta ya petrol
10; Kupanda kwa bei ya bidhaa za ujenzi kama cement,Nondo n.k
11; Teuzi za viongozi wasiokuwa na weledi kwa kigezo cha favour/Undugu/Kujuana (Mf. Riziwani Kikwete,Nape Nauye n.k) Tanzania ina vijana wasomi na wenye upeo mpana wa kifikra. Lakini cha kushangaza teuzi zimekuwa hazina matumaini ta kuipeleka Tanzania kule tunapotarajia.

12: Ukosefu wa uzalendo na ubadhirifu miongoni mwa watumishi wa umma.Siku si nyingi tumeshuhudia kiongozi mkuu wa serikali akiwaasa watumishi wake wale kwa urefu wa kamba zao. Hii inaashiria kwamba hata kiongozi mkuu anashiriki katika ulaji huo. Hali hii ni hatari kwa rasilimali za nchi.

13; Wananchi hususan wa hali ya chini kukosa nafasi katika nchi yao. Siku si nyingi tumeshuhudia wafanyabiashara ndogondogo maarufu kama machinga wakinyanyaswa kwa kuhamishiwa katika maeneo yasiyokuwa tija kwao. Vuta nikuvute hii imepelekea hali ya unyonge na sintofahamu miongoni mwao na kupelekea kuongezeka kwa umasikini miongoni mwa watanzania

14; Mikopo isiyokuwa na tija kwa taifa. Tangu Tanzania ipate uhuru viongozi wake wote walisisitiza kufanya mambo yetu kwa fedha zetu wenyewe bila kutegemea wahisani. Tanzania imebarikiwa rasilimali za kila aina. Mito, Maziwa, Bahari, Madini kama Tanzanite, Mbuga za wanyama, Gesi n.k Inashangaza Sana kuona kiongozi badala ya kusisitiza au kubuni namna ya kuzitumia rasilimali hizi ziweze kuwa na tija kwa watanzania,Badala yake tumekuwa tukijivunia mikopo!

15 ; Kuongezeka kwa gharama za uunganishaji umeme kutoka 27,000 iliyokuwepo mpaka zaidi ya 300,000 ya hivi sasa. Hali hii imepunguza mno kasi ya usambaaji wa umeme

16 ; Muingiliano baina ya mihimili kwa kigezo cha uchama. Inasikitisha kuona kiongozi wa mhimili mmoja anakosa uwezo wa kuikosoa na kuurekebisha mhimili mwingine kwa kuhofia kibarua chake. Hili tumelishuhudia baada ya kuona spika wa bunge la JMT kujiuzulu baada ya kuhoji kuhusu mikopo na tozo.

17 ; Safari zisizokuwa na tija wala umuhimu kwa taifa. Tumeshuhudia safari nyingi mno za nje ya nchi, Safari hizi zimekuwa zikiigharimu nchi fedha nyingi. Safari za vikao visivyokuwa na tija kama mkutano wa kujadili athari za gesi ya ukaa sidhani kama ina tija hususan kwa nchi ambazo bado uchumi wake ni mdogo. Ni sawa na mzazi anayemiliki baiskeli kwenda kuhudhuria kikao cha adha wanayopitia wamiliki wa magari kwa tairi zao kukosa ubora.

18 ; Kukosekana uhuru na ukandamizaji wa demokrasia. Tunaweza kusema kwamba pia hata katika awamu zilizopita hili lilikuwepo, Lakini hili la sasa limekuja kwa namna tofauti. Wakati mwingine baba anaweza kumpa mtoto adhabu ya kulima shamba,Mtoto akalia na kulaumu sana. Lakini shamba hilohilo baadaye likaleta chakula mezani wote wakala na kufurahia. Ila tofauti iliyopo sasa. Hakuna chakula kinachokuja mezani!

19 ; Kushughulikia zaidi mambo yasiyokuwa na tija kwa wananchi kuliko yale yenye umuhimu na tija kwa watanzania. Imekuwa jambo la kawaida kwa awamu hii kujihusisha zaidi na makongamano,Semina elekezi, Birthday Party pamoja na hafla mbali mbali badala ya kujikita katika kufufua na kubuni miradi ya kimaendeleo itakayosaidia kuwapunguzia wananchi mzigo wa umasikini na kuinua uchumi. Hafla ya machifu na watemi si muhimu kama hafla ya utiaji saini mradi wa uchimbaji na usambazaji wa gesi ya Mtwara!

20 ; Kukosekana ajira. Ubunifu na uibuaji wa miradi mipya si tu umekuwa na tija kiuchumi Bali umekuwa ukiajiri vijana wengi. Kukosekana kwa ubunifu na sera mbovu za serikali zimesababisha kukoseka kwa ajira miongoni mwa vijana wengi

21 ; Kuongezeka matukio ya uhalifu.
Mara tu baada ya awamu ya sita kushika hatamu sote tumeshuhudia jinsi wimbi la uhalifu lilivyoongezeka.Sio tu matukio ya wizi na ujambazi bali mpaka uchomaji wa masoko kama Kariakoo, mchikichini n.k wizi mauaji na utekaji nyara vimeongezeka kwa kasi mno. Hii inaonyesha udhaifu katika usimamizi wa majeshi yetu ya ulinzi na usalama

22 ; Kuongezeka gharama za simu
Kutokana na kodi za miamala Kuongezeka kampuni za simu zimejikuta zikilazimika kupandisha gharama za muda wa maongezi na huduma zinginezo za simu kama vile huduma za vifurushi ili kuweza kubalance gharama za uendeshaji. Hali hii imesababisha mzigo mzito kwa wananchi hasa ukizingatia mawasiliano ni nyenzo muhimu sana katika shughuli zao za kila siku

23 ; Kutoa vipaumbele kwa mambo ya hovyo na yasiyo na tija kwa taifa hususan kwa wakati huu.Hapakuwa na ulazima kutumia gharama kubwa na uwekezaji katika kutumia kodi za wananchi kiongozi mkuu wa serikali kusafiri na kutumia muda mwingi kutengeneza filamu wakati fedha hiyo haina uhakika wa kurudi.Mfano fedha hiyo ingewekezwa kwenye timu maarufu zinazoshiriki ligi za ulaya ingekuwa na tija na matokeo zaidi na Rais angepata muda kutekeleza majukumu mengine ya kiserikali kuliko kupoteza muda mwingi kusafiri.

Hakika ni mambo mengi ambayo yamekuwa yakifanyika kinyume na matarajio ya watanzania wengi ambao waliwaamini viongozi wao na kuwaweka madarakani huku wakiwa na matumaini makubwa ya kuondokewa na maradhi, ujinga na umasikini ambao ndio maadui wakuu wa taifa kama ilivyobainishwa na Mwl Nyerere badala yake watanzania hao ambao wengi ni masikini na wameteseka kwa umasikini kiasi cha kusahau tarehe zao za kuzaliwa huku wakishuhudia wale waliowachagua wakikata keki ikulu!
 
Samia ameleta mwanga kwenye kitu gani?

Unapotumia mfano wa matukio yaliyopita, ambayo mengi hayakufanyika wakati wa uongozi wake ndipo unapofeli, huyu anatakiwa kuhukumiwa kwa matukio ya sasa chini ya uongozi wake, ambapo mengine ni mabaya ya mtangulizi wake lakini yeye bado anayaendeleza.

Mfano, yale mapendekezo aliyopokea jana kutoka kwa kikosi kazi, kwa kiongozi aliye serious, baadhi alitakiwa ayafanyie kazi pale pale na kuyatolea uamuzi, lakini ameshindwa, amesema mpaka akapitie sheria kwanza!.

Issue ndogo kama kuruhusu mikutano ya kisiasa, hakuhitaji kupitia sheria, kama aliona kuna haja ya kufanya hivyo, basi asingewaelekeza wajumbe wa kikosi kazi wakafanyie kazi hilo suala, huyu anaonesha hajiamini, anapotezea wapinzani muda makusudi.
 
Mwanga umeanza kuonekana kutoka kwenye giza la kutisha.

Kuwatia Moyo Viongozi wetu waendelee kufanya right things sio kuwapinga pinga tu for the sake of kupinga haiko hivyo kuwakosoa iwapo tunaona kuna makosa sio kukosoa tu bila tija.

Naona tunaelekea kuzuri, tuenedelee na mijadala yenye kujenga hili Taifa letu sote.
Naona mvaa kobaz unajitahidi kutetea imani yako
View attachment 2394385
 
Labda mwanga wa kuhamasisha ufisadi katika Taifa🐒🐒🐒
 
Mambo yale ya kusema, eti korosho zote zitanunuliwa na jeshi, au kuanzia leo hakuna kuuza mahindi nje, yanaharibu na kuua sustainable economy, kwa sababu unaua mifumo ya uzalishaji, usafirishaji, utunzaji na uuzaji; shughuli ambazo zote kwa pamoja huchangia na kuhuisha uchumi. TUNAOMBA SERIKALI ISIISHIE TU KWENYE MAELEKEZO NA MAAGIZO, BALI IENDE PIA KWENYE KUTENGENEZA MABADILIKO YA SHERIA ILI KULINDA MIFUMO YA UCHUMI.
Imagine unachukua acre 5000 unaweka miundombinu ya kulima mahindi then anatokea mtu anakuzuia usiuze kwa bei ya faida yako! Ule ni ulevi wa kiuchumi.
 
Rushwa zimekua nje nje sio kujificha tena, mcheke kg 3500, maharage kg3200, mafuta ya kupikia lita 7000, unga wa sembe kg 2000 mwanga gani unaongelea ndugu yetu??. Bado umeme na maji ni shidaaa. Ifike stage tujitambue kama taifa tuache uchawa usio na faida
 
Licha ya kwamba tangu awamu ya sita iingie madarakani hakuna mradi wowote wa kimkakati ulioanzishwa bali pia hata ile miradi iliyokuwa ikiendelea imekuwa ikisuasua
Hivi hapa huwa mnamaanisha au, if yes then mnamaanisha nini? Mradi wa Bwawa la Nyerere ulianza 2018 hadi 2021 ulifikia 30%+ lakini leo 2022(mwaka mmoja baadaye) umefikia 74%. Mradi wa SGR kadhalika, je huu mwendo wa konokono mnaupimaje? Mnampimaje Rais aliyekaa miaka 6 na huyu wa mwaka mmoja na nusu? JPM aliingia November 2015, mnaweza kutuwekea miradi aliyoanziasha na kukamilisha mwaka mmoja na nusu baadaye?
 
Big No.
Nikuulize swali. Kwenye Uchumi anajenga nini? So far,
Kipengele kimoja tu: Kwa nini ameanzisha Tozo kwenye miamala ya simu!
Tukiri kwamba kila awamu ina wanufaika wake, sikuwahi kumkubali Magufuli, ila huyu wa sasa ni Failure pakubwa.
Uchumi gani unakandamiza tabaka la chini tu.
 
Hivi kwa nini maamuzi yote ya msingi yafanyike Dodoma? Unawizara kubwa ya Tamisemi kila wakati waziri anabadilishwa, naamini si kwamba hawajitahidi bali like nchi hili ni likubwa sana na maamuzi ya kikanda yanahitajika. Hivyo mama ataupiga mwingi kama ataliweka mezani swala la utawala wa majimbo na kuliingiza kwenye katiba mpya. Muda wa hili umefika.
 
Rushwa zimekua nje nje sio kujificha tena, mcheke kg 3500, maharage kg3200, mafuta ya kupikia lita 7000, unga wa sembe kg 2000 mwanga gani unaongelea ndugu yetu??. Bado umeme na maji ni shidaaa. Ifike stage tujitambue kama taifa tuache uchawa usio na faida
Omba mungu Vita ya ukrain na urusi iiishe. Haya Mambo ni mtambuka tu
 
Back
Top Bottom