Ukweli ni Kwamba Rais Samia ameleta mwanga

Tukitaka Taifa letu liwe mahali salama, cha kwanza ni lazima liwe na uongozi mzuri. Na kazi ya kuhakikisha Taifa linakuwa na uongozi mzuri, ni la sisi wananchi.

Wananchi hatustahili kuwa chawa wa watu au vyama, bali tuwe chawa wa kudumu wa ukweli, ingawa ni sahihi pia, kile ninachokiona mimi kuwa ni kweli kinaweza kisiwe ukweli, lakini ukweli hubakia ni ule ule wakati wote.

Viongozi wetu wanapofanya vizuri ni vizuri kuwapa moyo ili wafanye vizuri zaidi. Wanapofanya vibaya, ni muhimu kuwakosoa ili wabadilike, au kama hawawezi kubadilika, mamlaka zilizowaweka kwenye nafasi za uongozi ziwaondoe.

Kuna watu wanafikiria kuwa wanastahili kuwa viongozi wakati wote, na wengine wanaona kutokuwa viongozi ni adhabu. Hao ni tatizo kubwa. Ndio hao walio tayari kufanya chochote ili kuupata uongozi. Hawa ni maadui wa Taifa. Huwa ndio ambao kila siku, usiku na mchana wanafikiria kuweka hata sheria mbaya, wapo tayari kutumia vyombo vya dola vibaya, wapo tayari kufanya hata hadaa, na wakati mwingine wapo tayari kuteka, kutesa, na hata kuua ilimradi wabakie madarakani.

Kwa kuangalia mahali ambapo nchi ilikuwa kabla ya utawala wa Rais Samia, hakika yaliyofanyika katika muda mfupi wa uongozi wake, yanastahili pongezi KUBWA SANA:

1) Watu wengi waliofungwa kwa uonevu, hasa kutoka vyama vya upinzani, sahizi wapo huru. Ni furaha ilioje kwa wanafamilia wa watu hawa. KAMA BADO WALIOPO GEREZANI, TUNAOMBA WOTE WAACHIWE HURU.

2) Miili ya watu kupatikana kwenye viroba, watu kutekwa, kuteswa, kushambuliwa kwa risasi kama alivyofanyiwa Lisu, hakusikiki tena. TUNAOMBA KUWE NA SHERIA INAYOZUIA KABISA VYOMBO VYA USALAMA KUTEKA WATU. MTU KAMA ANA KOSA AKAMATWE LAKINI ASITEKWE.

3) Watu kutengenezewa kesi za uhujumu uchumi, na kuporwa pesa zao kwenye akaunti za benki, kumekoma. ILI KUZUIA MAMBO HAYA KUTOKEA TENA, ZILE SHERIA ZILIZOWEZESHA HAYO KUTENDEKA, ZIFUTWE.

5) Police kugeuka kuwa idara ya mapato barabarani, kumetoweka au kupungua. ILI KUWEKA MAZINGIRA MAZURI YA MATUMIZI YA BARABARA, VIBAO VYA 50KM/HR NA MATUTA KILA SEHEMU, KUANGALIWE UPYA, MAPENDEKEZO YATALETWA KWENYE JUKWAA LETU ILI WADAU WACHANGIE MAWAZO MAANA NI KERO KUBWA.

6) Kauli za uwongo za viongozi wa Serikali zimepungua. Zile kauli za uwongo kama zile za kusema eti makinikia yana dhahabu 90%, eti tunadai kodi ya zaidi ya trilioni 400 kutoka kampuni ya madini, tunajenga miradi yetu yote kwa pesa ya ndani; na ili wananchi waendelee kudanganywa mpaka tukajitoa mwenye UWAZI WA SERIKALI. WAKATI RAIS ANAJITAHIDI KUWEKA WAZI TAARIFA ZA KWELI, BADO KUNA VIONGOZI WANAOPENDA UWONGO, VIONGOZI WA NAMNA HIYO WAONDOLEWE. Ni haki wananchi kuambiwa ukweli wakati wote, hata kama ni ukweli unaoumiza.

7) Kwenye demokrasia, mwanga mkubwa umeanza kuonekana. Taarifa ya kikosi kazi aliyokabidhiwa Rais, na mara moja Rais kutoa kauli ya kuanza kuifanyia kazi, ni hatua kubwa sana. MAPENDEKEZO YALE YAKIFANYIWA KAZI NA KUTEKELEZWA KIKAMILIFU, HAKIKA RAIS SAMIA ATAWEKA ALAMA KATIKA TAIFA HILI, ISIYOFUTIKA. CHADEMA, bila ya kuangalia mchakato ulivyoanza, unganishe nguvu na wadau wengine ili Taifa lililobora. Kufanya hivyo kuna faida kubwa zaidi kuliko kuendelea kuwa nje. RAIS AEBDELEE KULINDA HAKI ZA KIDEMOKRASIA KWA KUHAKIKISHA TUNAKUWA NA KATIBA NA SHERIA ZINAZOHIFADHI HAKI HIZO. TUNASUBURIA SIKU AMBAPO KILA MWANAJF ATAPENDA KUWEKA JINA LAKE HALISI WAZI BILA YA HOFU YA KUTEKWA AU KUITWA KWEBYE KAMATI YA MAADILI YA BUNGE KAMA ALIVYOFANYIWA NDUGU YETU MAYALA, KWA VILE TU AMETOA MAONI YAKE.

8) Rais amekuwa akiufuta uchumi wa nadharia, uchumi usio na mizizi, na kujenga sustainable economy. Rais ni dhahiri anatengeneza mifumo ya uchumi imara, uchumi unaojiendesha, siyo ule uchumi wa hadaa. Japo, kwa haraka, tunaweza tusione matokeo yake kwa sababu inahitaji muda. Mambo yale ya kusema, eti korosho zote zitanunuliwa na jeshi, au kuanzia leo hakuna kuuza mahindi nje, yanaharibu na kuua sustainable economy, kwa sababu unaua mifumo ya uzalishaji, usafirishaji, utunzaji na uuzaji; shughuli ambazo zote kwa pamoja huchangia na kuhuisha uchumi. TUNAOMBA SERIKALI ISIISHIE TU KWENYE MAELEKEZO NA MAAGIZO, BALI IENDE PIA KWENYE KUTENGENEZA MABADILIKO YA SHERIA ILI KULINDA MIFUMO YA UCHUMI.

Kwa namna nchi ilivyokuwa imeharibika, mabadiliko yanayofanyika sasa hivi, hayawezi kutoa matunda tarajiwa kwa muda mfupi, lakini nina hakika mbeleni kila mmoja ataona faida ya kuwa na mifumo mizuri ya uongozi.

KWA YALE AMBAYO RAIS SAMIA NA WASAIDIZI WAMETENDA VEMA, JAPO NI WAJIBU WAO, TUNAWAPONGEZA,NA KUWATIA MOYO WATENDE VIZURI ZAIDI. NA KILA WALIPO NA DHAMIRA NJEMA, MWENYEZI MUNGU AKASHUSHE BARAKA ZAKE. Lakini viongozi wanafiki, wazidi kuumbuliwa na kuanikwa. Tunataka viongozi walio wakweli kwa kauli na vitendo.

Kwa vyovyote vile, tupo kwenye mazingira mazuri zaidi sana sasa kuliko ilivyokuwa katika utawala uliotangulia.

Kule Simiyu kuna kijana kafungwa miaka 7 jela kwa kumsema vibaya Rais. Hatujui alisema nini, lakini kwa vyovyote vile, hata kama sheria zetu zinaruhusu adhabu kama hiyo, busara ingetumika. Adhabu hiyo ni kali sana. Kama kuwafunga wapinzani kwa kumkosoa Rais haikuwa jambo jema, basi haitakuwa sahihi pia kumfanyia jambo hilo hilo mwingine yeyote. Kwa vyovyote vile, hukumu kama ile haiwezi kumfurahisha hata Rais Samia ambaye anataka kuijenga nchi yenye demokrasia, uhuru wa maoni na haki.
Umeandika gazeti la ujinga.

Mnambwela sana ndo maana mnajieleza eleza.

You don't need to express yourself so much for people to understand..

Samia hakuna lolote analofanya tofauti na kufanya maisha kuwa magumu na ubadhilifu wa Mali za umma.
 
Uchumi ni wawekezaji. Kipindi hiki wawekezaji wanamwagika Kila Kona ya nchi. Impact yake ni ajira Kila Kona siku hizi humuoni graduate anatembeza karanga au urembo barabarani
Nitajie hao wawekezaji.
 
We mvaa kobazi akili zako zipo kwenye nsonyo, hakuna msafara ambao ni kero. Viongozi lazima wapate heshima, wacha upumbavu wako. Wakati wenzenu wanapeleka Watoto shule wewe ulikuwa unakaririshwa majini.
Kwani huwezi kushambulia hoja kwa hoja, badala ya kumshambulia mtoa hoja?
 
Mimi ni kati ya wanaopinga, siyo tozo tu, bali hata VAT (iliyoanzishwa na utawala wa marehemu Magufuli) kwenye miamala ya simu. Hakuna mantiki.

Miamala ingebakia tu gharama za mtoa huduma kwa sababu anatumia mawakala ambavyo kwa vyovyote wanahitaji malipo. Faida inayopatikana kwenye huduma hiyo, ndiyo ipigwe kodi kwa mtoa huduma, kimsingi ndiye aliyetengeneza faida. Kuning'iniza kodi nyingi kwenye kipato kile kile (mshahara umelipiwa PAYE, kama umetuma hela uliyoipata kwenye biashara, nako imelipiwa kodi, na unayemtumia atakapoenda kuitumia atalipa kodi).

LAKINI PAMOJA NA HAYO YOTE, BADO NAAMINI TUPO KWENYE UONGOZI MZURI ZAIDI KULIKO AWAMU ILIYOTANGULIA.
Shida ni wewe kuweka benchmark test kuwa ni uongozi wa JPM.
Ungeweka Benchmark ya Mkapa au Nyerere.
 
Tukitaka Taifa letu liwe mahali salama, cha kwanza ni lazima liwe na uongozi mzuri. Na kazi ya kuhakikisha Taifa linakuwa na uongozi mzuri, ni la sisi wananchi.

Wananchi hatustahili kuwa chawa wa watu au vyama, bali tuwe chawa wa kudumu wa ukweli, ingawa ni sahihi pia, kile ninachokiona mimi kuwa ni kweli kinaweza kisiwe ukweli, lakini ukweli hubakia ni ule ule wakati wote.

Viongozi wetu wanapofanya vizuri ni vizuri kuwapa moyo ili wafanye vizuri zaidi. Wanapofanya vibaya, ni muhimu kuwakosoa ili wabadilike, au kama hawawezi kubadilika, mamlaka zilizowaweka kwenye nafasi za uongozi ziwaondoe.

Kuna watu wanafikiria kuwa wanastahili kuwa viongozi wakati wote, na wengine wanaona kutokuwa viongozi ni adhabu. Hao ni tatizo kubwa. Ndio hao walio tayari kufanya chochote ili kuupata uongozi. Hawa ni maadui wa Taifa. Huwa ndio ambao kila siku, usiku na mchana wanafikiria kuweka hata sheria mbaya, wapo tayari kutumia vyombo vya dola vibaya, wapo tayari kufanya hata hadaa, na wakati mwingine wapo tayari kuteka, kutesa, na hata kuua ilimradi wabakie madarakani.

Kwa kuangalia mahali ambapo nchi ilikuwa kabla ya utawala wa Rais Samia, hakika yaliyofanyika katika muda mfupi wa uongozi wake, yanastahili pongezi KUBWA SANA:

1) Watu wengi waliofungwa kwa uonevu, hasa kutoka vyama vya upinzani, sahizi wapo huru. Ni furaha ilioje kwa wanafamilia wa watu hawa. KAMA BADO WALIOPO GEREZANI, TUNAOMBA WOTE WAACHIWE HURU.

2) Miili ya watu kupatikana kwenye viroba, watu kutekwa, kuteswa, kushambuliwa kwa risasi kama alivyofanyiwa Lisu, hakusikiki tena. TUNAOMBA KUWE NA SHERIA INAYOZUIA KABISA VYOMBO VYA USALAMA KUTEKA WATU. MTU KAMA ANA KOSA AKAMATWE LAKINI ASITEKWE.

3) Watu kutengenezewa kesi za uhujumu uchumi, na kuporwa pesa zao kwenye akaunti za benki, kumekoma. ILI KUZUIA MAMBO HAYA KUTOKEA TENA, ZILE SHERIA ZILIZOWEZESHA HAYO KUTENDEKA, ZIFUTWE.

5) Police kugeuka kuwa idara ya mapato barabarani, kumetoweka au kupungua. ILI KUWEKA MAZINGIRA MAZURI YA MATUMIZI YA BARABARA, VIBAO VYA 50KM/HR NA MATUTA KILA SEHEMU, KUANGALIWE UPYA, MAPENDEKEZO YATALETWA KWENYE JUKWAA LETU ILI WADAU WACHANGIE MAWAZO MAANA NI KERO KUBWA.

6) Kauli za uwongo za viongozi wa Serikali zimepungua. Zile kauli za uwongo kama zile za kusema eti makinikia yana dhahabu 90%, eti tunadai kodi ya zaidi ya trilioni 400 kutoka kampuni ya madini, tunajenga miradi yetu yote kwa pesa ya ndani; na ili wananchi waendelee kudanganywa mpaka tukajitoa mwenye UWAZI WA SERIKALI. WAKATI RAIS ANAJITAHIDI KUWEKA WAZI TAARIFA ZA KWELI, BADO KUNA VIONGOZI WANAOPENDA UWONGO, VIONGOZI WA NAMNA HIYO WAONDOLEWE. Ni haki wananchi kuambiwa ukweli wakati wote, hata kama ni ukweli unaoumiza.

7) Kwenye demokrasia, mwanga mkubwa umeanza kuonekana. Taarifa ya kikosi kazi aliyokabidhiwa Rais, na mara moja Rais kutoa kauli ya kuanza kuifanyia kazi, ni hatua kubwa sana. MAPENDEKEZO YALE YAKIFANYIWA KAZI NA KUTEKELEZWA KIKAMILIFU, HAKIKA RAIS SAMIA ATAWEKA ALAMA KATIKA TAIFA HILI, ISIYOFUTIKA. CHADEMA, bila ya kuangalia mchakato ulivyoanza, unganishe nguvu na wadau wengine ili Taifa lililobora. Kufanya hivyo kuna faida kubwa zaidi kuliko kuendelea kuwa nje. RAIS AEBDELEE KULINDA HAKI ZA KIDEMOKRASIA KWA KUHAKIKISHA TUNAKUWA NA KATIBA NA SHERIA ZINAZOHIFADHI HAKI HIZO. TUNASUBURIA SIKU AMBAPO KILA MWANAJF ATAPENDA KUWEKA JINA LAKE HALISI WAZI BILA YA HOFU YA KUTEKWA AU KUITWA KWEBYE KAMATI YA MAADILI YA BUNGE KAMA ALIVYOFANYIWA NDUGU YETU MAYALA, KWA VILE TU AMETOA MAONI YAKE.

8) Rais amekuwa akiufuta uchumi wa nadharia, uchumi usio na mizizi, na kujenga sustainable economy. Rais ni dhahiri anatengeneza mifumo ya uchumi imara, uchumi unaojiendesha, siyo ule uchumi wa hadaa. Japo, kwa haraka, tunaweza tusione matokeo yake kwa sababu inahitaji muda. Mambo yale ya kusema, eti korosho zote zitanunuliwa na jeshi, au kuanzia leo hakuna kuuza mahindi nje, yanaharibu na kuua sustainable economy, kwa sababu unaua mifumo ya uzalishaji, usafirishaji, utunzaji na uuzaji; shughuli ambazo zote kwa pamoja huchangia na kuhuisha uchumi. TUNAOMBA SERIKALI ISIISHIE TU KWENYE MAELEKEZO NA MAAGIZO, BALI IENDE PIA KWENYE KUTENGENEZA MABADILIKO YA SHERIA ILI KULINDA MIFUMO YA UCHUMI.

Kwa namna nchi ilivyokuwa imeharibika, mabadiliko yanayofanyika sasa hivi, hayawezi kutoa matunda tarajiwa kwa muda mfupi, lakini nina hakika mbeleni kila mmoja ataona faida ya kuwa na mifumo mizuri ya uongozi.

KWA YALE AMBAYO RAIS SAMIA NA WASAIDIZI WAMETENDA VEMA, JAPO NI WAJIBU WAO, TUNAWAPONGEZA,NA KUWATIA MOYO WATENDE VIZURI ZAIDI. NA KILA WALIPO NA DHAMIRA NJEMA, MWENYEZI MUNGU AKASHUSHE BARAKA ZAKE. Lakini viongozi wanafiki, wazidi kuumbuliwa na kuanikwa. Tunataka viongozi walio wakweli kwa kauli na vitendo.

Kwa vyovyote vile, tupo kwenye mazingira mazuri zaidi sana sasa kuliko ilivyokuwa katika utawala uliotangulia.

Kule Simiyu kuna kijana kafungwa miaka 7 jela kwa kumsema vibaya Rais. Hatujui alisema nini, lakini kwa vyovyote vile, hata kama sheria zetu zinaruhusu adhabu kama hiyo, busara ingetumika. Adhabu hiyo ni kali sana. Kama kuwafunga wapinzani kwa kumkosoa Rais haikuwa jambo jema, basi haitakuwa sahihi pia kumfanyia jambo hilo hilo mwingine yeyote. Kwa vyovyote vile, hukumu kama ile haiwezi kumfurahisha hata Rais Samia ambaye anataka kuijenga nchi yenye demokrasia, uhuru wa maoni na haki.

Mungu amsaidie mama huyu ni kiongozi wa mfano.
 
Umeandika gazeti la ujinga.

Mnambwela sana ndo maana mnajieleza eleza.

You don't need to express yourself so much for people to understand..

Samia hakuna lolote analofanya tofauti na kufanya maisha kuwa magumu na ubadhilifu wa Mali za umma.
You need at least an average mind to differentiate between material from none, unfortunately you are not even close to the bottom limit of an average mind.
 
Shida ni wewe kuweka benchmark test kuwa ni uongozi wa JPM.
Ungeweka Benchmark ya Mkapa au Nyerere.
Nia yangu haikuwa kufanya ranking ya viongozi. Na wala hakuna mahali niliposema kuwa utawala huu ni bora kuliko tawala zote. Zaidi nimeangalia mahali ambapo tulikuwa.

Huko nyuma, pamoja na mapungufu ya hapa na pale, lakini angalao tulikuwa kwenye njia iliyokuwa inatupatia matumaini kuwa kuna siku tutafika. Lakini ikatokea ajali 2015, tukapotea kabisa, karibia kwenye nyanja zote. Tukawa gizani kabisa bila ya nuru yoyote.

Mwalimu Nyerere alihimiza sana ukosoaji, tena akasema anawataka vijana jeuri wanaoweza kuhoji mambo. Wakati wa awamu ya 5, tukaingia kwenye giza totoro. Ukihoji au kukosoa, ni sawa na kufanya uhaini, ambapo adhabu yako, ukiwa na bahati sana ni kutekwa, kuteswa au kubambikiwa kesi. Ukiwa na bahati mbaya, ni kupotezwa moja kwa moja.

Mwalimu alisisitiza sana maendeleo ya watu badala ya vitu, demokrasia ndani ya chama. Lakini awamu ya 5 ikawapeleka watu gizani kabisa. Mwalimu alisistiza sana umoja, na alikemea sana ubaguzi wowote ule. Awamu ya 5 ikatushusha gizani kabisa kwa kuendekeza upendeleo wa kikanda, na hata kutamka wazi kuwa hapeleki maendeleo watu wakimchagua mbunge kutoka vyama vya upinzani. Mwalimu, kutokana na mabadiliko ya Dunia, alisema ni lazima tuwe na vyama vingi vya siasa. Wakati wa awamu ya 5, tukaambiwa na Rais kuwa kufikia 2020 atahakikisha hakuna vyama vya upinzani.

Mkapa ndiye alitengeneza mifumo mingi ya utawala, kuanzia kwenye kodi mpaka kwenye matumizi ya pesa ya umma. Rais wa awamu ya 5 akaifuta mifumo yote,na kuifanya pesa ya umma kama ya kwake binafsi, na kuitumia alivyopenda.

Mzee Mwinyi alisistiza sana uhuru wa watu, hata akaitwa mzee ruksa. Lakini Rais wa awamu ya 5 aliua kabisa uhuru, hata kufikia kwa uwazi kabisa kuviambia vyombo vya habari visifikirie vipo huru kiasi wanachodhania.

Kikwete, alikuwa mvumilivu sana. Alisemwa sana. Aliongeza uwazi wa matumizi ya Serikali, kiasi sisi sote kujua matumizi yalivyokuwa, na ndiyo maana matumjzi yalipokuwa mabaya, tuliweza kuona haraka. Marehemu Magufuli akaiondoa Tanzania kwenye kundi la nchi ambazo matumizi ya Serikali hufanywa kwa uwazi.

Karibia kila mahali kulikuwa na giza. Ninachosema ni giza lile lililowekwa na utawala wa awamu ya 5 limeanza kuondolewa taratibu na awamu hii, japo halijaondoka kwa 100% lakini tunaanza kuuona mwanga.
 
We mvaa kobazi akili zako zipo kwenye nsonyo, hakuna msafara ambao ni kero. Viongozi lazima wapate heshima, wacha upumbavu wako. Wakati wenzenu wanapeleka Watoto shule wewe ulikuwa unakaririshwa majini.
Kwani wanaopata madarakani hapa nchini ni lazima wawe ni wenye elimu kubwa? Heshima inatakiwa apewe kiongozi aliyeingia madarakani kwa njia halali, sio kwa ule uchaguzi wa kihayawani wa 2020.
 
Mikutano ya vyama vya siasa haistahili kuruhusiwa wala kuzuiwa na Rais. Inatakiwa kufanyika kwa mujibu wa sheria na katiba.

Mtangulizi wake alivunja kwa kukanyaga na kuisigina katiba, alizuia mikutano ya vyama vya siasa.

Sasa, nadhani haitakiwi mikutano ya vyama vya siasa kurudi kwa agizo la Rais bali kwa sheria itakayoilinda ili isiwe Rais wala Polisi watakaokuwa na haki ya kuzuia au kuruhusu mikutano ya vyama vya siasa. Rais awe na uwezo wa kuizuia mikutano na mikusanyiko yote kwa sheria ya tangazo la hali ya hatari tu.
Huu ndio undumilakuwili, umeliona kosa kwa Samia badala ya kulaani, unakimbilia kutoa ushauri, lakini naamini kama angekuwa Magufuli ungelaani, wakati mwingine reasoning yenu inatawaliwa na mahaba sana.

Unashangaza unaposema Magufuli alizuia kwa kukanyaga na kusigina, lakini kwa Samia upo kimya..!!

The truth is, kama Magufuli alizuia kwa kusigina, hata Samia nae anaizuia kwa kusigina, wote hawafuati sheria, wacha double standard.

Haiwezekani CCM kila siku wanafanya mikutano ya siasa kwao sheria haihitaji kutazamwa, iko vizuri; ila kwa wapinzani ndio sheria inahitaji kutazamwa tena!

Na sijui ni mwanga gani unaouona kwa mtu asiyefuata sheria, labda mwanga wa giza.
 
Huu ndio undumilakuwili, umeliona kosa kwa Samia badala ya kulaani, unakimbilia kutoa ushauri, lakini naamini kama angekuwa Magufuli ungelaani, wakati mwingine reasoning yenu inatawaliwa na mahaba sana.

Unashangaza unaposema Magufuli alizuia kwa kusigina, lakini kwa Samia upo kimya..

The truth is, kama Magufuli alizuia kwa kusigina, hata Samia nae anaizuia kwa kusigina, wote hawafuati sheria, wacha double standard.

Haiwezekani CCM kila siku wanafanya mikutano ya siasa kwao sheria haihitaji kutazamwa, iko vizuri; ila kwa wapinzani ndio sheria inahitaji kutazamwa tena!

Na sijui ni mwanga gani unaouona kwa mtu asiyefuata sheria, labda mwanga wa giza.
Ni suala la lugha tu.

Kuanza kuuona mwanga, ni tofauti na kuishi katika mwanga.

Bado kuna mengi ambayo hayapo sawa:
1) Bado tupo chini ya katiba mbaya kabisa. Kauli tu ya kusema kuwa kutakuwa na mchakato wa kupata katiba mpya ni dalili ya kwenda kwenye mwanga. Kama yatabakia tu kuwa maneno, basi hatutafika kwenye mwanga. Mtangulizi wake alisema kwa uwazi kabisa kuwa katiba mpya siyo miongoni mwa ajenda zake.

2) Kuzuia mikutano ya vyama vya siasa ni giza. Lakini kueleza kuwa kutakuwa na utaratibu utakaozuia kugandamizwa kwa haki hii ya kikatiba, ni dalili ya mwanga. Hata kama na CCM nao wasingekuwa wanafanya mikutano, bado isingehalalisha uzuiaji wa mikutano ya vyama vya siasa.

3) Kutokuwepo kwa Tume Huru ya uchaguzi ni giza. Lakini kuna matumani, kutokana na kauli ya kuwa kutakuwa na Tume huru ya uchaguzi. Kama itabakia tu kwenye kauli bila ya vitendo, haitakuwa na msaada wowote, tutaendelea kuwa gizani, na kuna siku wananchi watachukua hatua.

Ukweli ni kwamba, ilitakiwa turudi kwenye utii wa katiba iliyopo kwa 100%, hata kama ni upungufu, wakati tunasubiri maboresho. Mikutano ya siasa haistahili kuruhusiwa na mtu, kwa vile tayari katiba ilikwisharuhusu.

Na kwa ushauri, Rais anastahili tu kutamka kuwa wakati tunasubiri maboresho, vyama vyote vya siasa, viendelee na yale yote ambayo katiba ya sasa inaruhusu, ikiwemo mikutano ya hadhara na ya ndani.
 
Ukiachana na demokrasia na haki za watu, Magufuli alikuwa rais wa hatari sana kwenye uchumi wa nchi
Kwa sababu alikuwa hatabiriki kwenye maamuzi maamuzi muhimu na alikuwa hasikilizi mtu

Imagine lile suala la korosho kipindi kile anaagiza jeshi kukusanya na kubangua hata kwa mabomu

Imagine kipindi kile maduka ya kubadilishia fedha yanavamiwa ghafla na wanajeshi na kupora fedha zote

Imagine ule utopolo unaoitwa vitambulisho vya machinga, visivyokuwa na jina wala picha
Sikuwa namkubali magufuli kwenye baadhi ya mambo ila huwa nachukia watu kama ninyi kuongea mambo ambayo hamna uhakika nayo,angalia hapo unapodai eti korosho kuna watu hawajapata pesa hiyo sio kweli ni uzushi tu hamna mkulima ambae hakupata hela yake
 
Kama wale wanaosema vinginevyo wanafukuzwa kazi na wengine kufungwa Kabisa does it mean nyie mnaosifia mnapewa Bakishishi au ni walamba asali ?
 
Yule mporaji hakukataa kulipa watu kwa kisingizio kuwa hawana mashamba?
 
Tukitaka Taifa letu liwe mahali salama, cha kwanza ni lazima liwe na uongozi mzuri. Na kazi ya kuhakikisha Taifa linakuwa na uongozi mzuri, ni la sisi wananchi.

Wananchi hatustahili kuwa chawa wa watu au vyama, bali tuwe chawa wa kudumu wa ukweli, ingawa ni sahihi pia, kile ninachokiona mimi kuwa ni kweli kinaweza kisiwe ukweli, lakini ukweli hubakia ni ule ule wakati wote.

Viongozi wetu wanapofanya vizuri ni vizuri kuwapa moyo ili wafanye vizuri zaidi. Wanapofanya vibaya, ni muhimu kuwakosoa ili wabadilike, au kama hawawezi kubadilika, mamlaka zilizowaweka kwenye nafasi za uongozi ziwaondoe.

Kuna watu wanafikiria kuwa wanastahili kuwa viongozi wakati wote, na wengine wanaona kutokuwa viongozi ni adhabu. Hao ni tatizo kubwa. Ndio hao walio tayari kufanya chochote ili kuupata uongozi. Hawa ni maadui wa Taifa. Huwa ndio ambao kila siku, usiku na mchana wanafikiria kuweka hata sheria mbaya, wapo tayari kutumia vyombo vya dola vibaya, wapo tayari kufanya hata hadaa, na wakati mwingine wapo tayari kuteka, kutesa, na hata kuua ilimradi wabakie madarakani.

Kwa kuangalia mahali ambapo nchi ilikuwa kabla ya utawala wa Rais Samia, hakika yaliyofanyika katika muda mfupi wa uongozi wake, yanastahili pongezi KUBWA SANA:

1) Watu wengi waliofungwa kwa uonevu, hasa kutoka vyama vya upinzani, sahizi wapo huru. Ni furaha ilioje kwa wanafamilia wa watu hawa. KAMA BADO WALIOPO GEREZANI, TUNAOMBA WOTE WAACHIWE HURU.

2) Miili ya watu kupatikana kwenye viroba, watu kutekwa, kuteswa, kushambuliwa kwa risasi kama alivyofanyiwa Lisu, hakusikiki tena. TUNAOMBA KUWE NA SHERIA INAYOZUIA KABISA VYOMBO VYA USALAMA KUTEKA WATU. MTU KAMA ANA KOSA AKAMATWE LAKINI ASITEKWE.

3) Watu kutengenezewa kesi za uhujumu uchumi, na kuporwa pesa zao kwenye akaunti za benki, kumekoma. ILI KUZUIA MAMBO HAYA KUTOKEA TENA, ZILE SHERIA ZILIZOWEZESHA HAYO KUTENDEKA, ZIFUTWE.

5) Police kugeuka kuwa idara ya mapato barabarani, kumetoweka au kupungua. ILI KUWEKA MAZINGIRA MAZURI YA MATUMIZI YA BARABARA, VIBAO VYA 50KM/HR NA MATUTA KILA SEHEMU, KUANGALIWE UPYA, MAPENDEKEZO YATALETWA KWENYE JUKWAA LETU ILI WADAU WACHANGIE MAWAZO MAANA NI KERO KUBWA.

6) Kauli za uwongo za viongozi wa Serikali zimepungua. Zile kauli za uwongo kama zile za kusema eti makinikia yana dhahabu 90%, eti tunadai kodi ya zaidi ya trilioni 400 kutoka kampuni ya madini, tunajenga miradi yetu yote kwa pesa ya ndani; na ili wananchi waendelee kudanganywa mpaka tukajitoa mwenye UWAZI WA SERIKALI. WAKATI RAIS ANAJITAHIDI KUWEKA WAZI TAARIFA ZA KWELI, BADO KUNA VIONGOZI WANAOPENDA UWONGO, VIONGOZI WA NAMNA HIYO WAONDOLEWE. Ni haki wananchi kuambiwa ukweli wakati wote, hata kama ni ukweli unaoumiza.

7) Kwenye demokrasia, mwanga mkubwa umeanza kuonekana. Taarifa ya kikosi kazi aliyokabidhiwa Rais, na mara moja Rais kutoa kauli ya kuanza kuifanyia kazi, ni hatua kubwa sana. MAPENDEKEZO YALE YAKIFANYIWA KAZI NA KUTEKELEZWA KIKAMILIFU, HAKIKA RAIS SAMIA ATAWEKA ALAMA KATIKA TAIFA HILI, ISIYOFUTIKA. CHADEMA, bila ya kuangalia mchakato ulivyoanza, unganishe nguvu na wadau wengine ili Taifa lililobora. Kufanya hivyo kuna faida kubwa zaidi kuliko kuendelea kuwa nje. RAIS AEBDELEE KULINDA HAKI ZA KIDEMOKRASIA KWA KUHAKIKISHA TUNAKUWA NA KATIBA NA SHERIA ZINAZOHIFADHI HAKI HIZO. TUNASUBURIA SIKU AMBAPO KILA MWANAJF ATAPENDA KUWEKA JINA LAKE HALISI WAZI BILA YA HOFU YA KUTEKWA AU KUITWA KWEBYE KAMATI YA MAADILI YA BUNGE KAMA ALIVYOFANYIWA NDUGU YETU MAYALA, KWA VILE TU AMETOA MAONI YAKE.

8) Rais amekuwa akiufuta uchumi wa nadharia, uchumi usio na mizizi, na kujenga sustainable economy. Rais ni dhahiri anatengeneza mifumo ya uchumi imara, uchumi unaojiendesha, siyo ule uchumi wa hadaa. Japo, kwa haraka, tunaweza tusione matokeo yake kwa sababu inahitaji muda. Mambo yale ya kusema, eti korosho zote zitanunuliwa na jeshi, au kuanzia leo hakuna kuuza mahindi nje, yanaharibu na kuua sustainable economy, kwa sababu unaua mifumo ya uzalishaji, usafirishaji, utunzaji na uuzaji; shughuli ambazo zote kwa pamoja huchangia na kuhuisha uchumi. TUNAOMBA SERIKALI ISIISHIE TU KWENYE MAELEKEZO NA MAAGIZO, BALI IENDE PIA KWENYE KUTENGENEZA MABADILIKO YA SHERIA ILI KULINDA MIFUMO YA UCHUMI.

Kwa namna nchi ilivyokuwa imeharibika, mabadiliko yanayofanyika sasa hivi, hayawezi kutoa matunda tarajiwa kwa muda mfupi, lakini nina hakika mbeleni kila mmoja ataona faida ya kuwa na mifumo mizuri ya uongozi.

KWA YALE AMBAYO RAIS SAMIA NA WASAIDIZI WAMETENDA VEMA, JAPO NI WAJIBU WAO, TUNAWAPONGEZA,NA KUWATIA MOYO WATENDE VIZURI ZAIDI. NA KILA WALIPO NA DHAMIRA NJEMA, MWENYEZI MUNGU AKASHUSHE BARAKA ZAKE. Lakini viongozi wanafiki, wazidi kuumbuliwa na kuanikwa. Tunataka viongozi walio wakweli kwa kauli na vitendo.

Kwa vyovyote vile, tupo kwenye mazingira mazuri zaidi sana sasa kuliko ilivyokuwa katika utawala uliotangulia.

Kule Simiyu kuna kijana kafungwa miaka 7 jela kwa kumsema vibaya Rais. Hatujui alisema nini, lakini kwa vyovyote vile, hata kama sheria zetu zinaruhusu adhabu kama hiyo, busara ingetumika. Adhabu hiyo ni kali sana. Kama kuwafunga wapinzani kwa kumkosoa Rais haikuwa jambo jema, basi haitakuwa sahihi pia kumfanyia jambo hilo hilo mwingine yeyote. Kwa vyovyote vile, hukumu kama ile haiwezi kumfurahisha hata Rais Samia ambaye anataka kuijenga nchi yenye demokrasia, uhuru wa maoni na haki.
Jiwe hakufaa kuwa Rais kabisa, jitu liuaji lenye roho mbaya, yule hakuwa binadamu
 
Kama wale wanaosema vinginevyo wanafukuzwa kazi na wengine kufungwa Kabisa does it mean nyie mnaosifia mnapewa Bakishishi au ni walamba asali ?
Unataka mtu atukane viongozi asipewe hukumu?
 
Ukiachana na demokrasia na haki za watu, Magufuli alikuwa rais wa hatari sana kwenye uchumi wa nchi
Kwa sababu alikuwa hatabiriki kwenye maamuzi maamuzi muhimu na alikuwa hasikilizi mtu

Imagine lile suala la korosho kipindi kile anaagiza jeshi kukusanya na kubangua hata kwa mabomu

Imagine kipindi kile maduka ya kubadilishia fedha yanavamiwa ghafla na wanajeshi na kupora fedha zote

Imagine ule utopolo unaoitwa vitambulisho vya machinga, visivyokuwa na jina wala picha
Yule mzee alikuwa empty kichwani
 
Back
Top Bottom