Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 19,768
- 49,949
- Thread starter
- #81
Ni rahisi sana kulaumu.JPM kiburi kilimzidi ingawa kila alipohutubia alitukumbusha tumuombee. Jeuri kwa ngazi ya urais haina faida. Unakuwa ukiwaumiza mamilioni ya watu wasio na hatia.
Huwezi kusema matajiri waishi kama mashetani pasipo kuwaumiza wafanyakazi na mzunguko mzima wa pesa. Unawachukia watu waliohangaika mpaka kufika juu kwenye jamii ili upate nini kutokana na hiyo chuki?.
Rais ni mtu mkubwa sana, unaweza kukuta Rais Samia hata hajawahi kumuona wala kusoma hicho alichotukanwa mpaka mtu akala mvua ndefu kiasi hicho. Huo ni ukubwa wa taasisi ya urais Tanzania.
Credit moja kubwa kwa Rais Samia ni kwamba anafahamu kuwa nchi ina watu wengi wenye vipaji mbalimbali, ujuzi mbalimbali, uwezo mbalimbali; na anafahamu kuwa yeye kuwa Rais haimaanishi amebeba vipaji vya watu wote, uwezo wa watu wote na ujuzi wa watu wote. Ndiyo maana hata katika maamuzi hujipa muda ili kuwashirikisha wengine katika maamuzi yake.
Magufuli aliamini kuwa yeye mmoja ni bora kuliko Watanzania wote wakiwekwa pamoja. Matokeo yake akaharibu karibia kila eneo.