Synthesizer
JF-Expert Member
- Feb 15, 2010
- 11,143
- 18,774
Sio lengo langu kutoa uzi huu kwa kivuli cha kampeni. Najua kuna mengi yanasemwa kuhusu Lowassa ambayo hata mie nakubaliana na baadhi. Hata hivyo, ni vema pia tukayasema ya Magufuli, ili Watanzania waelewe tunatarajia kuwa na viongozi wa aina gani.
Katika maamuzi ya Magufuli ambayo yaliniacha mdomo wazi ni lile la kugoma katakata kupeleka boti za Azam Ziwa Victoria toka Bandari ya Dar, akidai zingeharibu madaraja yetu.
Wakati Magufuli akiweka msimamo huo, Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi wakati huo, Prof Mwandosya, alijaribu ku-reason naye kwamba boti hizo hazikuwa na uzito wa kuweza kuharibu madaraja, kutokana na data walizokuwa nazo. Mwandosya alisisitiza juu yan umuhimu wa kutatua tatizo la usafiri kwa wananchi wa eneo la ziwa Victoria kwa kutumia boti hizo. Magufuli alikataa katakata na hata kutoa kauli kwamba kama mnataka zikateni vipande vipande hizo boti mkaziunganishe Mwanza, akijua hilo lisingewezekana.
Ilikuwa ni busara na hekima za Prof Mwandosya zilizoleta ufumbuzi kwa suala hili. Mwandosya aliwaendea Wa-Kenya na kuwaeleza tatizo alilokuwa akipata toka kwa Waziri mwenzake. Akawaomba Wakenya boti zisafirishwe kwenda Victoria kwa barabara toka Mombasa. Wakenya waliomba data za boti na wakaona kwamba uzito wa boti usingekuwa tatizo kuzisafirisha kwa barabara na wakakubali boti za Azam zipitie Mombasa kwenda Ziwa Victoria.
Leo hii sidhani kama watu wanakumbuka kwamba uwepo wa hizi boti ziwa Victoria ni busara za Mwandosya.
Na suala jingine linalolingana na hilo ni pale Zambia walipotaka kupeleka mabasi yao marefu (Megabus) Zambia toka bandari ya Dar. Magufuli aliyazuia mabasi haya Kibaha akidai sheria za Tanzania haziruhusu mabasi marefu ya kiwango kile katika barabara zetu. Kwa mara nyingine tena likawa jambo kubwa sana. Magufuli alieleweshwa kwamba haya mabasi yatakuwa transit bila abiria, na hayafikii urefu wa malorikama semitrailers ambazo tunaziruhusu barabarani, lakini akashika msimamo kwamba Wazambia watafute namna nyingine ya kuyapeleka mabasi yao Zambia, sio barabara zetu hata kama hayana abiria yako transit tu. Jambo hili likawa kubwa sana ukizingatia Zambia kutumia bandari yetu, hadi ikabidi ngazi za juu upande wa Zambia na Tanzania ziingilie kati ndipo mabasi yakaruhusiwa kwenda Zambia.
Ndio maana niliwahi kusema, napenda uchapakazi wa Magufuli, lakini katika suala la "rational thinking", mmmh!