Ukweli mgumu ambao nimelazimishwa kuamini

Ukweli mgumu ambao nimelazimishwa kuamini

Ambonyi,

Leo Kama ilivyo Ada ya kila mwisho wa week siku Kama ya leo nilikuwa nimekaa mahali napata tuchupa twangu tuwili tutatu.
Kwa pembeni yangu akaja mzee wangu wa siku nyingi, akanijoin pale tukaendeleza libeneke. Katika kuongea ongea ikaibuka stori nikamuuliza mzee: hivi umewezaje kukaa kwenye ndoa kwa miaka yote hii takribani 40???

Mzee akaniambia, unataka kujua ukweli... Na mm kwa kiherehere changu nikamwambia mwaga.
Mzee akasema

"tatizo lenu nyie vijana mnawafuatilia sana hawa wanawake zenu... Ukishamuoa mwanamke jua umelima miwa karibu na Shule ya msingi, Kama ni wa kupigwa atapigwa tu. Mimi mama yenu naweza kujua kabisa ujinga wake, lakini kwa sababu ananiheshimu na hakudhamiria kunionyesha, najisahaulisha. Kwa hiyo kijana wangu Mkeo atakuwa anapigwa tu na usimfuatilie sana. Waza mambo ya maana."

Alipomaliza Hilo nikanyanyua chupa yangu nikagigida funda la mwisho, nikasimama nikamwangalia mzee nikapukuta miguu nikala kona.

Ukweli mgumu, ila nimeupokea.
Sasa ukamuacha mzee wa watu uliyempa ofa ajilipie na akulipie na wewe kisa tu umeambiwa ukweli mchungu!! Dah!!..
Sio fair kabisa mkuu.
 
naona watu wanaegemea upande mmoja tu, kwani ndoa nibkwa ajilibya mwanamke peke yake? hata mwanaume anawajibu wa kulinda ndoa, na siyo wanawake peke yao ndiyo wasaliti.wanaume wenyewe ndiyo wasaliti wakubwa
 
Wanaume n nyie mmezidi kila kitu mna ongea tu. Ina maana nyie hamchepuki? Tena unakuta mwanaume na lipete lake kubwaaaa kidoleni bado anafuata vibinti hata hajisikii vibaya. Au kwenu kuchepuka ni sawa ila akichepuka mwanamke ndo anapata dhambi. Vitu vingine kabla hamjaongea jiangalieni kwanza na nyie.
 
Nasikia wazee wa zamani wakati wanaporudi nyumbani wakifika karibu na nyumba hujikoholesha mkewe ajue kuwa mumewe amerudi, ili kama mkewe kaingiza mchepuko ndani amtoe kabisa yeye akifika asimkute.

Siku hizi vijana mapenzi wameyafanya ni kama rangi nyeupe,ndiyo maana ikiingia doa kidogo inaonekana na inakuwa tatizo zamani haikuwa hivyo.
 
Nasikia wazee wa zamani wakati wanaporudi nyumbani wakifika karibu na nyumba hujikoholesha mkewe ajue kuwa mumewe amerudi, ili kama mkewe kaingiza mchepuko ndani amtoe kabisa yeye akifika asimkute.

Siku hizi vijana mapenzi wameyafanya ni kama rangi nyeupe,ndiyo maana ikiingia doa kidogo inaonekana na inakuwa tatizo zamani haikuwa hivyo.
Wazee walikuwa wanawatuma watoto wapeleke bakora nyumbani, wakiwa mtaa wa tatu...mama akipokea bakora anaukimbiza mchepuko wake anaiosha anamsubiri mzee.
 
Sisi huku Pwani tunasema:
YALIOMKUTA MAMBA, NA BOKO NAE YATAMKUTA!
 
Back
Top Bottom