Ukweli mgumu ambao nimelazimishwa kuamini

Ukweli mgumu ambao nimelazimishwa kuamini

Ambonyi,

Leo Kama ilivyo Ada ya kila mwisho wa week siku Kama ya leo nilikuwa nimekaa mahali napata tuchupa twangu tuwili tutatu.
Kwa pembeni yangu akaja mzee wangu wa siku nyingi, akanijoin pale tukaendeleza libeneke. Katika kuongea ongea ikaibuka stori nikamuuliza mzee: hivi umewezaje kukaa kwenye ndoa kwa miaka yote hii takribani 40???

Mzee akaniambia, unataka kujua ukweli... Na mm kwa kiherehere changu nikamwambia mwaga.
Mzee akasema

"tatizo lenu nyie vijana mnawafuatilia sana hawa wanawake zenu... Ukishamuoa mwanamke jua umelima miwa karibu na Shule ya msingi, Kama ni wa kupigwa atapigwa tu. Mimi mama yenu naweza kujua kabisa ujinga wake, lakini kwa sababu ananiheshimu na hakudhamiria kunionyesha, najisahaulisha. Kwa hiyo kijana wangu Mkeo atakuwa anapigwa tu na usimfuatilie sana. Waza mambo ya maana."

Alipomaliza Hilo nikanyanyua chupa yangu nikagigida funda la mwisho, nikasimama nikamwangalia mzee nikapukuta miguu nikala kona.

Ukweli mgumu, ila nimeupokea.
Teh teh teh! Kua busy brother
 
Mwanaume anayepoteza muda wa kumchunga mke wake ni mwenye ndoto za kufa maskini haiwezekani upate muda wa kumchunga mke na muda wa kutafuta pesa.
Ishi maisha yasiyo na stress mengine mwachie Mungu Tu
Ila usisahau kuhakikisha nyumbani mkono unaenda kinywani sawa sawa.
 
Ooh fucking bittersweet fact!!!...so hard to swallow but there is the truth in it to some extent...though i don generalize for all ladies!!
 
Mhhh!!!!...ni njia nzuri ila inauma kweli....
 
nikasimama nikamwangalia mzee nikapukuta miguu nikala kona[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Back
Top Bottom