Ukweli mgumu ambao nimelazimishwa kuamini

Ukweli mgumu ambao nimelazimishwa kuamini

Ambonyi,

Leo Kama ilivyo Ada ya kila mwisho wa week siku Kama ya leo nilikuwa nimekaa mahali napata tuchupa twangu tuwili tutatu.
Kwa pembeni yangu akaja mzee wangu wa siku nyingi, akanijoin pale tukaendeleza libeneke. Katika kuongea ongea ikaibuka stori nikamuuliza mzee: hivi umewezaje kukaa kwenye ndoa kwa miaka yote hii takribani 40???

Mzee akaniambia, unataka kujua ukweli... Na mm kwa kiherehere changu nikamwambia mwaga.
Mzee akasema

"tatizo lenu nyie vijana mnawafuatilia sana hawa wanawake zenu... Ukishamuoa mwanamke jua umelima miwa karibu na Shule ya msingi, Kama ni wa kupigwa atapigwa tu. Mimi mama yenu naweza kujua kabisa ujinga wake, lakini kwa sababu ananiheshimu na hakudhamiria kunionyesha, najisahaulisha. Kwa hiyo kijana wangu Mkeo atakuwa anapigwa tu na usimfuatilie sana. Waza mambo ya maana."

Alipomaliza Hilo nikanyanyua chupa yangu nikagigida funda la mwisho, nikasimama nikamwangalia mzee nikapukuta miguu nikala kona.

Ukweli mgumu, ila nimeupokea.
HUkupaswa kuondoka, ulipaswa kuendelea kumdodosa ili afunguke zaidi.
 
Angeniua kwa kisukari,... Yule mzee Hana maana.
Tatizo hamko tayari kuambiwa ukweli. Nakumbuka wakati nimeoa nilikuwa namuwivia sana mke wangu, siku zilipoenda nikaanza kukaa vikao na walonitangulia kuoa wivu ulipungua .. siku hizi sitaki hata kusikia mtu ananambia oh! mkeo kaonekana sehemu fulani kwa sababu ni kuondoleana amani ya ndani na amani ikitoweka hakuna kinachoweza kufanyika kwa ufanisi.
 
Haya mambo hua sitaki hata kuyafikiria, maana yanaweza sababisha mapigo ya moyo yakasimama ghafla.
Na hizi mambo ndio zinazid kunifanya nichukie hii kitu inayo itwa kuoa...[emoji16] [emoji16] [emoji16]
 
Baby beauty girl,kwani wewe unaonaje baby?,nimekuelewa upande mmoja lakini upande wa pili umenimix,hebu kuwa narrative please mamii,nina hamu na uchanganuaji wako coz nakuona kama prominent fulani hivi au?
bahati mbaya sina uchanganuaji zaidi na nilichokiandika.nadhan kinaeleweka vizuri tu. haahhaha
 
Ngumu kumesa hio... Labda kama unampenda toka papuchini na si moyoni
 
Kuwa na uhakika wake zao wanachepuka afu wakachukulia poa tu. Maana wanaume wengi wa sasa hivi, yeye atakuwa hata na michepuko mitatu, ila mke ukichepuka tu ni kwenuuuuu
Hahaha uchepuke uachwe???? Nahisi wazee Wa zamani hawakuwa sawa.
 
Wewe wazee wa zamani walikuwa wanalea hadi watoto ambao wanajua sio wa kwao
Walikuwa na mioyo mashine.
Nadhani ulimwengu umebadilika mno, maisha yamebadilika mnoo... So hata wamama Wa zamani wakikuwa wanakaa kimya wazee wakichepuka??
 
Walikuwa na mioyo mashine.
Nadhani ulimwengu umebadilika mno, maisha yamebadilika mnoo... So hata wamama Wa zamani wakikuwa wanakaa kimya wazee wakichepuka??
Asa zamani mwanamke alikuwa ana la kusema? Wale ndo walikuwa wavumilivu hadi kwenye hakuna
 
Back
Top Bottom