Ukweli mchungu: Ndoa bila watoto sio ndoa

Miss Bunyeta

Member
Feb 22, 2015
70
0
Watoto ni mungu anayepanga..mimi na mama gaude wangu miaka 9 ndoa ndoano hakuna wAtoto wala nini na mahaba moto moto mwanzo kati mwisho..kwanza mitoto inasumbua tu kuja kuanza kuvunja simu zangu buree.aaagh

nimecheka hadi basi utafkr mazuri kha
 

kabanga

JF-Expert Member
Dec 12, 2011
36,873
2,000
ndio maana maadili yanazidi kupungua, sabau ya hawa wanaoshinikiza uzinzi....
 

dreams

Member
Feb 13, 2015
11
20
Nafikiri unapotosha jamii ukisema WAMECHOROPOA, WAMECHEZEA UJANA WAO wako wanaochoropoa usiku na mchana na bado wanazaa, wangine wanafungwa vizazi bado wanazaaa! msituhukumu tusiozaa, ni majaliwa! aliyewapa nyie hao watoto ndiye aliyetukosesha sisi!

Nenda shule upya ukajifunze maana ya "NDOA" ... naona uliondoka kabla darasa halijakamilika. Hope hujaoa/kuolewa, ukioa/olewa mahari ikatolewa ukavalisha/wa pete, ukaenda kanisani/msikitini ndo utajua kama unaoa kwa ajili ya watoto ama kwa ajili yako mwenyewe ... watoto ni zawadi ya ndoa kutoka kwa MUNGU as well as temporary assignment for your marriage, Ndoa ya zote ni muunganiko wa hiyari wa watu wawili na MUNGU wao, watoto wenyewe watakuona chizi kama unawapenda sana wao kuliko Mama/Baba yao.

Tafuta amani na mwenza wako, mpende Mume/Mke wako unconditionally, pendaneni unconditionally halafu utaona jinsi maisha yalivyo matamu hata kama hamna hao watoto unaowazungumzia.

NB:Nina ndoa bila mtoto, muda ukifika watakuja but kwa sasa nafikiri bado tunahitaji kuwa wawili kwanza.

(Ni mtazamo binafsi)
 

50thebe

JF-Expert Member
Mar 10, 2011
2,886
2,000
Tuachane na masuala ya Dini inasema...hapa tunazungumzia hali halisi.

Hali halisi ni matokeo ya chanzo fulani. Zipo historia ndani ya vitabu vitakatifu zinazoelezea maisha ha ndoa bila watoto. Zipo tafiti za kisayansi na kijamii zinazojadili suala hili vizuri tu. Hivyo, uhalisia unaouzungumzia hauwezi kuepuka historia ama uzoefu.
 

McDonaldJr

JF-Expert Member
Sep 25, 2013
6,390
2,000
Mungu akinijaalia mtoto kwenye ndoa yangu nitasema shukrani na nisipopata mtoto nitasema shukrani pia maana kama siijui kesho yangu kwa nini nilaumu kwa kukosa mtoto kuna mambo yapo juu ya uwezo wa binadamu na ukifikiria sana unakufuru.
 

Babeake

JF-Expert Member
Aug 28, 2014
456
250
Duh! ukweli huu ni mchungu sana. Nina dada yangu kaolewa na mume kwa miaka kadhaa hawajapata mtoto walipoanza kwenda hospitali kupima kote walikotembea imeonekana mwanaume hana uwezo wa kupata mtoto kabisaaa! Sasa dada yetu ambaki njia panda! Na sisi hatuna cha kumshauri tumewaachia wenyewe!

hata mimi nina ndugu yangu wana hii kesi jamani.......
 

mrsleo

JF-Expert Member
Jan 13, 2014
2,524
2,000
Kama msingi wa ndoa bora na yenye furaha ni watoto mbona kuna wanawake wengi sana wananyanyasika na hata kutelekezwa wakati wamezaa tena watoto wa kutosha tu?

Tena unakuta mwanaume katelekeza mama na watoto amehamia kwenye nyumba ndogo yuko bize kutunza watoto wa mwanaume mwenzie au hakuna hata watoto huko aliko lakini anasau kabisa ana hatunzi hata hao watoto wake.

yani kesi hizo ni nyingi tunazisikia kila leo, na usiwadanganye wenzio kuzaa kabla ya ndoa, manake kuna single mothers kibao dunia ya leo na wengi wao walijilengesha wakazaa wakazani wataolewa lakini mwisho wake wameishia kuachwa na wanaume hawataki hata kukumbuka kama kuna mahali alizaa
 

mrsleo

JF-Expert Member
Jan 13, 2014
2,524
2,000
mungu akinijaalia mtoto kwenye ndoa yangu nitasema shukrani na nisipopata mtoto nitasema shukrani pia maana kama siijui kesho yangu kwa nini nilaumu kwa kukosa mtoto kuna mambo yapo juu ya uwezo wa binadamu na ukifikiria sana unakufuru.

nimekupenda bure
 

MZEE RAZA

JF-Expert Member
Feb 19, 2015
2,718
2,000
Mtoa mada kajipange upya

Kwanza hakuba ukweli katika ukweli wako mchungu unaosema

Itbis only a call of nature kwamba watoto wanapatikana iwe nje au ndani ya ndoa

Kusudio la.kwanza la.ndoa sio watoto bali ni mwanamke na mwanaume waambatane wawe mwili mmoja.....watoto ni zawadi tu

Kwa hiyo kwa wenye ndoa ambao hawana watoto wasikwazike ni kwamba Mungu hajaamua kuwapa zawadi hiyo.

NB nina ndoa na nina watoto

Umenifurahisha kwenye NB hapo,umemaliza vema kabisa mkuu!!!
 

nyumba kubwa

JF-Expert Member
Oct 8, 2010
10,313
2,000
Asikwambie mtu...mtoto si nguo...
Japo apangae ni Mungu...

Familia iso na watoto in mtihani mkubwa sana
 

MZEE RAZA

JF-Expert Member
Feb 19, 2015
2,718
2,000
Ni nadra sana other wise kulikuwa na "ushirikina" ndani yake wa kumfunga mmoja asizae hasa mwanamke, Nakumbuka kijijini kwetu kuna dada aliambiwa na shangazi yake wewe hutakuja kuzaa wewe..na kweli yule dada kila aliko olewa hakubahatika kupata mtoto mpaka anafariki.

daaaah!!!inauma sana aisee!!!
 

MZEE RAZA

JF-Expert Member
Feb 19, 2015
2,718
2,000
Watoto ni mungu anayepanga..mimi na mama gaude wangu miaka 9 ndoa ndoano hakuna wAtoto wala nini na mahaba moto moto mwanzo kati mwisho..kwanza mitoto inasumbua tu kuja kuanza kuvunja simu zangu buree.aaagh

hahahaha!!!!upo serious mkuu au unatania??
 

MarianaTrench

JF-Expert Member
Dec 29, 2014
1,214
2,000
Mtoa mada wewe ni agenti (sijui ndio inavyoandikwa) wa shetani kabisa...unachochea uzinzi. Tuseme ukweli watoto wa ndani ya ndoa ni baraka saaana. Sijasema wa nje ni laana. Utubu kabisa...watoto ni Mungu anatoa kwa taarifa yako...usijigambe ni kwa neema tu.
 

The Businessman

JF-Expert Member
Jan 9, 2014
7,412
2,000
Mtoa mada wewe ni agenti (sijui ndio inavyoandikwa) wa shetani kabisa...unachochea uzinzi. Tuseme ukweli watoto wa ndani ya ndoa ni baraka saaana. Sijasema wa nje ni laana. Utubu kabisa...watoto ni Mungu anatoa kwa taarifa yako...usijigambe ni kwa neema tu.

Ubarikiwe na bwana, Ila ni kwa mujibu wa dini yako sio yangu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom