Mkodoleaji
JF-Expert Member
- Apr 27, 2008
- 458
- 138
Kuna siku nilikuwa na rafiki zangu wawili kutoka Kanada. Mmoja ameshawahi kuja Tanzania mara nyingi sana hivyo anaifahamu hii nchi na mwingine ilikuwa ndiyo mara yake ya kwanza. Sasa katika mazungumzo ikafikia mahali tukaongelea siasa za Afrika. Moja ya hoja ilikuwa mgawanyiko wa nchi zile zinazoongea kiingereza (anglophone) na zile zinazoongea kifaransa (francophone). Katika hiyo hoja mimi nilikuwa naeleza tofauti iliyopo kati ya nchi zetu (ikiwamo Tanzania) ambazo ni anglophone na francophone. Yule ambaye ilikuwa ni mara yake ya kwanza kuja alikuwa ananisikiliza kwa makini sana wakati yule mwingine alikuwa ananiangalia kwa jicho la wasiwasi kidogo. Nilipomwuliza kwa nini, aliniambia kuwa Tanzania siyo english speaking country bali ni swahili speaking country. Tukacheka yakaisha.
Jana wakati wa uchaguzi wa wabunge wa Afrika Mashariki niliona jinsi wagombea na waulizaji maswali walivyokuwa wanapata taabu basi nikamkumbuka huyo rafiki yangu. Sasa nikawa najiuliza hivi sisi watanzania tuna nini? Kwa sababu tunajua kuwa kiingereza ni lugha muhimu basi tunalazimishana kila mahali? Hivi hao jamaa hata kama wangekuwa wanaweza kutema yai, je wananchi wao wanaweza hiyo kiasi gani? Na kama mikataba ya afrika mashariki inaandikwa kwa kiingereza kwa nini tunakubali wakati tunajua wananchi wetu wengi hawaijui hiyo lugha? Nimejiuliza maswali mengi lakini mwishowe nikafikia hitimisho kama lile la kwenye maongezi na rafiki zangu wale kwamba wengi tunataka nchi yetu iwe english speaking country lakini ukweli ni swahili speaking country. Hivi jenga picha kama lile bunge letu wangesema kuanzia leo mijadala yote ni kiingereza ingekuwaje.
Nawasilisha