Ukweli kuhusu wimbo wa Malaika

Ukweli kuhusu wimbo wa Malaika

nemulo

JF-Expert Member
Joined
May 5, 2014
Posts
1,589
Reaction score
441
Habarini wadau,

Leo nimekumbuka hili na kuona sii vibaya tukashare:

Wimbo wa "Malaika" ni wimbo unaofahamika sanaaa sio Afrika tu bali hata katika mabara mengine,nakumbuka mwaka 2011 nikiwa chuoni walikuja wanafunzi kutoka Asia na waliusikia huo wimbo kwenye laptop ya mtu na mmojawapo (mkorea) aliweza kuuimba nusu na kuonesha kuupenda sana.

Mwaka huo huo mwishoni nikiwa nasikiliza kipindi cha miziki ya zamani na historia zake nilisikia kuwa wimbo wa malaika ulitungwa na kuimbwa kwa mara ya kwanza kabisa mkoani Arusha(eneo la kaloleni ya leo) kabla kabisa ya uhuru,nilitafituli zaidi kwa kuwauliza baadhi ya wazee wapenda miziki nikaambiwa huu wimbo uliimbwa na kijana aliyekuwa akichunga mbuzi karibu na maghorofa ya wahindi kipindi hicho kumwimbia binti mmoja mwenye asili ya Asia,na kurekodiwa na binti huyo kwenye redio yake ndogo.

Baada ya hapo binti yule alikuwa na uhusiano na kijana yule Ila uhusiano wao ulikatishwa na wazazi pamoja na ndugu wa binti.Binti yule alihifadhi ile rekodi ya wimbo na kuja kuirudisha kwa muimbaji naye akawapa baadhi ya watu,

Baada ya hapo studio za kwanza kabisa Arusha kama Radio Habari Maalum(RHM) zikaanza kuupiga wimbo huo pamoja na kwaya za mwanzoni na kukubalika sana.

Leo hii wimbo huu bado ni maarufu sana na ulirudiwa kuimbwa na mwimbaji maarufu Miriam Makeba (Mama Afrika) na wengine. Binafsi naupenda huu wimbo.
 
Mtunzi wa asili wa wimbo wa malaika anadaiwa kuwa ni Fadhili William Mdawida wa Kenya na kuna wakati kulishawahi kuwa na mzozo juu ya hasa mwenye haki na huu wimbo. - Labda hiyo rekodi unayozugumzia ilitua mikononi mwa huyu bwana!!!
 
Inawezekana kwasababu watz wenye vipaji walikuwepo tokea zamani ila tatizo lilikuwa recodings na studios na ndio maana hata Les wanyika ingawa ni watz walihamia Kenya na kurkodi huko na hata baadhi ya wakongo walikuwa wanarekodia nyimbo zao Nairobi miaka hiyo.
 
Huu wimbo ulitungwa Moshi mkoani kilimanjaro.Alitungiwa dada mmoja wa kichagga kutoka Lyamungo...alikuwa mzuri kwelikweli na mtungaji alikuwa akitumia box gitaa..hii ilikuwa miaka ya hamsini.Baadae huyu dada aliolewa na Muhindi na kuzaa binti akaitwa Sugra.Huyu akajaolewa na bwana wa kihindi akiitwa Aslam alikuwa ni Rally driver na owner wa Aslam Garage.Mama sugra aliachika na kuolewa arusha na mzee mmoja akiitwa Saidi Larusai...alikuwa hakimu.Huyu Mzee ni miongoni mwa wazee ma alwatan wa Arusha..sasa hivi wote hao ni marehemu..Mama sugra..mtoto wake sugra..Aslam..na Mzee Saidi Larusai.Inasemakana huyu mama alikuwa mzuri saana na mwenye tabia ya upendo Mwenyezimungu amrehemu.
 
Mtunzi wa asili wa wimbo wa malaika anadaiwa kuwa ni Fadhili William Mdawida wa Kenya na kuna wakati kulishawahi kuwa na mzozo juu ya hasa mwenye haki na huu wimbo. - Labda hiyo rekodi unayozugumzia ilitua mikononi mwa huyu bwana!!!

Miriam Makeba mwenyewe anasema aliupata Tanzania ni nyimbo ya kitanzania hata tone pia wakenya wana tone mbovu wakiimba kiswahili wake up dude
 
wakiume jee!??

Bado nafikiri jina la kumpa wa kiume ila lazima liwe la kiswahili, so far nina Amani au Heri naendelea kufikiri mengine.

Malaika ni jina nililonalo kichwani toka miaka mingi. Vp wewe mkuu?
 
Hii nyimbo ilitaka kutolewa tuzo ya nobel ikashindikana
 
Huu wimbo ulitungwa Moshi mkoani kilimanjaro.Alitungiwa dada mmoja wa kichagga kutoka Lyamungo...alikuwa mzuri kwelikweli na mtungaji alikuwa akitumia box gitaa..hii ilikuwa miaka ya hamsini.Baadae huyu dada aliolewa na Muhindi na kuzaa binti akaitwa Sugra.Huyu akajaolewa na bwana wa kihindi akiitwa Aslam alikuwa ni Rally driver na owner wa Aslam Garage.Mama sugra aliachika na kuolewa arusha na mzee mmoja akiitwa Saidi Larusai...alikuwa hakimu.Huyu Mzee ni miongoni mwa wazee ma alwatan wa Arusha..sasa hivi wote hao ni marehemu..Mama sugra..mtoto wake sugra..Aslam..na Mzee Saidi Larusai.Inasemakana huyu mama alikuwa mzuri saana na mwenye tabia ya upendo Mwenyezimungu amrehemu.

Wachaga mna mambo hata chadema ilianzia kwa mromboo
 
CHADEMA ilianzia kwa Sangisi kwenye shamba la kahawa linalomilikiwa na Mzee Mtei.hapa ni kama mita 500 kufika tengeru...arusha
 
Huu wimbo ulitungwa Moshi mkoani kilimanjaro.Alitungiwa dada mmoja wa kichagga kutoka Lyamungo...alikuwa mzuri kwelikweli na mtungaji alikuwa akitumia box gitaa..hii ilikuwa miaka ya hamsini.Baadae huyu dada aliolewa na Muhindi na kuzaa binti akaitwa Sugra.Huyu akajaolewa na bwana wa kihindi akiitwa Aslam alikuwa ni Rally driver na owner wa Aslam Garage.Mama sugra aliachika na kuolewa arusha na mzee mmoja akiitwa Saidi Larusai...alikuwa hakimu.Huyu Mzee ni miongoni mwa wazee ma alwatan wa Arusha..sasa hivi wote hao ni marehemu..Mama sugra..mtoto wake sugra..Aslam..na Mzee Saidi Larusai.Inasemakana huyu mama alikuwa mzuri saana na mwenye tabia ya upendo Mwenyezimungu amrehemu.

Sio kweli,labda kama ulifika moshi mapema,ulitungiwa Arusha miaka mingi na mtunzi alitumia a very primitive zeze alilokuwa anatumia akiwa machungani...uliza wazee wa zamani.
 
Naomba mnisaidie kujua jina la wimbo wa aei afrika u naopigwa radio DW wanapokuwa wanasoma Habari za Africa...naupenda sana ila sijui muimbaji...
 
Mtunzi ni Adam Salim alikuwa ni Mtanzania aileishi Nairobi, na alikuwa ni mechanics wa magari alimuimbia Halima mnamo mwaka 1945-46
 
Authorship of the popular song is usually
credited to Kenyan musician Fadhili William ,
though this is disputed.
Some sources claim that the song was written
by Tanzanian songwriter Adam Salim while he
was living in Nairobi in 1945-46. According
to this story: "Malaika was composed by a
mechanic called Adam Salim of Nairobi (born
1916).
MIRIAM MAKEBA 1974
She introduced the song
as having come from
Tanzania. Miriam Makeba's early recording helped make it famous throughout the continent and eventually the world. Her performances of the
song brought it to the attention of such
famous names as Harry Belafonte, Pete Seeger , Boney M , Usha Uthup and Angélique Kidjo
 
Back
Top Bottom