Ukweli kuhusu Wema Sepetu kukutwa na Msokoto wa Bangi.

Zero Hours

JF-Expert Member
Apr 1, 2011
12,943
18,665
Ndugu zangu nina maswali najiuliza juu ya hii saga ya huyu nyota Wema Sepetu kukutwa na msokoto wa bangi.

Nakumbuka kuwa Wema aliitwa kituoni kujibu tuhuma zake za kuhusishwa na madawa ya kulevya. Yeye pamoja ma wenzake waliwekwa ndani na baadaye kwenda kupekuliwa majumbani kwao.

Baada ya kupekuliwa hakukuwa na habari yoyote kuwa Wema alikutwa na Msokoto wa bangi. Tena katika ile audio aliyerecordiwa wema alisema kuwa walimpekuwa ila hawakumkuta na chochote.

Hii audio ili trend sana mitandaoni na baada ya siku ndipo Sirro aliitisha waandishi wa habari na kusema kuwa wema alikutwa na msokoto wa bangi.

Mimi hapa nashindwa kuelewa. Huu msokoto waliukuta kipindi kile wameenda kuwapekua mara ya kwanza au walirudi tena kumpekua wema ndyo wakaukuta?

Hivi ile list ya siku ya pili ambayo waliitwa wakina Tunda je na wao walienda kupekuliwa au walikuwa wamemlenga kumpekuwa mtu flani tu?
Ningepeta pia hujua kisheria. Hivi mtu ukikutwa na msokoto wa bangi hukumu yake inakuaje? Je huwa anapewa dhamana?
 
Kosa la kukutwa na bangi linayo dhamana.Sema la kukutwa na madawa ya kulevya hilo halina dhamana.Sema hii ishu imetengenezwa kuna watu wamelengwa kuchafuliwa.
 
Yawezekana walimwekea iyo bangi ili kumkomoa kwakuvujisha siri ya hawara ya arasii makongo.
Kamanda siro ameamua kutumika na kitoto ambacho anaweza kukizaa.
Kutumikia tumbo kubaya sana.
 
Tusitoke kwenye mada. Nilichoona kwa upande wangu. Kwanza alitajwa kwamba anavuta akaomba apimwe damu na mkojo wakikuta chembe chembe wamfunge. Wakambadilishia case kwamba punda. Nayenyewe wakakosa ushahid Wakambadilishia case yamatusi.
 
Hivi kati ya watu wote hao waliotajwa, nadhani watakuwa 100+. Je, kunaushahidi uliokamatwa hata 1kg kwa baadhi ya hao watu?
 
Tusitoke kwenye mada. Nilichoona kwa upande wangu. Kwanza alitajwa kwamba anavuta akaomba apimwe damu na mkojo wakikuta chembe chembe wamfunge. Wakambadilishia case kwamba punda. Nayenyewe wakakosa ushahid Wakambadilishia case yamatusi.
Subiri tarehe 22 mwezi huu majibu ya mkemia mkuu wa serikali baada ya vipimo tujue
 
Haya maswali uliyouliza yote majibu yake yanajulikana, subiri tu viingilio vikishakusanywa na 'ukumbi ukajaa' hata mabaunsa hawatakaa milangoni! Umesikia eh!?
 
Ndugu zangu nina maswali najiuliza juu ya hii saga ya huyu nyota Wema Sepetu kukutwa na msokoto wa bangi.

Nakumbuka kuwa Wema aliitwa kituoni kujibu tuhuma zake za kuhusishwa na madawa ya kulevya. Yeye pamoja ma wenzake waliwekwa ndani na baadaye kwenda kupekuliwa majumbani kwao. Baada ya kupekuliwa hakukuwa na habari yoyote kuwa Wema alikutwa na Msokoto wa bangi.
Tena katika ile audio aliyerecordiwa wema alisema kuwa walimpekuwa ila hawakumkuta na chochote.
Hii audio ili trend sana mitandaoni na baada ya siku ndipo Sirro aliitisha waandishi wa habari na kusema kuwa wema alikutwa na msokoto wa bangi.

Mimi hapa nashindwa kuelewa. Huu msokoto waliukuta kipindi kile wameenda kuwapekua mara ya kwanza au walirudi tena kumpekua wema ndyo wakaukuta?

Hivi ile list ya siku ya pili ambayo waliitwa wakina Tunda je na wao walienda kupekuliwa au walikuwa wamemlenga kumpekuwa mtu flani tu?

Ningepeta pia hujua kisheria. Hivi mtu ukikutwa na msokoto wa bangi hukumu yake inakuaje? Je huwa anapewa dhamana?
huyu alibambikiwa ..hawa jamaa unawajua vizuri kweli?
 
wamchafue wema kwa lipi? na kwa maisha gan? c bora hata zari
Mimi hata huyo zari simjui, umaarufu wa mtu unatokana na followers wake na ndio maana magazrti ya udaku yananunuliwa zaidi ya yenye serious contents. Siku ukienda kwenye ofisi ya mtu unayedhani ni mkubwa na ukakuta nakala za ijumaa na risasi huku the citizen hata ya mwaka juzi haimo ndio utajua kuwa hawa watu 'wanajuana'!
 
Tusitoke kwenye mada. Nilichoona kwa upande wangu. Kwanza alitajwa kwamba anavuta akaomba apimwe damu na mkojo wakikuta chembe chembe wamfunge. Wakambadilishia case kwamba punda. Nayenyewe wakakosa ushahid Wakambadilishia case yamatusi.
Hakuna sheria ya kumfunga mtumiaji
 
Back
Top Bottom