Ukweli kuhusu v2 wa wimbo :nasonga mbele"

Ukweli kuhusu v2 wa wimbo :nasonga mbele"

Ashampoo burning

JF-Expert Member
Joined
May 12, 2023
Posts
1,296
Reaction score
3,929

View: https://youtu.be/dmc-xxRof60?si=AQyC2o1xsr_iCO7m


Bro hebu kaa chini tusimuliane hii ishu ya zamani lakini bado inabamba hadi leo. Kama uliishi enzi za Bongo Flava halisi, lazima utakumbuka ule wimbo mkali wa “Nasonga Mbele” kutoka kwa V2 – mrembo mwenye sauti ya dhahabu aliyewatoa machozi wengi kipindi hicho.

Ngoma hiyo iliachiwa rasmi mwaka 2000, ikirekodiwa kwenye studio ya Heart Beat kule Zanzibar, chini ya mikono ya Producer Babu Chuchu – mzee wa kuchanganya emotions na beats kama mapenzi ya first love.

Sasa stori yenyewe kwenye wimbo ilikua moto – mwanamke amechoka na boyfriend wake anayependa michepuko, hajali tena, hana nidhamu ya mapenzi. V2 akamwaga ukweli, akasema:

“Nasonga mbele… sitaki tena kurudi nyuma!”
Maneno hayo yaligusa wengi, hasa mabinti waliowahi kuumizwa.



Lakini bro, mambo yakabadilika. Miaka ilivyopita, mitandao ikaanza kueneza taarifa za kusikitisha – eti V2 alifariki kwa UKIMWI, na video king wa ile ngoma, Ahmada, naye kafa. Mashabiki tukabaki midomo wazi, roho zikatetemeka.

Mimi binafsi nikasema hapana – lazima nifuatilie. Nikaingia deep kwenye mitandao, page za muziki, mashabiki wa zamani… bro nikagundua kitu kikubwa:
V2 YUPO HAI!
Na zaidi ya hapo – ameolewa na mwanaume kutoka Sudan Kusini, wana familia yao, na wanaishi maisha ya furaha. Niliona picha zake, updates, bro nilijikuta natabasamu kama nimepokea salamu za ex wangu ambaye nilidhani alishahama dunia 😅

Pia, kuna tetesi zilizosambaa mitandaoni kuwa V2 aliwahi kuwa na mahusiano ya karibu na Joseph Kusaga, mmiliki wa Clouds Media Group. Hii haijathibitishwa rasmi, lakini majina hayo mawili yamewahi kutajwa sana kwenye forums za zamani. Unajua mitaa haikosi chai 🫖

Cha maana ni kwamba, V2 bado ni legend, na wimbo wake “Nasonga Mbele” umekuwa classic – ngoma ya milele, si ya msimu. Aliimba kwa hisia, akaacha alama kwenye historia ya Bongo Flava.


--- instagram yake hii bonyeza hapa ukamuone v2 Login • Instagram

🔥 Nasonga mbele, nasonga mbele... 🔥

Kama uliwahi kupenda huu wimbo, share story hii!
V2 ni kumbukumbu ya dhahabu kwenye game ya muziki – na bado anang’aa kama zamani.

Screenshot_20250629-055741_Instagram.jpg
 
Back
Top Bottom