Ukweli kuhusu Udsm huu hapa

Hii dhana tuliyonayo watanzania ya kulalamika kwa kila jambo sio nzuri kabisa inajenga tabia ya kutofikiri nje boksi itaturudisha sana nyuma kimaendeleo kijana soma kwa manufaa yako na taifa kwa ujumla usiangalie nani amesomaje na amepataje Fanya sehemu yako mbona wengine wanafaulu
 
Kiasi cha kufeli kimeiongezeka na disco ni nyingi kuliko miaka ya zamani na waalimu wanalalamika kua wanafunzi wa sasa hatujibu mitihani kwa viwango vya standard level of perfomance
 
Mbona mim nimesoma miaka minne udsm chemical engineerng na cjawah sup wala kudisco. Mi naona elimu ya yakawaida tu . Na mara nying ukifundishwa na masterz holder uwa wanasupisha tofaut na phd na prof.
 
sasa jembe.. ulitegemea kuona idadi ndogo ya supp na disco kwa sababu watu wanasoma sana na kupiga discussion nyingi na practice? haipo hivyo, kusoma ni kuelewa mtu wangu, unaweza kuona mtu amekaa na daftari masaa mawili lakini hakuna kinachoingia wala kinachotoka.. fanya kautafiti, wengi wanaopata "A" hawana mbwembwe.
 
Manzi sina sapu na napiga book ila nachosema ni kua chuo chetu ni bora tz wanavodai ila sa mbona sap na disc nyingi
 
Mimi ni mwana udsm.Nimeishi na ni mwaka wa3 hapa,Ni kweli chuo chetu kina sifa ambayo ni ya zamani ila kwa sasa mabadiliko yanahitajika mana Saplimentary ni nyingi sana afu tunadai sisi ni bora.Watu 500walidisco campus zote mwaka juzi, na watu wanasoma sana lakini bado matokeo ni ya kawaida sana.Malalamiko ya mitihani kua migumu ni wimbo wa kila siku,na kama elimu yetu ni bora yote haya yanini?

Usitake kufanya elimu kama wimbo wa
♪♪oya msela oya♪♪
 
Unajua Elimu ya nchi yetu inashuka kuanzia primary hadi higher learning
 
ni bora kwa sababu wanaostahili SUP wanapata sup, wanaostahili honours wanapata honours. bila TCU yaonekana we ni mmoja wa wale ambao UDSM si saizi yao.
 
Endelea kusifia chuo bora chuo bora, mambo ya kishamba kabisa hayo. Ubora wa chuo ni mtu mwenyewe wala si chuo. Hawa mawaziri mizigo na makatibu wakuu mizigo unajua wamesoma chuo gani? Udom au Saut? Si ndio upime ubora unao usema wewe wa majengo, idadi ya maprofesa au uelewa wa products?
 
TCU imeua sifa ya UDSM.sasa ni kama vyuo vingine vya kata tu.

Ndiyo mkuu unachokiongea ni sahihi kabisa, kuna mabadiliko makubwa sana ya wanafunzi wanaoingia Udsm miaka hii tangu TCU wachukue nafasi ya kuchagua wanafunzi.

Miaka ya nyuma kidogo Udsm walikuwa na cuts point zao ambazo kwa kweli ni wanafunzi wachache walikuwa wakifeli. Sasa hivi wanafunzi wanapelekwa wengine wakiwa na point ndogo sana. Ni wachache sana wenye point hizo wanaoweza kukop na mchakamchaka wa hapo na ukizingatia chuoni hamna tuition kwa wale shake well before use.

Pia hili suala la millenium goal limefifisha elimu kwenye nchi nyingi za afrika. Hii inatokana na wanasiasa kuangalia ongezeko la shule na vyuo na idadi ya wanafunzi bila kujali nyenzo nyinginezo zitakazoweza kuhakikisha kuongezeka kwa shule na wanafunzi kunaenda sambamba na ukuaji wa elimu.
 
Sawa Tcu inachagua sawa ila vuo vingine kama Mzumbe wanachaguliwa na Tcu na wapo vizuri
 
Mimi ni mwana udsm.Nimeishi na ni mwaka wa3 hapa,Ni kweli chuo chetu kina sifa ambayo ni ya zamani ila kwa sasa mabadiliko yanahitajika mana Saplimentary ni nyingi sana afu tunadai sisi ni bora.Watu 500walidisco campus zote mwaka juzi, na watu wanasoma sana lakini bado matokeo ni ya kawaida sana.Malalamiko ya mitihani kua migumu ni wimbo wa kila siku,na kama elimu yetu ni bora yote haya yanini?

mkuu ulivyojielezea kwa mbwembwe utadhani uko main campus???? ungeverify tu MUCE (MKWAWA UNIVERSITY COLLEGE OF EDUCATION)...
 
Back
Top Bottom