Ukweli Kuhusu UDOM huu hapa

Chunguza waliotoa thanks kwa mleta topic.
Kwanza wamepinga hapohapo wamekubaliana.
Kizungumkuti.
 
Hivi mnatumia methodology gani kujua dini ya mtu?
unamwangalia usoni? au unaangalia jina lake au mnafanyaje wandugu?


Hata mie sielewi, nimeenda kwenye website nimeona majina tu sijaona DINI!!!!!!!!

Hawa watakuwa ni wanafunzi wa Sheikh Yahaya, wanaTABIRI.
 
Afadhali yangu mimi ambaye sina Dini kabisa maana kila siku Dini tu why you guy
 

Wale wale


Mkuu hapa umenena. Kwa muda mrefu sasa jamiiforums imeanza kupoteza dira kutokana na mijadala mbalimbali kuhodhiwa na mantiki, utashi na matusi ya udini. Imetoka wapi hii? Kuna baadhi ya mijadala ya maana inaanzishwa na haipiti muda kidogo wanatokea wanabaraza fulani wanaofahamika vyema na kuleta "hoja" zao zilizotopea chuki, dharau na za uchochezi ambazo hazina mchango wowote chanya katika majadiliano kwenye baraza kama hili.

Hivi humu jamvini kuna moderators? Basi naombeni mfanye kazi na kuwajibika, kuna "michango" mingi ya kubomoa kuliko kujenga. Msitumie malengo ya jamiiforums ya kuchochea na kuimarisha matumizi ya haki za msingi za binadamu kama sababu ya kufumbia macho hawa wachangiaji na "michango" yao. Pamoja na kwamba kila mtu ana uhuru na haki ya kusema, moderators tafadhali simameni imara kuhakikisha baadhi hawapotoshi maana halisi ya uhuru huu kwa kuutumia bila ya uwajibikaji. Baadhi ya hii "michango" ya hawa wanabaraza haifai hata kuwa katika jukwaa la dini humu ndani, maana ni kashfa kwa jamii ya wastaarabu na watanzania kwa ujumla.



Jamani tuache kujaribu kuchafua watu, hivi Prof. Kikula unamfahamu vizuri? Sio kila mwenye imani tofauti na mimi na wewe ana malengo hasi na sisi.
 
Hizi dini zinachosha wajomba,haya mambo ya kupendeleana kwa ajiri ya dini au ukabila yapo sana TZ,yaaani kweli sielewi kabisa ndio maana sina hata cha kuandika naona michosho tuu!
 

Hongera kwa kuwapa elimu watanzania waachane na majungu wachape kazi kujenga taifa letu
 
Waungwana Habari za udini hazifai kutajwa na kujadiliwa na jamii ya watu makini kinachotakiwa ni kueleza mapungufu ya mtu fulani mwenye cheo fulani kwani upungufu au uimara wa mtu hauletwi na dini ila ni mtu mwenyewe.

Tukianza na dini tutaelekea kwenye kabila then tumalizie na jinsia.
 
huko tuendako, tukifanikiwa kuushinda ufisadi, tutasambaratishwa na udini
 
Wanafunzi - Christians 92%
- Muslim 8%

Jamani mambo mengine kweli yanachekesha,hivi hamjui kwamba mtu anaweza kuwa na jina la dini fulani lakini si wa dini ile?
halafu katika swala la admission ya wanachuo kama wakristo kwa mfano hawaja-apply utawalazimisha kuwapa admission ili tu uwiano uwe sawa?
na hata kama wame-apply na grade zao ziko chini,utawapa admission kwa kulazimisha ili kuogopa watu wa dini moja wasizidi.
Labda nieleweshwe au kuna watu maalumu hapo UDOM wanabania watu wa dini fulani wasipate nafasi hata kama wana sifa?

Vinginevyo ianzishwe programme maalumu ya pre-entry kama ya UD ya wanawake wasiokidhi viwango vya direct entry,ili kuwepo na uwiano wa dini pia.
 

Mdini ni wewe! unakerwa na uislamu na post zako zimesheheni chuki dhidi ya uislam.

Hebu isome tena post yako uone ulivyo mdini, kwa akili yako kuwa na waislam 3 uongozi wa juu ni udini (isomeke uislamu) sasa je na hivyo vyuo vingine vilivyobaki ambavyo sio tu viongozi watatu wa juu ni wakristo bali WOTE ni wakristo huoni udini?

Wewe wafahamika hapa kwa chuki zako kwa waislam na kwako hakuna jema kutoka kwa waislam, lakini dini hii imepingwa na makafiri wakubwa kuliko wewe lakini bado ni dini inayo kuwa kwa kasi kuliko dini zote duniani. Endelea na chuki zako mgalatia wewe
 
Unajua ukisikia kuna UDINI maana yake kuna UISLAMU.

Jana nilikuwa nasoma Thread moja kuhusu Udini NSSF kwa swahiba wangu Dr Ramadhani Dau. Utaona waziri Prof Kapuya, na a lot of bla bla.

Jamani WAKATOLIKI nyie tu ushike kila pahala, wakishika waislam basi Nongwa.

hakika chuki zenu dhidi ya waislamu na Uislam zitaiweka pabaya nchi yenu. Na Uislam hamtauweza hata mkifanya nini, kwani umejengwa kwa misingi madhubuti sana. Tieni kila aina ya fitna lakini uislamu utapaa tu.
 
Mamkwe tunashukuru kubainisha ukweli. Sasa tuleteee data kama hizo za SUA, UCLAS, Muhimbili na UDSM.
tulinganishe na kupata ukweli wa mambo.

Allah akubariki saaaaaaaaana
 
Hoja zingine ziko so light yaani jamani hili nalo la kubishana....nenda kwenye taasisi zote utaona wakristu wengi kuliko waislamu....yaani ni katika hali ya kawaida bila kuhusisha upendeleo.Nchi hii population yetu ya watu kama milioni 40 ina waislamu wengi kuliko wakristu ila wasomi wengi zaidi ni wakristu...kama hutaki shauri yako huu ndo ukweli hasa unaosababisha kuwe na wakristu wengi katika kila sector nchi hii. Kwa hiyo suala hapa ni kwa waislamu kusoma,haitoshi tu kwenda madrasa jamani...tupate na elimu dunia ili tuweze kupata nafasi nyingine za kiutendaji katika serikali yetu.
 
Ukiona watu wanaanza kutumia majukwaa ya dini kuingia katika siasa ujue wamefilisika kisiasa. Vyama vya siasa kuingiza masuala ya dini kwenye ilani zao za uchaguzi ndio chanzo cha haya yote. Viongozi wetu wanatafuta cheap popularuty kwa ku influence makundi fulani katika jamii bila kufikiria kwanza athari zake.

Huu ni sawa na wendawazimu wa kufikiria ni kwa jinsi gani wataendelea kubaki madarakani hata kama ni kwa gharama kubwa kwa jamii na kuhatarisha utengamano wa nchi.

Hisia za kidini zimeletwa na watawala wetu kwani mpaka sasa huwezi kusikia mtu akikemea kwa nguvu na nia moja chokochoko za kidini.
 


kwa kweli haya mambo yanahitaji kutazamwa na kutafutiwa suluhu afisini ukipiga nyimbo za gospel hakuna anaesema fungua quran mdini

ukipanda mabasi ya mikoani utasikia nyimbo za gospel ukifungua quran hapatoshi

hili tuliangalieni sana kama ni kweli tunapenda haki basi utaona wazi kuwa jamii ya wakristo haiwatendei haki waislam na inajaribu kuwafanya waonekane ni class 2 ktk nchi yao
 
Uongo ni kitu kibaya sana especially uongo wa kutunga wenye nia za hila hila. Hata hivyo udini pia ni kitu kibaya sana sana. Tujiangalie tusifikiri tumesimama kumbe ndo tunaanguka. Mambo ya aina hii hayako sustainable kwa individuals na kwa Taifa letu. Tuanze kuangalia dunia yetu kwa jicho pana. Hili la udini na uongo hili litatuangusha wenyewe. Time will tell
 
ki ukweli watanzania sio wadini bali hutumia huo udini kwa manufaa mengine maana ni wachache sana ktk maisha yao ukifuatilia ndio kweli wnafuata hizo dini zao ila wengi ni wahini wahuni na ni watu wa kawaida sana nadhani inafaa sasa tufuate siasa za cuba au communist countries
 
no wonder kila kwenye vita (sehemu nyingi) ni kwasababu ya watu kama nyie... Somalia, boko haram(nigeria), afghanistan, iraq, sudan....

Mnaboa sana na analysis zenu hizi za kidini bila kufikiria nje ya box kwanini inakuwa hivyo.


chuki na udini umekujaa, najua hampendi kuambiwa ukweli hasa pale hila zenu zinapofichuliwa.

Sehemu zote hizo zenye vita ni kwa sababu ya uroho wa wagalatia dhidi ya mali za waislam walizjaaliwa na mola muumba.

Hapa kin achotakiwa ni kujibu hoja kwa hoja sio kushutumu na kutukana kwa sababu tu hoja zilizowasilishwa umeshindwa kuzijibu.

Waleta hoja wakiziwasilisha bila data mnasema uzushi, wakiweka data mnasema analysis zinaboa sasa mnatakaje?????.

Hapo ndo inpodhihirika hila na chuki dhidi ya uislam.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…