Miongoni mwa vitu ambavyo nilijitahidi sana kuichimba sana historia yake ni hivi Vita vya Kagera na hapa kulikuwa na uzi mmoja, ulinoga sana kuhusiana vita hivyo; wachangiaji wakuu nakumbuka tulikuwa ni pamoja na Mkandara, chama, Jasusi, Mzee Mwanakijiji pamoja na wengineo! Nikiri wazi kwamba katika kutafuta tafuta huko nikiri wazi sikuwahi kukutana na ushiriki wa Kagame kwenye vita hiyo!Hayo ni mawazo yako NasDaz ila sio lazima yawe na ukweli ndani yake.Wakati Kagame analipigania hili Taifa yenye historia ya kipekee hapa barani Afrika dhidi ya mchokozi Idd Amin,Mtikila alikuwa wapi?Kagame atabakia kuwa mmoja wa mashujaa wa Tanzania wakati Mtikila atabakia kuwa mtu muoga,Asiye mzalendo na anayetumika na Wanasiasa wasio waadirifu katika Taifa hili la Tanzania.
Lakini hata kama ni kweli kwamba Kagame alipigana upande wa Tanzania, bado siwezi kushawishika kwamba alifanya hivyo kwa maslahi ya Tanzania bali alifanya hivyo kwa maslahi ya Yoweri Museveni ambapo alifahamu kabisa kuondoshwa kwa Iddi Amin kungekuwa ni some steps forward kwa Museveni kuitwaa Uganda na hivyo Kagame kupata eneo muafaka kwake kuendeleza harakati zake!
Kwamba Kagame ni Shujaa wa Tanzania hicho ni kutuko cha kufungia nusu mwaka, na kwa hakika kinaweza kuwa Top 3 ya Vituko Vikubwa kabisa 2013 hapa Tanzania! Suala la yeye kupigana bega kwa bega na Majeshi ya Tanzania kamwe hakutoshelezi kumweka katika kundi la Mashujaa wa Nchi hii...!! Mfano mzuri, miezi michache iliyopita Kenya alipeleka majeshi Somalia kuwapiga Al Shabab iliyokuwa inawatesa sana Somalia! Kwa hili katu hatuwezi kui-brand Kenya kwamba ni Shujaa wa Somalia wakati ukweli unafahamika kwamba Kenya alipeleka majeshi si kwa ajili ya Somalia bali alipeleka majeshi ili kuiangamiza Al Shabab iliyokuwa inaisumbua Kenya! Huo ni mfano wa karibuni kabisa kupata kutokea ukanda huu! Lakini tukiend pande zingine za dunia, tunaona George Bush alipeleka Majeshi Afghanistan ni kuwafukuzia mbali Taliban! Hasilani hapo hatuwezi kuthubutu kusema kwamba George Bush ni Shujaa wa Afghanistan kwa kigezo kwa kuwa ukweli ulio ni wazi ni kwamba hakupeleka Majeshi Afghanistan kwa maslahi ya Afghanistan na watu wake bali alifanya hivyo kwa ajili ya kwenda kumfagia Osama aliyekuwa anaisumbua Marekani yenyewe! Si hivyo tu, Marekani huyo huyo alimsaidia Osama na Taliban kuifukuza Urusi iliyokuwa imeweka Majeshi yake Afghanistani lakini hatuwezi kusema kwamba US ni shujaa wa Afghanistan kwa kuwa alisaidia kuifukuza Urusi ndani ya ardhi ya Afghanistani kwa kuwa inafahamika wazi kwamba US hawakufanya hivyo kwa kuipenda Afghanistan bali walifanya hivyo kwa ajili ya kuondosha ushawishi wa hasimu wake mkuu Urusi kwenye eneo hilo!
Lakini pamoja na kutumia nguvu zote hizi kukuonesha ni namna gani mtu kupigana upande wako si lazima awe anafanya hivyo kwa maslahi yako, bado nasisitiza sijawahi kusikia popote suala la Kagame kuhusika na kuikomboa Tanzania! Weka hapa source ya taarifa yako ili nami nipate kuongeza ufahamu! Historia pekee ninayoifahamu mimi inayofanana fanana na hiyo ni pale Kagame alivyoungana na Museven wakiwa na lengo la kumwangusha Obote (baada ya Obote kurudi Uganda mara ya pili)! Na sababu kubwa ni ile ile niliyoisema hapo kabla; kwamba Kagame alilazimika kumsaidia Museveni ili apate uwanja usio na bughudha wa kuendesha harakati zake!
Last edited by a moderator: