Mi naamini hayo ma-pyramids yamejengwa na wanadamu, tena wanadamu wa kawaida kabisa,
Maana wanefili (majitu) waliangamizwa na waisrael kule caanan, japo zilibakia mbegu chache sana kama yule Goliath mfilisti .
Nani waliojenga na kwanini walijenga?!
Bila shaka pyramids zilijengwa na wamisri (wakale) au waisrael (watumwa wao) kwa kufuatisha elimu na ufundi wa hali ya juu waliokuwa nao enzi hizo!
Walijengaje?!
Mimi naamini sikweli kwamba eti walibeba tofali moja ambalo lina uzito wa tani 2500, bali inawezekana pia hao watu waliojenga enzi hizo walijenga hayo matofali huko huko juu,
Yaani walijenga tofali juu ya tofali lingine wakiyaacha mpaka yakauke, kama vile tunavyojenga linta ya nyumba! Walienda kwa mtindo huo mpaka kumaliza pyramid zima wakifuatisha mahesabu yao na ufundi wao.
Maana tukikazania na kung'ang'ania kwamba eti walibeba tofali la tani 2500 haileti sense, hawakuwa na mitambo (winchi) wala vifaa vya kubebea, wala hawakuwa na nguvu za kuyabeba physical hayo matofali,
Bali kuna uwezekano kuwa yalijengewa huko huko juu kama tunavyojenga linta za nyumba, hilo pia linawezekana, kwanini lisiwezekane??????!!!!!