Jina la mtela Allan mwampamba limeendelea kukua kwa kasi kubwa katika medani za siasa hapa nchini hasa baada ya kijana huyo machachari jukwaani kujiunga na Chama Cha Mapinduzi akitokea chama cha Upinzani Chadema na kuwachachafywa viongozi na wanachama wa chadema kwa kutoa siri zao za ndani na mipango mbalimbali ya uhujumu iliyokuwa ikiandaliwa na chama hicho dhidi ya CCM na Serikali yake.
Wakati wa sokomoko la kusimamishwa akina mwampamba na shonza ndani ya chadema kutokana na kukua na kushamiri kwa makundi ya urais ndani ya chama hiko yakiongozwa na Zitto kabwe dhidi ya Dr Slaa, kiongozi mmoja wa chama cha siasa ambae pia ni mmoja wa wanajamvi maarufu kama tandaleone aliandika kuwaasa chadema juu ya nguvu na uwezo wa vijana hao kutoka kusini mwa Tanzania lakini kama ilivyo kawaida ya uongozi wa chadema hawakusikia nasaha hizo na hatimae sasa maneno ya tandaleone yametimia ambapo vijana Mtela amekuwa kaa la moto linalochoma nyumba ya chadema.
Kwa takribani miezi 6 tangu mtela ajiunge na CCM ameshavujisha mipango zaidi ya 14 iliyokuwa ikiendelea ambayo ilikuwa ya Chadema ya kuihujumu CCM na amekuwa akifanya hivyo katika vikao vya ndani vya CCM na hata katika majukwaa.
Kijana huyo kwa sasa ni mwanachama na mwajiriwa wa UVCCM na leo hii yupo pamoja na wajumbe wengine wa baraza kuu la taifa la UVCCM katika ukumbi wa Ofisi Kuu ya Chama Kisiwandui Zanzibar akimpitisha Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo ya Vijana Ndugu Sixtus Mapunda.
Maisha ya Mtela ndani ya CCM yamekuwa ya faraja na yanayotamaniwa na kijana yeyote mwenye ndoto za kisiasa, mtela amepata fursa ndani ya CCM ambayo aliikosa chadema kwani fursa aliyoipata Mtela CCM kwa chadema inapatikana kwa watoto wa kichaga na wale wanaotoka uchagani tu. (ushahidi wa majina upo ya vijana ambao si waajiriwa wala wanachama vindakindaki wa chadema lakini wanafaidika na fursa ndani ya chadema kwa kuwa tu wanatoka katika maeneo hayo tajwa)
Mtela fanya siasa na simamia kweli hata ikiwa ukweli huo unatishia maisha yako, sisi tutakukumbuka hata baada ya kufikwa na yale wanayopanga yakufike, Tanzania ijayo itakukumbuka na Dunia itakukumbuka.