Mkuu Kimbunga,
Nakubaliana na mtazamo wako kwamba Mihangwa anaweza kuwa na ukweli mwingi. Nilisoma simulizi ya Ahmed Rajab nikakuta ina matobo mengi sana (dots nyingi sana hazijaungana). Mihangwa ametumia reference za vitabu vya simulizi za akina Sheikh Thabit Kombo ili ku-justify simulizi zake, Bwana Ahmed Rajab naona anatupa stori tu ambazo hazina support yoyote.
Nikisoma simulizi ya Ahmed Rajab, ninakuta kuna mapengo mengi na pia kuna maswali mengi. Kama Okello alikuwa "insignificant" kwenye hayo mapinduzi, ilikuwaje akaenda Dar kukutana na Mwalimu? Alipokelewa na Mwalimu akiwa kama nani? Kwamba eti aliyetakiwa kutangaza aligoma/ogopa, then ndipo Okello akaamua kwenda kutangaza kwa kuwa alikuwa na sauti ya kutisha na lafudhi ya ajabu ajabu ndio aachwe na kupewa heshima ya kwenda kukutana na Mwalimu, akiwa kama nani? Mwisho kabisa, kama Okello alikuwa insignificant, kwanini serikali iingie gharama ya kumpeleka Kenya peke yake kwenye ndege kubwa? Ni kipi ambacho serikali ya Marehemu Mzee Karume ilikuwa inakiogopa?
Nikijiuliza hayo maswali, ninafika mahali ninahisi kwamba Okello aliongoza mapinduzi na Mzee Karume kwa kuhofia kupinduliwa aliamua kumuondoa haraka sana ili asije akaleta balaa. Kama angekuwa "insignificant" wala serikali isingeingia gharama/usumbufu wa kumpeleka Kenya na pia asingeenda kukutana na Mwalimu Nyerere.
Few days ago kwenye uzi fulani nilisema kwamba Tanzania tumekuwa na utaratibu wa kuficha ukweli, na hiyo inaanzia kwa waandishi na mpaka kwa watawala. Watawala wetu wanataka waandikwe kwa mazuri tu, wakati kuna mabaya/mapungufu mengi ambayo yanafichwa na hivyo kupotosha historia na ukweli au kuishia kuleta mikanganyiko kama hii na kuwaacha wasomaji wakijiuliza je ni simulizi la nani ambalo lina-make sense?
Mkuu ni taswhishi ya kukipata kitabu cha Okello. Naweza kukipata wapi mkuu?naiunga mkono simulizi ya Mihangwa kwa kuwa ina supporting evidence. Pia zamani kidogo nilisoma kitabu Field Marshal John Okello ambacho kimezungumzia namna alivyoongoza mapinduzi, alivyokutana na Mwalimu na alivyotokomezwa. Pia nimesoma kitabu cha Masimulizi ya Thabit Kombo Jecha ambacho nacho kimempa credit Okello. Kwa mantiki hiyo, naiunga mkono simulizi ya Mihangwa. Huyo mwingine mpotoshaji tu!
Mkuu ni taswhishi ya kukipata kitabu cha Okello. Naweza kukipata wapi mkuu?
Makala za Mihangwa ziko kiukweli zaidi na ukitaka kuijua historia ya Zanzibar na mapinduzi yake hadi muungano kati ya Zanzibar na Tanganyika basi soma makala za Mihangwa.
Mkuu hiyo ni kweli. Ushauri mzuri sana huo. Kuna jamaa mmoja alikuwa akiitwa Lt. Maganga ambaye alishiriki kwenye jaribio la mapinduzi miaka ya 1980. Jamaa alikuwa akiandika simulizi za mpango wa mapinduzi hayo kwenye gazeti la Rai nikakutana naye nikamshauri atunge kitabu tukakubaliana lakini masikini bahati mbaya alikufa kabla hajautekeleza huo mradi.
Mihangwa aunganishe makala zake atengeneze kitabu. Si rahisi kukusanya makala zake zilizosambaa katika magazeti mbali mbali na kwa matoleo tofauti tofauti tena kwa muda mrefu.
mapinduzi ya zanzibar yalikuwa ni genocide hiyo inajulikana,lakini sioni sababu ya kurejesha mambo yaliyopitwa na wakati, hizo video sio za leo wala jana zimezagaa europe,lazima tujiulize kuonyesha video hizo zitaisaidia chochote jamii ya wazanzibar ambao wengi wetu hayo mapinduzi tunayasikia tu,tafakari
Mzee
Hii link yako inasema CCM siyo Chama Cha Mapinduzi bali ni ''Christian Church Movement'':
Quote :''This is a clear testimony that the union of Zanzibar and Tanganyika was the creation of Karume, a racist dictator nominal Muslim from Nyasaland (Malawi) and Nyerere, an autocratic devout Christian from Tanganyika. And consequently, Zanzibar has lost her strong Islamicity and sovereignty to Tanganyika since April 26, 1964 when the dictator Karume, signed the Articles of the Union, drafted by British expatriates, Attorney General Roland Brown and Chief Parliamentary Draftsman, P.R.N. Fifoot, to form Tanzania under the clique of the Christian Church Movement (CCM) of Tanganyika''.
Hivi wakereketwa wa CCM mnaikubali hii ? au ni Freemasons na Da Vinci Code?
..tatizo la Zenj linatokana na Sultani wa Kiarabu aliyetawala hapo kujihusisha na biashara ya utumwa.
..upumbavu mwingine waliofanya kuacha makazi yao Uarabuni na kuhamia moja kwa moja hapo Zanzibar.
..Waingereza na Wafaransa hawakuhamia moja kwa moja kwenye makoloni na kuzikana nchi zao za asili. hiyo iliwawezesha kujiondoa na kurudi makwao, na kuepusha shari na mauaji pale wenye nchi yao walipoanza kudai uhuru.
..Waarabu na mzao wao wamewakandamiza Waafrika hapo Zenj miaka na miaka na sijui walikuwa wanategemea mwisho wake utakuwa kitu gani.
..binafsi nasikitishwa na kilichotokea wakati wa Mapinduzi, lakini kwa upande mwingine sishangazwi.
Let's be fair na tuseme bila kigugumizi, kwa mkakati wa mkoloni hawa jamaa 'waarabu au washirazi na wafrika' walikuwa wanasoma shule za pamoja na walisomeshwa shule za kata yaani za hali ya chini. Lakini kwa nini wauane kwa kiasi hicho kinachosemwa kwenye video hii. Mi nilishaiona video hii ulaya lakini naomba tujihadhari na mbinu chafu za kimagharibi. Huwezi kuwa ulikuwa na helkopta ya kuchukua matukio halafu ukaacha watu wakateketea wakati una silaha. Pili kupiga picha kwa helkopta wakati wa vita isingewezekana hata kama wasingekuwa nayo hapa. Video ni uzushi mtupu wenye lengo la kuchochea uhasama miongoni mwa wazanzibari na watanzania kwa ujumla, tuikatae!mzigo wa mwenzako kwako ni ganda la usufi
kwa waliouliwa wazee wao na kwa wanaowaona wazee wao wamepoteza akili kwa kuuliwa waume zao kwa mapinduzi kwa sababu tu ya rangi yao na kwa walioingiliwa dada zao na kwa waliozaliwa kwa wazee wa ubakaji na kwa mateso yaliyotangulia mpaka siku za uchaguzi za hivi karibuni , mapinduzi yanabaki ni jinamizi kubwa lisilosahaulika
Let's be fair na tuseme bila kigugumizi, kwa mkakati wa mkoloni hawa jamaa 'waarabu au washirazi na wafrika' walikuwa wanasoma shule za pamoja na walisomeshwa shule za kata yaani za hali ya chini. Lakini kwa nini wauane kwa kiasi hicho kinachosemwa kwenye video hii. Mi nilishaiona video hii ulaya lakini naomba tujihadhari na mbinu chafu za kimagharibi. Huwezi kuwa ulikuwa na helkopta ya kuchukua matukio halafu ukaacha watu wakateketea wakati una silaha. Pili kupiga picha kwa helkopta wakati wa vita isingewezekana hata kama wasingekuwa nayo hapa. Video ni uzushi mtupu wenye lengo la kuchochea uhasama miongoni mwa wazanzibari na watanzania kwa ujumla, tuikatae!
Mzee
Hii link yako inasema CCM siyo Chama Cha Mapinduzi bali ni ''Christian Church Movement'':
Quote :''This is a clear testimony that the union of Zanzibar and Tanganyika was the creation of Karume, a racist dictator nominal Muslim from Nyasaland (Malawi) and Nyerere, an autocratic devout Christian from Tanganyika. And consequently, Zanzibar has lost her strong Islamicity and sovereignty to Tanganyika since April 26, 1964 when the dictator Karume, signed the Articles of the Union, drafted by British expatriates, Attorney General Roland Brown and Chief Parliamentary Draftsman, P.R.N. Fifoot, to form Tanzania under the clique of the Christian Church Movement (CCM) of Tanganyika''.
Hivi wakereketwa wa CCM mnaikubali hii ? au ni Freemasons na Da Vinci Code?
Kama mpaka sasa hivi waarabu Hapa Zanzibar wanatubagua namna hii, je yasingefanyika mapinduzi maisha ya sisi waZanzibar weusi yangekuwaje?
Marafiki zangu wa karibu sana wapo waraabu na Wazanzibar.. Niliwahi kuwauliza maswali machache tu husiana na video hii ya Mapinduzi ambayo nijuavyo mimi ilitengenezwa kwa minajiri ya sinema lakini wameigeuza kuwa ukweli na matukio halisi. Nawaombeni muitazame tena vizuri na kutafakari ukweli ni upi haswa na nini lengo la hizi filamu..Maswali yangu ni haya:-Ukitaka kuwajua waarabu na mambo yao angalia picha za watumwa. Yale maminyororo huwa sipendi hata kuyaangalia